(Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917
{{ SEHEMU YA 26 }}
#Endelea_nayoo==>Rocky sasa alianza kuwaweka kwenye target majangiri mmoja baada ya mwingine.......
Laizer pamoja na maaskari wake bado walikuwa wakiendelea kuwa na subira....
Maaskari wao walikuwa wakisubiri ruhusa kutoka kwa Laizer...........
Laizer naye alikuwa kashika bunduki yake ya usiniper akiwa anawaangalia majangiri wake kupitia lenzi iliyopo katika bunduki yake hiyo wakati anamtazama kiongozi wa majangiri ambaye ni Michael alishangaa kumuona Michael akianguka chini........
Wakati akiwa bado yupo katika kutazama kupitia lenzi yake hiyo aliweza kuona tena jangiri wa pili akianguka huku hawa wengine saba waliobaki wakakimbilia katika vichaka.......
Laizer akajua sasa hapa kuna sniper katika msitu huo hakusita kuwaambia asikari wake kupitia zile microcheap za masikion.........
"nadhani mnashuhudia kuna mdungaji kwa hiyo tukienda kichwa kichwa kuna msala huko utatutokea kwahiyo endeleeni kuwa wapole"
Laizer alimaliza kutamka maneno hayo.....
Juu ya mti Rocky aliweza kudungua majangiri wawili walipeana tano yeye na Lisa kwa kuona wamefanikisha swala zima la kupunguza maadui zao......
Wakati wanaendelea kupongezana Rocky akaona aangalie tena huenda wamerudi ili aendelee kuwapunguza....
Na kweli aliweka jicho lake katika lenzi ya bunduki yake aina ya sumraki akaweza kuona majangiri watatu wamejitokeza katika ile sehemu ya wazi wakati anaendelea kuwatazama alishangaa kuona wote watatu wakianguka na kufa pale pale alishtuka akaona sasa kuna mkubwa zaidi yake.......
Aliyewaangusha majangri wale hakuwa mwingine ila Laizer....
Laizer aliwapiga haraka tena kwa speed ya ajabu alifanya hivyo makusudi ili kumtumia Rocky salamu kwamba na yeye yupo kama majangiri wataisha bado tu atakuwa na kibarua kingine......
Kwa mtu wa kawaida asingeelewa lakini Rocky alielewa hilo na akagundua kuwa ana kazi nzito hakusita kumwambia Lissa
"daaaah bado nina kazi nzito hata hawa majangiri nikiwamaliza
"kwanini tena?"
"kuna mtu kama mimi humu na amenitumia salamu kwa vitendo na nimemuelewa hebu tazama kwa darubini pale"
Lissa alinyanya darubini akaiweka kwenye macho yake aliweza kuona maiti tatu zimeongezeka katika ule uwazi waliokuwepo majangiri
"nani kawauwa wale? Mbona maiti ulizodunga zilikuwa mbili sasa hawa watatu wametokea wapi?"
"na ndio maana nakuambia nina hali ngumu ya kugundua ni nani huyo aliyenitumia hiyo salamu"
Sasa majangiri wakiwa na kiongozi wao ambaye alikuwa ni kiongozi msaidizi wa Michael ambaye walifanya tukio la kuunguza moto nyumba ya Rocky hakuwa mwingine alikuwa ni Steveni swahiba wake mkuu na Michael yeye aliyekuwa kachukua nafasi ya Michael na sasa alibakiwa na majangiri watatu huku yeye akiwa ni wa nne alianza kwa kuwaambia......
"sikieni pamechafuka humu sahivi cha msingi turudini wilayani tukajipange maana huyu jamaa ni kama mzuka hafai kabisa"
Majangiri wale hawakuwa na neno walifuata kiongozi wao anavyosema wakaanza kukimbia kurudi walipotokea.....
Laizer aliwaona hivyo hakuwa na shaka akawapa maasikari wake maelekezo ya namna ya kufanya
"wakikaribia jitokezeni muwaweke chini ya ulinzi"
"sawa mkuu"
Steveni akiwa na kundi lake la majangiri wakirudi walipotokea awali ili wapande gari na kurudi wilayani walistaajabu Maaskari watano wakijitokeza mbele yao kisha kwa pamoja wakasema
"mpooo chini yaa ulinzi"
Lilikuwa ni tukio la ghafla hivyo hawakujiandaa kwa lolote na hawakuwa na jinsi walinyoosha mikono juu......
Walishangaa kumuona mtu wa sita akitokea nyuma ya mti wa mgunga akiwa na silaha.....
Kisha mtu huyo akaongea
"vijana lazima mkanyee ndoo naomba maafande wanne wabaki hapa kila mmoja amrinde wa kwake na mmoja anifuate"
Laizer akawa anasonga mbele kwa kujibanza katika miti huku naye askari akifana vivyo hivyo..........
Walifika katika ule usawa wa wale majangiri walipokuwepo pasipo kuonekana na wakina Rocky.....
Rocky bado walikuwa wapo juu ya mti yeye pamoja na Lissa.......
Bado alikuwa na wasiwasi wa kushka kutokana na kutoelewa adui yake atakuwa upande gani....
Laizer alifika mpaka kwenye maiti ya Michael na aliweza kuona jeraha katika paji........
Hakutaka kufuatilia alitoa miwani yake na kuivaa miwani ambayo ilikuwa na uwezo wa kuona sehemu yoyote ambayo ilikingizwa na kitu chochote alipotazama kila kona kwanza aliona hema ambalo ni kama lilitelekezwa hapo kitambo...
Alitazama mpaka kwenye miti na aliweza kuona watu wawili na mmoja ni kama alikuwa akitumia lenzi ya kwenye bunduki kuangalia kama kuna usalama......
Ndipo Laizer naye aliweka target huku yeye akiwa anamuona adaui yake lakini yeye akiwa haonekani na adui yake....
ITAENDELEAAAAAA.....
Nini kiliendelea kwenye chuma hiki je Laizer alifanya maamuzi gan?