Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 25

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 25 }}
#Endelea_nayoo==>Majangiri wale walipofika umbali wa kilomita moja Laizer pamoja na asikari wake wakapeana ishara za kuwafuatilia kwa nyuma..........
Michael pamoja na majangiri wake hawakujua kama maadui zao wamewaacha kwa nyuma........
Laizer na maaskari wake wakiwa bado wanaendelea kuwafuatilia majangiri hao ghafla Laizer akawapa ishara Askari wake kujibanza nyuma ya miti mikubwa ya migunga kilikuwa ni kitendo cha haraka sana na maaskari wakafanya kama mkuu wao alivyowataka wafanye kisha Laizer akaongea kupitia Microcheap za mawasiliano.....

"maafande wote mfuate nitakachowaambia ni kuwa msije mkafanya mistake hata kidogo kuna mitego eneo hili kuweni makini"

"sawa mkuu"

Michael pamoja na majangiri wake hata hawakuwa na wasiwasi waliendelea kusonga mbele zaidi huku wakiwa wameweka silaha zao tayari kwa mashambulizi.....
Rocky akiwa pamoja na Lissa juu ya mti mkubwa uliozongwa na matawi yaliyopambwa na majani ya kijani aliweka tayari silaha yake ya udungaji ambayo ni Sumrak Slvk-14 kisha akaweka jicho lake kwenye binocular yaani ile lenzi ya kwenye bunduki yake.....,.. Aliweza kuona kundi kubwa la watu wakiwa katika eneo la mitego waliotega kwaajili ya kukamatia nguruwe pori........

"lissa hebu njoo hapa uangalie kwa kutumia darubini"

Lissa alitii akasogea sehemu aliyoambiwana na Rocky akaweka darubini machoni mwake na kuangalia usawa wa mbalii

"hawa watu wote wana silaha wanataka nini humu ndani ya msitu"

"sijajua kwa kweli nahisi wananifuatilia mimi ngoja tuone mwisho wao"

Michael alisita kidogo baada ya kuona kamba ndogo ya mnyira/manyira kisha akamuita kijana wake mmoja........

"Heeey Henry?"
"ndiyo mkuu"

"naomba uje ukaniletee ile manyira pale niichunguze ni ya lini"

Laizer pamoja na maaskari wake walikuwa wakishuhudia yote hayo wakiwa wameachana kwa hatua kama ishirini na majangiri wale...... 
Jangiri yule anayeitwa Henry alisogea mpaka pale paliposadikika kuonekana kuwa kuna manyira.....
Rocky alijikuta akitabasamu tu kwani aliweza kushuhudia jangiri yule akisogelea kifo ambacho kitaondoka na wenzie watano......

"acha leo tukose nyama siku moja sio mbaya uwongo mamaa?"

"kweli sio uwongo dear"

Kweli yule Henry alisogelea ile kamba ya manyira na bila kufikiria akaivuta ile kamba kama anaiokota ili ampelekee mkuu wake.......
Mara Kukuru kakara mtego ulifyatuka na miti iliyokuwa imechongwa kama misumari iliweza kuwajeruhi majangiri wawili huku wanne wakiwa ni maiti........ 
Michael kuona hivyo akapayuka kwa sauti kubwa 

"mwageni risasi kila pande"

Kweli majangiri hawakuwa wakijua mbinu ya kujikinga na hatari na wao wakafuata kama alichosema mkuu wao risasi zilikohoa ndani ya msitu huo kwa dakika tano.... 

"stoooop"

Ni kauli ya kuamrisha kutoka kwa Michael ili majangiri wake waache kupiga risasi.....
Laizer akiwa na kikosi chake alitulia tu kuona majangiri wa Michael watafanya nini je watasonga mbele ama watarudi nyuma.....
Ili kama wakirudi nyuma wawarushie risasi za kutoshaa......
Rocky alishuhudua kila kitu halafu akatamka neno la kizungu

"it's show time"ni muda wa kuonyesha"

Lissa alikuwa kimya tu akitazama kwa darubini aliwaona majangiri waliobaki akawa anawahesabu 

"wamebaki wangapi?"

Lilikuwa swali la Rocky kuhusiana na idadi ya majangiri waliobaki 

"wamebaki tisa"
"okay kazi ndogo"

Michael sasa alikuwa akiwapanga vijana wake huku yeye akiwa kama muheshimiwa waziri akawafanya majangiri wake kama mabodyguard wake.....
Laizer na maaskari wake walikuwa wamejituliza tu kwani kile ambacho kundi mbili wanakitafuta hawajakifikia bado......
Rocky sasa alianza kuwaweka kwenye target majangiri mmoja baada ya mwingine
ITAENDELEAAAAAAAA.....

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.