Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 24

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 24 }}
#Endelea_nayoo==>DEFFENDER ililisogezwa na maaskari hao watano pamoja na Laizer wakapanda na safari ikaanza....
Upande wa bwana Jamali naye hakupteza muda kuandaa vijana wake ambao waliingia ndani ya gari lijulikanalo kama NOAH yenye rangi nyeusi......
Laizer pamoja na askari wa kitengo cha F.F.U sasa walitimu ndani ya msitu kisha gari/deffender lao likaweza kurudi kituoni.....
Dereva wa gari hilo la kituo cha polisi aliweza kuona kwa mbali gari aina ya NOAH yenye rangi nyeusi ikiwa inaelekea usawa ambao ametokea hakusita kutumia michrocheap ambayo amepewa na Laizer kwaajili ya mawasiliano

"haloo kiongozi wa mission unanipata?"

"ndiyo nakupata kuna tatizo?"

"ndiyo mkuu nayaona manjembaa yanakuja na gari aina ya NOAH kuweni makini mkuu"

"sawa sawa"

Kisha akaendelea kuwa makini na usukani wake....... 
Dereva wa gari lile aina ya NOAH aliweza kuona gari la jeshi la polisi akawashtua viongozi wake.....
Nao viongozi wakajadiliana kisha Michael ambaye alikuwa ni kiongozi mkuu akawageukia vijana wake na kuwaambia

"sikieni kuna gari la polisi naona linarudi baada ya kupeleka askari sasa inatakiwa tulishambulie jenyewe kwanza ili lisije likarudia askari wengne tukazida si mnaliona haya jiandaeni"

Dereva wa gari la NOAH akaanza kupunguza mwendo naye dereva wa gari la DEFFENDER Kuona vile akajua kwa vyovyote kuna kitu kinataka kutokea akakanyaga mafuta ili kuongeza mwendokasi dereva wa NOAH kuona vile akasimamisha kabisa gari kando ya barabara kisha majangiri yale ya kwenye gari la NOAH yakashuka huku mikononi yakiwa yamebeba bunduki aina ya S.M.G 
(sub machine gun)......
Na kabla dereva wa DEFFENDER hajafika majangiri yale yakaanza kurusha risasi kwa fujo.....
Dereva wa DEFFENDER hakuwa lena katika kucheza na usukani alizikwepa risasi hizo kwa kukimbiza gari kwa mwendo wa zing zang yaani mwendo wa nyoka.....
Wakati majangiri wale walipokuwa wakirusha risasi ndani ya pori kina Laizer waliweza kusikia sauti za risasi hizo achilia mbali na kina Laizer kusikia sauti za risasi hizo hata Rocky pamoja na Lissa waliweza kuzisikia pindi walipokuwa wakitega mitego yao ya kunasia ngurue pori pamoja na wanyama wengine wa kuliwa kama digidigi,swala na sungura......
Dereva wa DEFFENDER aliweza kuepuka kizuizi kile lakini Tairi moja la upande wa nyuma likawa limetusuliwa na risasi kwa hiyo alikuwa akitembelea limu tu....
Baada ya risasi kuacha kurindima aliweza kuisikia sauti ikiongea katika microcheap yake ya mawasiliano,........

"afande nini huko mbona sauti za risasi tena?"

"manjemba wamenirushia risasi nusura nife mkuu kuweni makini sahivi hapa nawaona kwenye side mirror wapo wengi sana kutuzidi sisi na sasa nawaona wameingia ndani gari lao wanakuja huko"

"sawa sawa afande"

Michael ambaye ndiye kiongozi mkuu wa majangiri wale aliwaambia vijana wake

"tuondokeni fasta nimepata mawasiliano kwamba kuna askari watano tu ndani ya huu msitu kwahiyo haitakuwa kazi kuwamaliza twendeni"

Wakaingia ndani ya gari na safari ikaendelea.......
Upande wa Laizer pamoja na kikosi chake waliingia ndani zaidi ya pori hilo akawa anawapatia maasikari wake maelekezo

"sikilizeni maafande hapa tupo vitani kwahyo ni kupona ama kufa ila mkifuata maneno yangu mtapona wote watatu waende upande ule na wawili wabaki na mimi msishambulie kama sijatoa ishara nadhani tumeelewana"

"ndiyo mkuu"

Maafande hao Wakafanya kama Laizer alivyowaelekeza..
Rocky na Lissa sasa wakawa wameingiwa na hofu ni baada ya kusikia sauti za risasi zikiwa zinanung'unikia ndani ya mstu waliokuwa wakiishi

"au majambazi wanawindana na maasikari humu?"

"huenda ikawa hebu twende kwanza kwenye hema letu kuna kitu nataka nifanye"

Yalikuwa ni maongezi ya Lissa na Rocky na ni Rocky ndiye aliyemuambia Lissa waondoke mahali hapo.........
Baada ya kutumia dakika kumi nzima kuelekea katika hema lao waliweza kufika naye Rocky akaingia ndani moja kwa moja akafikia kibox chake kile cha chuma kisha akakifungua akatoa bunduki yake ya udungaji na
kuanza kuipanga Bunduki hii
ilitengenezwa Urusi ni bunduki ambayo ilifanya mauaji ya wale wazungu wawili waliokuwa wakihamishwa kituo cha Masaki kwenda kituo kingine.........
Ni hiyohiyo bunduki iliyopoteza uhai wa Rais Markdaniel....
Rocky alipomaliza kuipanga akamgeukia Lissa ambaye alikuwa bado kataharuki hakuamini kama Rocky siku zote angemficha siri ya kumiliki bunduki........
Akatoa na darubini pamoja na bastola iliyokuwa humo humo kwenye hicho kibox kisha akamkabidhi Lissa

"twende kule kwenye ule mti mkubwa"

Lissa alifuata jinsi Rocky anavyomuambia walifika kwenye ule mti wakakwea juu Rocky akawa anampa Lissa Maelekezo...
Kundi la Michael lilifika ndani zaidi ya msitu huo......
Kina Laizer walikuwa wanawachora tu na wakawaacha ili waende mbele zaidi.....
Walipofika umbali wa kilomita moja Laizer pamoja na asikari wake wakapeana ishara za kuwafuatilia kwa nyuma
ITAENDELEAAAAAAAAA.....
Haya sasa mambo yamewivwa kutatokea nini huko mbele

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.