Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 23

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 23 }}
#Endelea_nayoo==>Aliingia hata bila wasiwasi huku furaha yake ikiwa imejidhihirisha usoni pake.......
Alivuta kiti na kukaa kisha akampatia Laizer Maji hayo aliyotumwa Laizer naye hakusita kumuuliza swali

"vipi sergeant mbona una furaha sana"

"kawaida tu Laizer nafurahi sana kuona tumefanikisha hili swala"

"okay usijali na nitahakikisha nipate mpaka matawi"

Kisha Laizer akatabasamu kinafki.......
Seargeant Edwine aliondoka ndani ya chumba lakini hakujua kama alishashtukiwa na Laizer............
O.C.D Bihamunuro alimstikitia askari wake huyo kwa kutokuwa mzarendo wa nchi yake.... 
Laizer alianzisha maongezi ili kumtoa O.C.D Bihamunuro katika lindi la kuwaza 

"usiwaze mkuu kinachotakiwa ni kumuacha afanye tu analofanya nasi inatakiwa tujiandae kwenda huko porini kwa kuwa ramani tunayo hatuna shaka naomba uniandalie vijana watano muheshimiwa"

"okay sawa Laizer nitafanya hivyo"

Wakati wanaendelea kuongea mara ghafla wakasikia sauti katika komputa ilibidi watulie wasikilize kwa makini

"upo nyumbani si ndio basi napita usiondoke andaa vijana muingie humo pori kabla jamaa hajawahi maana yule ni mtu wa machale sana"

"sawa Edwine nitafanya hivyo sasa niandae vijana wangapi?"

"maana nahisi kwa vyovyote vile O.C.D wangu ataandaa askari kumi kwa hiyo we andaa vijana kumi na watano ili muweze kuwadhibiti mapolisi"

Maneno yote yale yalisikiwa na Laizer pamoja na 
O.C.D Bihamunuro na yote ni kwa sababu seargeant Edwine hakutoa ile noti aliyopewa na Laizer akanunue Maji....

"ina maana hakutoa ile noti niliyompatia aisee kweli mjinga ni mjinga tu"

Ni maneno ya mshangao aliyoyasema Laizer..........
Upande wa Jamali alifurahi sana pembeni mwake walikuwepo vijana wawili alijikuta akiropoka kwa furaha iliyokuwa na ujazo wa tani mia

"kazi imeisha vijana wangu kwahyo raundi hii msirudie makosa leo hamtakuwa nyie tu nitawaongeza vijana wengine kwenye hii kazi huku nyie mkiwa ni viongozi wao wewe Michael utaongoza vijana 13 na wewe Steven utaongoza vijana 12"

Akachukua simu na kuanza kuwatumia vijana wake ujumbe......
Kituoni O.C.D Bihamunuro aliandaa askari wake watano aliokuwa akiwaamini mwanzo alitokea kumuamini sana Edwine sasa hamuamini tena.....
Laizer ndiye aliyekuwa kiongozi wao mkuu wa kuwaongoza katika mission hiyo....

"mguu pande,mguu sawa,nyumaa geukaa, nyumaa geukaa haya tulieni kusikiliza wito wa ghafla tuliowaitia"

Yalikuwa ni maneno ya O.C.D Bihamunuro aliyowaambia vijana wake wa kitengo cha Field Force Unit (F.F.U) ambao walikuwa katika paredi ya kituo cha polisi....... Kisha akaendelea kuongea.

"wito huu niliowaitia ni kuhusu kwenda katika operation ya kufichua maovu ambayo yamefichika ni kwamba leo kwanzia sasa naomba vijana watano ambao nitawataja muweze kupita hapa mbele Zephania,Omary,Muhamed,Charles pamoja na Frank nyie wengine naomba mtawanyike nibaki na hawa watu" 

Maaskari wengine wakatawanyika kisha Laizer akasogea mbele ili kuongea machache 

"najua mnawaza sana msiwaze maafande hii ndo kazi yenu ya kutetea maslahi ya nchi yenu hivyo basi mkiwa na sare zenu hivohivo tutaondoka kuelekea katika msitu uliopo jirani na wi nawaomba mmoja baada ya mwengine aje hapa mbele niwapatie microcheap za kuwasiliana"

Laizer alitoa vicheap vidogo akawa anawawekea maaskari hao masikion.....
Gari likaandaliwa kwa ajili ya kuanza safari ya kuelekea katika msitu huo...,
ITAENDELEA.......

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.