(Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917
{{ SEHEMU YA 22 }}
#Endelea_nayoo==>Laizer alipozima simu.....
Akatazama tena kompyuta kwa kuwa alijua namna ya kucheza na programe alifungua programe yake aliyokuwa ameipa jina la #spycaller akafungua kisha ikawa inampa maelekezo...........
General Brown aliporudia kuipigia tena simu ya Laizer lakini aliambulia patupu....
Akaona afuatilie location ya Rocky inaposomeka alifurahi sana kwani hapakuwa mbali na igunga ndipo alipompigia simu Bwana Jamali ambaye ndiye mtu aliyempatia kazi hiyo....
Laizer sasa akawa na kazi ya kudukua mawasiliano ya General Brown muda ambao Brown alikuwa akimpigia bwana Jamali ndo muda ambao Laizer alikuwa akidukua mawasiliano yake pasipo yeye kujua katika programu ya Laizer lilikuja neno linalosomeka #record_caller aliibonyeza kisha ikanzaa kuhesamu dakika............
General Brown hakujua kama anadukuliwa mawasiliano yake alianza kuongea pindi simu yake ilipopokelewa na Jamali
"Haloo Mr Jamalii nakupa chance ya mwisho yule kibaraka hayupo mbali na hapo Igunga ni katika pori lililopo jirani tu sasa nitakutumia whatsapp ramani ya pori hilo pamoja na sehemu aliyopo mtu huyo"
Haakuongea maneno mengi sana kisha akakata simu.....
Upande wa Laizer komputa yake ilimletea maneno yaliyosomeka #_Audio_done_play..........
Alibonyeza neno play akaanza kusikiliza yalikuwa ni yaleyale maongezi ya Brown na Bwana Jamali na ilipofikia sehemu ya general Brown kumwambia Jamali kuwa atamtumia ramani Bwana Jamali Laizer akaona hapa sio pa kupoteza muda moja kwa moja akafungua programe yake ingine tena iliyokuwa inaitwa #Hacking_social_network kisha ikamuomba namba akaingiza ile namba ya general Brown wakati anafanya yote hayo
O.C.D Bihamunuro pamoja na Sageant Edwine walikuwa wakimtazama lakini Seargent Edwine alikuwa akibonyeza bonyeza simu yake sijui kwanini...........
Laizer alikuwa akiparangana mpaka pale alipoweza kuona picha iliyotumwa kwa Jamali picha iliyokuwa na muundo wa jpg alifungua na aliweza kuona ramani yote ya wilaya ya igunga na akaona kuna sehemu imewekwa kidoti kuonyesha mahali pale kuna kitu ambacho kilitakiwa kifuatwe mahali pale............
Akaweza kuona pia chatting za Gener Brown pamoja na Jamali
"naomba usikosee Jamali ni muhimu mtu huyo apoteze maisha maliza kazi ili tuende wote mimi na wewe Marekani tukapumzishe akili"
"sawa Brown usijali nitapambana mpaka nione tone la mwisho la damu yangu ili huyo kibaraka apotee
"nitashukuru sana acha nikutakie kazi njemaa"
Laizer alitabasamu kuonyesha ushindi upo upande wake akamgeukia O.C.D Bihamunuro kisha akamwambia
"mambo yamewiva naomba uandae vijana tukafanikishe misheni hii sio kesho ni leo leo tukaingie katika pori lililo jirani na wilaya hii ya Igunga"
O.C.D Bihamunuro hakuamini masikio yake alifurahi kwa kumpigia makofi.......
Seargeant Edwine alinyanyuka na kutaka kutoka nje ila Laizer alimuita
"samahani Seargeant naomba unichkulie vocha ya elfu mbili hapo nje"
Huku akiitoa noti ya shilingi elfu kumi iliyokuwa imekunjwa kunjwa na kumpatia seargeant Edwine.....
Naye Seageant Edwine alipokea na kuweka katika mfuko wa shati pasipo kukunjua noti hiyo na moja kwa moja akatoka nje.......
Ndani walibaki Laizer na
O.C.D Bihamunuro kisha Laizer akaanzisha maongezi
"unajua huyu kijana wako simuamini"
"kwanini Laizer?"
"we subiri dakika kadhaa utaniamini tu"
Seargeant Edwine alipofika tu nje alimpigia simu Bwana Jamali..........
"eeeeh Jamali jamaa amedukua mawasiliano yako wewe na Brown kwahiyo ahirisheni kwenda kesho nendeni leo leo mumfuatilie huyo mtu mmalizen kabla mambo yenu hayajabumburuka"
"sawa Edwine ukitoka hapo pitia mzigo wako umenifurahisha sana"
Kisha Seageant Edwine akakata simu huku akiwa na na furaha kuwapa taarifa watu wake na moja kwa moja akaeleke dukani huku akiwa na furaha yake moyoni akasahau hata kutoa ile noti aliyopewa na Laizer badala yake akatoa Wallet yake na kutoa noti moja ya elfu kumi kumpatia muuza duka.....
Kituo cha polisi Laizer na Bìamunuro walikuwa wakisikia maongezi yote yale ya Edwine pamoja na bwana Jamali kwani Laizer alipompatia Edwine noti aliyokuwa kapachika kinasa sauti kidogo ambacho kilihitaji mtu makini sana kugundua.....
Seargeant Edwine alipopatiwa maji alinyoosha mpaka kituo cha polisi katika chumba alichowaacha Laizer pamoja na O.C.D Bihamunuro aliingia hata bila wasiwasi
ITAENDELEA...........
Sasa sijui itakuwaje hapoo
hebu usikose Muendelezo.....