Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 19

TRIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 19 }}
#Endelea_nayoo==>Akazoom kwa ukaribu kabisa likatokea jina liitwalo Nanga Igunga alipiga makofi kwa kuona kuwa amefanikiwa wakati akiwa katika furaha yake simu yake ya mkononi iliita akapokea na maongezi yakaanza

"haloo nani mwenzangu"

"mr Jamali hapa naongea yule mtu tuliyeongea pale 
New Sun Rise hotel"

"ooh Jamali sawa sawa nimekupata naomba tukutane pub moja inaitwa 
Dark Night Pub tuweze kuchonga zaidi"

"sawa Brown usijali baada ya nusu saa nitakuwa hapo"

Kisha simu ikakata.........
Katika chumba cha Komputer Laizer sasa alikuwa akihangaikia kupata taarifa kamili kuhusuana na hiyo picha iliyotokeza katika komputer yake alicheza sana na komputer nia ni kutaka kujua ilikuwaje mmarekani huyo aishi katika nchi ya Tanzania ili kujificha pasipo kujua mambo yake ya nyuma ya pazia.....
Wakati anaendelea kuchakata komputer yake lilikuja neno lililosomeka kwa lugha ya kizungu

"Notification of this person has broked try to make communication with administration call number +123 55 88 9 for privet help"

Laizer aliinukuu namba ile pembeni ili aipigie..............
General Brown aliweza kukutana na bwana Jamali....
Wakaongea maneno yao hayo

"Jamali yule kibaraka yupo Nanga Igunga unapajua?"

"Ndiyo napajua hiyo sehemu nina migodi ya dhahabu nanga ni kijiji na Igunga ni wilaya kwahiyo ulikuwa unatakaje?"

"Nataka tumpoteze duniani tutaenda wote Igunga ntakuoyesha ilipo nyumba yake" 

Kisha General Brown akatoa bahasha ya rangi ya Kaki halafu akampa Bwana Jamali 

"hizo ni hela ndogo tu ni millioni tatu kwaajili ya kujiandaa kwenda safari ya Igunga ila ukifanikisha ntakupatia milioni 20"

"sawa nimekuelewa Brown hakika nafanya kazi na mtu mzito"

Waliendelea kunywa pombe huku wakisindikizwa na nyimbo nzuri za kukonga nyoyo zao baada ya muda kila mmoja alitoka na kuingia ndani ya gari yake........
Asubuhi palipokucha bwana Jamali alijiandaa kwaajili ya safari ya mkoani Tabora akaona njia bora ni kuondoka na gari lake alimpigia simu General Brown na waliweza kuonana na moja kwa moja wakapanda ndani ya gari la bwana Jamali na safari yao ikaalianza.......
Dereva alikimbiza speed ya fast and Furious alivuka vituo vingi na sasa alikuwa amebakisha mikoa miwil tu Dodoma, pamoja na Singida.....
Baada ya masaa kama 5 walifika wilaya ya Igunga wilaya yenye utajiri wa dhahabu pamoja na umaarafu wa ulimaji wa pamba.......
Walitafuta Lodge nzuri kwaajili ya kupumzika ili asubuhi patapokucha waamkie katika kijiji cha Nanga.... 
Walipokuwa wakipata chakula cha usiku General Brown alianzisha maongezi

"sasa kesho tutakapoenda sitotaka huyo kibaraka anione ila nitakuonyesha mahala anapoishi"

Alisema Brown naye Jamali hakupinga walikubaliana pasipokuwa na maneno.....
Na kila mtu aliondoka kwenda kupumzika.......
Palivyokucha wakaweza kuondoka kwenda katika kijiji cha Nanga...
Hapakuwa mbali sana ni kama kilomita 10 tu..
Gari lilipokuwa kasi General Brown alikuwa bize na laptop yake akitazama 
Location/mahali ambapo Rocky alikuwa akiishi ramani ilikuja ilionyesha kuwa wamekaribia kidogo tu wafike mahali alipokuwa akiishi Rocky..,.....
Baada ya Dakika kama kumi General Brown alimwambia dereva kuwa asimamishe gari kando ya barabara kwani jinsi ramani inavyoomuonyesha kwenye laptop yake anaona tayari wamefika
ITAENDELEAAAA
Hapo vipi nimeirefusha hii story nadhani mashabiki zangu mtafurahia.......
ina maana General Brown ndo kaona nyumba ya Rocky? Hebu usikose sehemu ifuatayo ya riwaya hii....

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.