Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 18

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 18 }}
#Endelea_nayoo==>"eeeh bwana Jamali bado naendelea kuwa beneti na huyu Laizer kwahiyo nitakuwa nawajulisha kila kinachoendelea"

"okay basi itakuwa vizuri maana nilihisi umenisusa kwahiyo ukitoka hapo upitie mzigo wako nyumbani kwangu"

Maongezi yao yakaisha halafu akarudi ndani kuendelea na mpango aliouacha ukiendelea alipofika tu.....
Aliweza kumuona Laizer akihangaika kupata data za mtu ambaye alikuwa akiishi kwenye ile nyumba iliyoungua na moto...
Alihangaika sana baada ya nusu saa nzima iliweza kutokea picha kubwa iliyokuwa imeandikwa kwa chini tena kwa lugha ya kiingereza katika kioo cha komputer...

"he is black America"

Jibu hilo lilimshangaza kila mtu katika chumba kile maalumu cha tarakishi za kudukua mawasiliano pamoja na data....
Sergeant Edwine alijikuta akiuliza swali kwa mshangao

"ina maana huyu ndo muhanga wa ile nyumba iliyoungua moto?!!!"

Swali ambalo hakuna aliyejishulisha kumjibu Laizer aliendelea kuchakata computer......
Turudi Marekani
General Brown bado hakukata tamaa......
Alitaka kuhakikisha ushahidi unapotea kabisa kitendo cha Rocky kuendelea kuvuta pumzi ya dunia ni sawa na yeye kuendelea kujiweka matatizoni........
Aliamua kujiandaa kwa ajili ya safari ya kuingia nchini Tanzania kwa mgongo wa kuwekeza mradi wa ufugaji wa kuku wa kisasa 
Rais wa nchi ya Tanzania alimpokea General Brown
kwa mikono miwili pasipokujua nia halisi ya mtu huyo........
Siku moja General Brown akiwa yupo katika 
New Sun Rise Hotel ndipo alipoweza kuonana pamoja na kujuana na bwana Jamali ambaye alikuwa akilindwa na mabodyguard wake 
General Brown alimsogelea na kumsalimia......

"kwema ndugu nimependa mabodyguard wako wanavyokulinda naweza kuongea nawe kidogo?"

Bwana Jamali alitabasamu tabasamu ambalo alijiona yeye ni mshindi kusemeshwa na mzungu yule...
Alimkaribisha 

"usijali karibu sana sijui ulikuwa na maongezi gani?"

"Ahsante kwa kunipa nafasi hii kwa Majina yangu ni Brown Karly ni mfanyabiashara mkubwa sana Marekani na nimekuja kwenye nchi hii kuja kuwekeza mradi wa kuku wa wa kisasa lakini kuna mfanyabiashara mwenzangu naona ananikwamisha kwa kuniwekea kizingiti na sijajua ni kwanini kuna kibaraka chake kimoja tu ndo kinasumbua akili yangu"

Maneno yote aliyoyasema General Brown ni ya kujitungia hayakuwa na ukweli wowote aliyasema tu ili kumshika masikio bwana Jamali..... 
Bwana Jamali kabla hajatia neno lolote General Brown aliendelea

"naomba kufanya kazi na wewe ukinisaidia kummaliza huyo kibaraka wa tajiri mwenzangu nitakupa kiasi kikubwa sana cha pesa ili kudhihirisha hicho nachokisema ngoja nikupe hii"

General Brown alitoa bahasha ya kijivu ndani ya Briefcase na kumpatia bwana Jamali............
Naye bwana Jamali alipokea na kutazama kilichopo ndani ya bahasha hiyo alistaajabu kuona pesa nyingi za kigeni zikiwa ni dola mia mia kisha akamtazama General Brown.... 
Alipotaka kuongea General Brown akadakia

"hizo ni pesa kidogo sana tafuta mahali tuongee mimi na wewe kama hutojali"

"okay usijali mr Brown niachie bussines card yako"

Wakapeana mawasiliano na kila mtu akafuata njia yake.......
General Brown alipokuwa katika nyumba aliyopanga alitoa laptop yake akaiwasha huku mawazo yake yakiwa ni kwenda kumtafuta Rocky ambaye alikimbilia nchini Tanzania kwaajili ya kujiepusha na wao....
Aliwasha laptop yake na moja kwa moja
akafungua programe aliyokuwa ameipa jina la 
#F.B.Imission ilipofunguka ilikuja ramani ya dunia huku ikionyesha ramani ya nchi ya Tanzania akazoom kwa ukaribu kabisa likatokea jina liitwalo Nanga Igunga alijikuta akijipigia makofi kwa kuona kuwa amefanikiwa  
ITAENDELEAAAAAA
Mmmmh sasa huyu General ameona nini? 
basi usikose Muendelezo wa riwaya hii...

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.