(Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917
{{ SEHEMU YA 16 }}
#Endelea_nayoo==>Sergeant Edwine alipokata simu alibaki akitafakari ni jinsi gani ya kumkwepa Bwana Jamali ambaye ni tajiri mkubwa anayemiliki migodi ya madini iliyopo Igurub na anamiliki genge kubwa la uharifu.......
Michael na Steven walipofika nyumbani kwa bosi wao bwana Jamali walimueleza jinsi kazi itakavyokuwa ngumu bosi naye aliwaambia jinsi sergeant Edwine anavyotaka kuwageuka kutokana na ujio wa huyo mtu anayejiita Laizer........
Tukirudi upande wa pili wa Laizer asubuhi na mapema anajiandaa kwaajili ya kwenda katika eneo la tukio la nyumba kuchomwa moto wanaondoka yeye na
O.C.D Bihamunuro huku wakiwa beneti na sergeant Edwine wakati wapo ndani ya gari O.C.D Bihamunuro alianza kumpa maneno kijana wake huyo ambaye ni sergeant Edwine
"Edwine?"
"ndiyo mkuu"
"cheo changu cha O.C.D kilisababishwa na bwana Laizer Zuber kwa sababu nilipenda sana kufuatana naye kila kona anayokwenda na siku Rais alipokuwa anatunuku vyeo nami nikawa mmoja wapo kutoka ukoplo mpaka o.c.d huoni ni kwaajili ya Laizer kwahiyo kijana wangu fuatana sana na Laizer ili ufanikiwe"
"sawa nimekuelewa mkuu"
Safari iliendelea mpaka walipofika katika kijiji cha nanga......
Walishuka ndani ya gari na moja kwa moja Wakaingia ndani ya nyumba iliyokuwa imebaki pasipo na mapaa na yote sababu ya kuungua moto........
Walipofika tu ndani Laizer akatoa groves akazivaa pamoja na kinotibuku chake anachoandikia mambo yake.....,.
Akalitazama lile godoro lililotupwa pembeni ni kama alikuwa kang'amua kitu na kuamua kuandika....
muda wote alipokuwa akifanya mambo yake O.C.D Bihamunuro pamoja na Sergeant Edwine walikuwa wakimtazama tu kile ambacho Laizer alifanya.....
Laizer alitoa mfuko wa nailoni kisha akamgeukia
O.C.D Bihamunuro
"umeona hilo dongo lililogandia hapo kwenye godoro?"
Aliuliza Laizer huku akimuonyesha kwa Kidole
O.C.D Bihamunuro donge kubwa ambalo limeng'angania kwenye godoro.......
"ndiyo nimeliona"
"umegundua nini Mkuu?"
O.C.D Bihamunuro akawa kimya kidogo kisha akajibu wakati wanaongea Sergeant Edwini alikuwa kimya huku akirekodi maongezi ya Laizer na O.C.D Bihamunuro pasipo wao kujua............
O.C.D hakuwa na jibu la kumpa Laizer hivyo basi Laizer akamjibu
"Kwa kuwa swali langu gumu acha nikujibu mwenyewe"
ITAENDELEAAA........
Mimi naona ndo kwanza story imeanza kwanini Laizer amegundua uwepo wa dongo hilo kwenye godoro na kwanini sergeant Edwine anarekodi maongezi ya Laizer na O.C.D Bihamunuro mmmmh mimi sijui naomba tukutane sehemu ifuatayoi usikose Muendelezo wa riwaya hii...