Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 15

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 15 }}
#Endelea_nayoo==>O.C.D Bihamunuro alimkaribisha Laizer kwa furaha tele pamoja na bashasha kisha akaongozana naye mpaka kwenye gari lake maasikari wao waliwapisha ili waingie katika gari.........
Laizer akiwa kavalia miwani yake pamoja na saa yake mkono wa kushoto kabla hajaingia katika gari hilo la 
O.C.D Bihamunuro saa yake ilipiga king'ora huku ikionyesha rangi ya kijani naye Laizer hakuingia ndani gari badala yake akaitazama saa yake huku akiwa kavalia miwani yake aliweza kuona neno lililosomeka kwa kingereza #See_it kwenye kioo cha saa yake alibonyeza kitufe cha kijani kisha saa hiyo ikatuma mawasiliano kwenye miwani naye Laizer aliweza kugundua kitu kisha akamgeukia O.C.D Bihamunuro 

"kuna kinasa sauti kimetegeshwa chini ya uvungu wa gari je ni wewe umekiweka??"

"Hapana Laizer sijui chochote kwa kweli"

Laizer aliinama na kuweza kukitoa kinasa sauti hicho halafu akampatia O.C.D Bihamunuro.....

"daaah nadhani unaona Laizer kwamba kazi hii ni ngumu mno kiasi kwamba nikaomba msaada"

"usijali O.C.D tutawapata tu hawana ujanja wowote"

Yote hayo 
Michael na Steven walikuwa wakiyatazama huku wakikiri kweli wana kazi ngumu ya kufanya na hiyo yote ni kwa sababu Laizer ameweza kugundua hiyana yaoo....
Laizer pamoja na O.C.D Bihamunuro walipanda kwenye gari na safari ya kuelekea kituo cha polisi ikaanza......
Steven na Michael na wao hawakuona kama kuna haja ya kuendelea kukaa katika uwanja ule waliondoka na wao moja kwa moja mpaka nyumbani kwa bosi wao.......
O.C.D Bihamunuro pamoja na Laizer walifika kituoni ambapo baada ya maaskari kuwaona waliwapigia saluti......
Kisha O.C.D Bihamunuro akamuongoza Laizer mpaka ofsini mwake na akaanza kuongea naye kwa kumpa habari mbali mbali

"bwana Laizer lile tukio si la kawaida kabisaa kesho nitakupeleka ukaone jinsi palivyo"

"vipi mlizungushia redcross sehemu ya tukio au mliacha hivyohivyo"

"hiyo haiwezi kusahaulika tulizungushia na tena kuna maasikari wanalinda mchana na usiku"

Walimaliza kuongea kuhusu tukio lile la nyumba kuchomwa moto,......
Ni katika nyumba ya sergent wa kituo cha polisi Igunga......
Sergeant Edwine anaonekana akipiga simu kisha anasubiri ipokelewe

"vipi Edwine mambo yanasemaje huko nini kinaendelea aisee?"

"daaah bwana Jamali we acha tu yaani mtu aliyeletwa yupo makini sana na kazi yake si unamkumbuka 
Laizer Zuber?"

"ndiyo namkumbuka si yule ambaye serikali ilijitoa kumpeleka nchi za nje kusoma?"

"eeeh sasa huyo ndo kaja kufanikisha swala zima la kufanya upelelezi yaani ile kufika amegundua kile kinasa sauti mlichonipatia nikiweke sasa unadhani tutamfanyaje naona kazi yenu itanishinda aisee"

Alisema kwa kirefu Sergeant Edwine kisha akakata simu yake......
Sasa fire linawaka hilo yaani mpaka Sergnt Edwine ameona hiyo kazi ni mbindeee Je Laizer akienda eneo la tukio atagundua nini? basi usikose Muendelezo wa riwaya hii....

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.