Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BLACK AMERICA SEHEMU YA 14

RIWAYA:BLACK AMERICA
        (Mmarekani Mweusi)
MTUNZI:NELSON KIMOY
SIMU:0758638391
SIMU2:0625293917

{{ SEHEMU YA 14 }}
#Endelea_nayo==>Simu ilipokwisha katika 
O.C.D Bihamunuro alibaki na tabasamu mororo usoni mwake.......
Upande wa Rocky na Lissa walitokea kupatana sana kiasi kwamba ni siku nyingi walionana......
Waliendelea na maisha yao katikati ya pori lililopo jirani na pori la Igogo chakula chao kikuu kilikuwa ni wanyama pori waliokuwa wakiwawinda japokuwa Rocky hakuwa mzoefu lakini alijikuta akizoea maisha hayo......
Hatimaye wiiki moja ilipita wiki ambayo O.C.D Bihamunuro alikuwa akiisubiri kwa hamu na hii yote ni kwaajili ya ujio wa rafiki yake wa kitambo sana....
Upande wa Michael na Steven wale vijana ambao waliichoma na moto nyumba ya Rocky walikuwa na kikao na bosi wao mkuu kikao kilichokuwa kikihusu utekelezaji wa mauaji ya Rocky.....
Bwana Jamali alikuwa akilalama sana huku akiwalaumu vijana wake kwa kushindwa kutekeleza mauaji hayo.....
Michael alimtuliza bosi wake huyo kwa maneno huku wakimuahidi kwamba watahakikisha wanamtafuta popote pale....
Wakati wakiendelea kuongea mara ghafla simu ya bosi wao ikaita....
Alipokea na maongezi yakaanza

"haloo Mr Jamali nini unafanya kama vipi rudisha pesa zangu haiwezekani nikupe kazi halafu ushindwe kuifanya na pesa zangu ule tutaonana wabaya"

"Samahani Brown unajua nimewatuma vijana wangu wamechoma nyumba yake moto na wakahakikisha imeteketea lakini nitashangaa kama yupo hai naomba unipe chance ingine mr Brown"

Bwana Jamali akawa amemalizana na Brown kwa kupewa nafasi ingine ya kutekeleza mauaji ya Rocky..........
Helcopter ya jeshi la wananchi Tanzania (J.W.T.Z) inaonekana katika anga la wilaya ya Igunga ikitaraji kutua katika uwanja wa mpira wa miguu...
Maaskari walikuwa sambamba na O.C.D wao kwenda kumpokea mgeni ambaye alikuwa ni wa umuhimu kwao....
Helcopte ilitua huku asikari wakikaa chonjo na bunduki zao kwaajili ya kumlinda mgeni wao huyo kama ungekuwepo katika eneo la tukio ungesema mtu huyo ni Raisi wa nchi........
Baada ya helcopta kutua alitoka Kijana mdogo aliyevalia mavazi nadhifu sana alikuwa kavaa suti ya kijeshi yenye rangi ya kijani pamoja na mabaka mabaka meusi.....
Kisha rubani wa helcopter hiyo alianza kuondoa helcopter huku akipayuka kwa sauti ya juu

"kaziiii njemaaa Laizerrr"

Alipomaliza kusema maneno hayo naye Laizer akapiga saluti kisha akampungia mkono wa kheri Rubani huyo wa ndege......
Wakati yote hayo yakiendelea raia walishangaa ila hawakujua nini kilichokuwa kinaendelea.... 
Steven na Michael hawakuwa mbali katika kushuhudia kila kilichokuwa kinaendelea kwani wameshapata taarifa ya mgeni huyo kuja
ITAENDELEAAA...........  
Mafanis wangu eeeh me naona moto ndo kwanza umeanza hivi hujiulizi kuwa kina Steven wamejuaje huo ujio? Je katika ujio wa Laizer nini kiliendelea basi usikose Muendelezo wa riwaya hii.....

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.