Mahitaji
1.Chenga za mkaa(ule unga unga )
2.udongo wa kichuguu au mwingne wowote
3.Maji
4.chombo cha kuchanganyia
HATUA
1.chukua besen lako weka chenga za mkaa& udongo vichanganye kwa mkon vichanganyikane vzr.
2.Baada ya hapo weka maji kidg kidg kulingana na mchanganyiko wako,mchanganyiko wako usitepete sana uwe wa kawaida
3.Anza kutengeneza maumbo kama ni duara au yai ya size utakayo
4.Anika juani kwa siku 2 au kulingana na ukali wa jua mpaka likauke liwe gum,anika juu ya bati,kwenye karo,jiwe au sehem yoyote ya juu usianike chini.
5.Baada ya hapo tayari kutumia
"Jinsi ya kutumia mkaa uliotengeneza"
1.chukua mkaa uliotengeneza utangulize kwenye jiko lako
2.juu yake weka vimikaa kidg vya kupikia kushikishia mabumba yako yakishika hayo ni kama unapikia jiko la gesi
Hapo utapunguza gharama ya kununua mkaa kwani utatumia mkaa kdg tu wakati wa kuwasha jiko lako yakishika mabumba yako ndo yanaendeleza upishi wako.
Baada ya kujua hilo nimepunguza gharama ya kununua mkaa,kwani mkaa ninaonunua ni kwa ajili ya kuwashia tu si kupikia.