UKI OLEWA NA MWANAUME AMBAE ANAISHI NA WAZAZI WAKE KUNA MAMBO USIFANYE NA KUNA MAMBO FANYA
1)USIPENDE KUJIACHIA UKWENI Kuanzia mavazi mpaka maamuzi ya mambo muulize mumeo hapa huwa mnafanyaje.
2)USIWE MVIVU shirikiana na ndugu wa mume kwenye shida na raha.
3)MUMEO NA MAMA YAKE WANAPO GOMBANA USITIE CHUMVI au kuonyesha una furahi ugomvi wao bali tumia maneno mazuri kwa Mumeo juu ya mama yake.
4)UKIONA KUNA MATATIZO HAKUNA UTULIVU muombe mumeo mpange chumba muhame iwe kwa heri muepuke mizozo.
5)UKWENI NI SEHEMU YA HATARI
wana kuangalia mpaka maongezi yako uwe makini.
6)USINGILIE MAMBO YA NDUGU WA MUMEO kama mambo ya kheri sawa.
7)MUMEO ANAPO KUWA ANA MUONGELEA MAMA YAKE VIBAYA ONYESHA UNA CHUKIZWA huenda wewe ukaleta neema wakaelewana.
8)KUNA WANAWAKE WAMEENDA MBALI ZAIDI ANA MFOKEA MUMEWE MBELE YA MAMA WA MUME WAKE.
9)USIONYESHE UPENDI CHAKULA FULANI AU UKAPIKA CHAKULA TOFAUTI NA KILICHOPIKWA.
10)KUNA WANAWAKE WAMEENDA MBALI ZAIDI wapo ukweeni wana amka saa saba mchana.
💦Ushauri mume jitahidi mkeo asikae pamoja na ndugu zako kwa Muda mrefu💦