Story :CITY LIGHT
BY: mogy shine
Mahali: dar
No.;0659746098
///////////////
EPISOD YA 5 | CITY LIGHT
Mogy alianza kuwaza hivi nimacho yangu au ndio yule msichana ambae nilimwokoa kwenye daraja jana madale baada ya kusobwa na maji ,mogy alitaka kumwita akasita na kuangalia tair ya mkokoteni wake ili kubaini nini chanzo kilichosababisha tair ikabasti .Latifa alimwangalia sana mogy na kujisemea moyoni mwake ,mmmmh najua lote hili huyu kaka anasukuma mkokoteni na amejaza mataka taka kibaya zaidi hayo matakataka yalianza kutoa harufu yote sababu ya kukaa muda mrefu , latifa aliamua aondoke zake ,maana kwa mzee lisu ashafukuzwa ,alianza kuwaza tena ,mmmh yule mama mbona anaroho mbaya na mwanae kwa nini wamenifukuza wakati mimi nimepelekwa na mme wake ,au yule mme wake alitaka nikafanye kazi za ndani kwake ,lakini lile jumba linaonekanika safi ,huyu mzee anaonekanika ana hela ,aaah acha nijiondokee katika hili eneo nisije nikaambiwa mwizi .
Latifa aliondoka lakini baada ya kutembea umbali kidogo aliwaza ataenda wapi na hana mahali pa kwenda ,wakati huo tayari ishafika saa sita mchana alianza kusikia njaa ,huku kwenye sehemu zake za siri alikuwa anasikia maumivu makali ila alikuwa anajikaza anatembea kwa kujikaza yote sababu ya kubakwa na kundi la akina rama
Latifa aliona mti mkubwa wa mwarobaini aliamua akae kwenye kivuli maana jua lilikuwa linawaka sana kuashiria mvua itanyesha muda si mrefu,latifa alijiangalia kifua chake na kuangalia jinsi gauni lake lilivyochanika na kufanya ziwa lake moja la kushoto kutokeza nje ,kile kitendo kilizidi kumfanya latifa akose amani kabisa.
Tukirudi upande wa mogy baada ya mkokoteni wake kuzingua mogy wala hakujali aliusukuma vile vile japo ulikuwa mzito alipambana nao hivyo hivyo ,mogy alikuwa akihema juu kwa juu aliendelea kupambana nao hadi alipofika eneo ambalo walikuwa wakitupa ule uchafu , mogy alianza kuwaza ,daaah haya maisha ya siku hizi sio hata kidogo daah hivi nami nitatoboa kwa kazi zangu za kuunga unga na kuzoa mataka taka majumbani ,mmmmmm si dhani mogy alijiwazia baada ya kumwaga uchafu wake aliwaza apite kwanza kwa mama ntilie akapate chakula halafu ataangalia ustaarabu wa kupeleka mkokoteni wake kwa fundi
Nyumba ya mzee lisu alibaki mke wake pamoja na mwanae mudy ,walikaa sebuleni na kuanza kuteta jambo ,mama alianzisha maada ,"mwanangu unajua baba yako siku hizi anahangaika sana kama unavyoona analeta watu wa ajabu ajabu hapa nyumbani ,baba yako anataka mtu wa kurithi mali zake pia nahisi hataki kukurithisha wewe hizi mali zake sababu wewe si mtoto wake wa kumzaa ,ndio maana siku hizi unaona kabadilika ,ni maneno aliyeongea mama mudy akiwa kakaa na mwanae sebuleni ,"mudy alimwangalia mama yake ,na kusema mama usijali mali zake zote lazima ataandika jina langu na mimi ndiye mrithi wake ,kwanza baba mwenyewe hana mtoto hivyo lazima tu mali zake atanipa mimi ,
Mudy aliongea huku amekalia kwenye sofa akichezea laptop yake ,mama mudy alimwangalia mwanae kisha akamwambia ,mwanangu pia huyu baba yako siku hizi amepata ugonjwa mmoja hivi anasema anamatatizo ya kupoteza kumbu kumbu ,hivyo usijali nitatumia njia flani ili tumdanganye halafu mali zake ziwe mikononi mwetu ,
Basi mama na mwanae walikumbatiana kisha mama alisema anapandisha juu kwenye gorofa ya juu ili akajipumzishe anahisi mwili hauko sawa ,basi aliagana na mwanae kisha akaenda kulala
Kabla hajapanda juu mzee lisu alikuwa tayari karudi alifika cha kwanza aliuliza ",mke wangu yule binti niliyokuja nae yuko wapi?
Mama mudy akiwa anapandisha ngazi kashika glass ya juice alijibu kwa dharau "hii nyumba hatufugi mayatima wala watoto wamitaani nimemtimua kaondoka zake .alijibu vile huku akienda zake juu
Mzee lisu alichoka alivua miwani kisha akakaa kwenye kochi ,huku anamawazo mengi ,alimwangalia mudy ambae yupo bize na laptop akicheza gemu ,kisha akatikisa kichwa ,huyu mwanamke niliyemuoa sio hata kidogo sasa atamfukuzaje binti yule wakati mimi nimemleta? Mzee alijiwazia kisha akavua koti lake na kuingia chumbani kwake kulala na kumwacha mudy akicheza na laptop
Japo lisu alikuwa na jumba la kifahari magari mazuri pia alikuwa kaoa mke ambae alikuwa ki umri ni mdogo tofauti na yeye alikuwa kazeeka sana ,pia huyu mke mama mudy ambae anae sasa alimuoa baada ya mke wake kufariki na ajali ya gari miaka mitano iliyopita ,lakini yule mke aliyefariki hakufanikiwa kupata mtoto hata mmoja ndipo alipomwoa mke wa pili ambae ni mama yake na mudy ,ambae alikuwa na mtoto wake aliyezaa na baba mwingine ,
Kwakuwa mzee lisu alikuwa na uwezo wa kifedha na maisha yake safi hakuona shida kumwambia mke wake wa pili mama mudy baada ya kumuoa ahamie na mtoto wake na atamlea kama mwanae maana alikuwa na hamu ya kupata mtoto lakini hadi uzee ukamfika hakuwa na mtoto ,
Mzee alijilaza kitandani na kuanza kuwaza "huyu mke wangu mbona kabadilika sana siku hizi ,kwanza kanipa chumba changu cha kulala mwenyewe siku hizi silali nae ,yeye analala juu halafu mimi chini kwanini?,pia amekuwa mkali mkali na ananipangia sheria kila siku "mzee aliwaza hadi usingizi ukampitia na kulala zake
Wakati huo mke wake yupo kwenye chumba chake alikuwa anajipodoa safi kapaka make up alivyomaliza alivaa nguo safi kisha aliteremka chini na kumkuta mwanae kakaa kwenye sofa bado anacheza na laptop yake "aliita mudy
"Mudy alivua headphone kisha akaitika naam mama"
Mama kwa sauti ya upole aliuliza vip baba yako kalala ama kaondoka ? "Mudy alivaa headphone zake na kujibu mama baba kalala zake kisha akaendelea kucheza gemu
Mama alitabasamu kisha akaenda kwenye kabati kubwa pale sebuleni alichukua ufunguo wa gari kisha akapindisha mdomo na kusema "we mzee ushazeeka lala tu maana hata siku hizi unikidhi haja zangu ngoja nitoke zangu tutaonana baadae alijiwazia na kutoka aliingia kwenye gari yake alifunguliwa gari na mlinzi kisha akaondoka zake
Tukirudi mtaani ,mogy aliendelea kusukuma mkokoteni wake hadi alipofika kwa mama ntilie mmoja pale masikani kwao anakopaki mkokoteni akiwa ameweka shati lake begani ,aliingia kwenye ule mgahawa kisha akamwita
"Mama azizi " njoo na njaa kinoma nahisi kizungu zungu na njaa ,mogy aliwmita huku akimimina maji kwenye glass ,kwanza mogy alipiga glass tatu za maji ndipo mama azizi akafika "
Mogy alimwangalia mama azizi kisha akamwambia"mazaa leo na buku halafu na njaa kibaya zaidi mkokoteni wangu umezingua umebasti tair moko unahitaji niupeleke kwa fundi "mama azizi niko mbaya naomba wali wa buku jero halafu jero utanidai au ukiona namna gani baadae jion ntapita utanipatia kauchafu ntaenda kutupa mzaa niko doro ujue "mogy aliongea kwa huruma na kufanya mama azizi kumwelewa
"We mogy ushakuwa muongo wewe ole wako usilete hio miatano nimekusikia ,umesahau juzi nilikupa maandazi mawili na chai hela hujaleta hadi leo nakuangalia tu "yalikuwa maneno ya dada mmoja ambae alikuwa akisaidiana kazi na mama azizi aliongea akiwa yuko bize na kusugua safuria ,mogy alitabasamu kisha akajibu we zaituni bana masuala gani tena kuzalilishana hio hela yako ntakuletea bana baadae jioni ntakupa leo leo mogy alijibu wakati huo mamq azizi ashamletea wali wake kajaza na maukoko mengi kisha akapewa na mchuzi wa maharage basi mogy alianza kula taratibu
Mgahawa ule wa mdogo wa mama azizi ulikuwa na wateja wengi waliendelea kumiminika wakiwa wanaenda kula pale yote sababu mama azizi alikuwa mkarimu na mwenye busara
Mara kundi la akina rama nao waliingia pale kwa ajili ya kupata chakula ,rama alipitiliza moja kwa moja hadi mahali aliko zaituni na kumpiga makalio kidogo na mkono kisha akamwita zaiiiii
,
Zai alishituka baada ya kupigwa kwenye makalio yake aliinuka na kusema ,"halafu we rama tabia mbaya kunipiga chura wangu ,"ha ha ha rama alicheka na kusema lakini chura wako yuko vizuri rama aliongea huku akipeleka mkono kwenye maziwa ya zai na kubinya kidogo
"Zai aliruka kidogo na kuongea we rama mi sipendi tabia yako ntakuwagia maji machafu ujue ohoooo zai aliongea huku akiangalia ziwa lake lililobinywa na rama kisha akajisemea ki moyo moyo ,"daaa hizi kazi kwakweli zina changamoto hata kama mteja ni mfalme lakini si kwa kugusa gusa huko aaah "alijiwazia kisha akachuchumaa na kuendelea kuosha vyombo vyake wakati huo akina rama washaingia na kuanza kupata chakula kwa mama azizi
Mara akina hamisi na juma nae walifika kwa ajili ya kupata chakula kwa mama azizi ,mogy alivyo waona akina hamisi kwanza alitabasamu na kusema "oyoo mwamba nawaona ujue nini nilivyowaona nikajua hapa mambo fresh hamisi kabla hujaagiza chakula ndugu yangu mie mkokoteni wangu umezingua nitie hata buku baadae nikitengeneza kwa fundi ntakupa buku lako "hamisi kabla hajamjibu alikaa kwenye kiti kisha akasema "mogy unazingua haya buku ntakupa sasa wakati tunapita mitaa flani tukakutana na dem flani mweupe wa wastani nakuambia mtoto chuchu dodo zaituni haoni ndani ,sema yule manzi alikuwa anatembea peku sijui anaenda wapi ila tulivyomwangalia kama mgeni mgeni
Sema nini sura yake kama ya yule demu ambae jana ulimwokoa kwenye maji kule madale anafanana kichizi hadi nguo ,sema wa leo ananguo zimechanika chanika
Kabla mogy hajajibu alivyoelezewa na rafiki yake hamisi nae alikumbuka binti kama huyo alipishana nae kwa mzee lisu na ndie hata yeye alimfananisha na binti ambae alimwokoa darajani alivyozama na maji
Mogy alimwangalia hamisi na kumuuliza huyo binti umekutana nae wapi na kavaa nguo za aina gani? Hamisi alimwambia mogy tulia kwanza ninawe mikono mbona unaharaka? Si utulie mtu wangu
Hamisi alimaliza kunawa kisha akamjibu mogy "nimekutana jae mitaa ya pale kati kwa yule don tajir tajiri anae itwa lisu,na kavalia gauni moja limechanika kifuani ndio maana nakuambia mtoto jojo ,ha ha ha hamisi alicheka na kumwambia mogy kula we mademu utawaweza?
Mogy alimsikiliza vizuri hamisi na kugundua yule binti hata yeye amemwona lakini mogy akapotezea na kujisemea aah kwanza mtu mwenyewe simjui wala simfahamu inahaja gani kumfuatilia mogy aliendelea kula kama kawaida
Alivyopiga jicho kwa zai alimwona zaituni akisugua safuria na kufanya maziwa yake kunesa nesa ,ndipo mogy alimtizama vizuri na kujisemea ndio maana wanaume wengi wanapenda kuja kula kwa mama azizi kumbe kula mtu anamtamani zaituni daaah
"Ila mama azizi mungu anakuona unatafuta wasichana wazuri ili auze daa
Mogy aliendelea kula ,lakini katika huo mgahawa ambao walikuwepo akina mogy, hamisi,juma ,pia kuna kundi la akina rama ambao ndio walimfanyia kitendo cha kinyamba bibie latifa kwa kum baka tena wanaume wanne ,na walimsikiliza vizuri hamisi akiwa anamwelezea mogy kuwa amekutana na dem mkali
rama aliwaambia vijana wake ama kundi lake oi vany,na chidi hivi hawa kachaliii wanamzungumzia dem gani hebu twendeni maeno ya huyo don lisu ili tukamcheki yawezekana ndio yule ambae tulmfanya kitu mbaya usiku ,inaonekanika yule dem hana mahali pa kwenda
Kundi la akina rama waliacha kula na kulipa pesa kisha safari zikaanza kuelekea kwa maeneo ya don lisu ili kumcheki yule bint anae zungumziwa ni yeye ama sio yeye
Wakati huo zaituni alivyomaliza kuosha vyombo alienda moja kwa moja kukaa karibu na mogy na kumwangalia jinsi anavyokula ,zai alichombeza neno kwa mogy "ujue mogy nimekumiss halafu unasiku mbili hujaja kula hapa kwenye mgahawa wetu , zai aliongea huku akipeleka mkono kwa bega la mogy ,
Pale pale mogy aligeuza macho na kumtizama zaituni usoni mogy akajikuta mawazo yana hama kabisa "lipsi za zaituni zilikuwa nyembamba macho yakulegeza kila kiungo mogy alivyotizama kifua cha zai kilichosimama ndani ya dela jepesi
Mara mogy kuangaza macho nje ya ule mgahawa aliweza kumwona latifa akiwa anakatiza bara bara akiwa peku peku na lile lile gauni lake alivyotizama vizuri alisikia kijana mmoja akiita" rama njoo huku yule dem nimemwona yule pale anakatiza barabara
MWENDELEZO
------------
EPISOD YA 6 | CITY LIGHT
Tulipo ishia jana baada ya mogy kumwangalia sana zaituni wakiwa wamekalia bechi moja pale kwenye ule mgahawa , Mara mogy kuangaza macho nje ya ule mgahawa aliweza kumwona latifa akiwa anakatiza bara bara akiwa peku peku na lile lile gauni lake alivyotizama vizuri alisikia kijana mmoja akiita" rama njoo huku yule dem nimemwona yule pale anakatiza barabara .
Mogy alisimama na kutaka kwenda kujua akina nani hao wanamfuatilia huyu binti na kwanini wanamfuatilia pia mogy alipenda kwenda kuhakikisha kweli ndio yeye ,ama yuko tofauti na binti aliyemuokoa kwenye daraja.
Wakati huo mogy alishamaliza kula ,na kuwaacha akina hamisi na juma wakiendelea kupata chakula kwa mama aziza,mogy aliinuka na kumwambia zai"zai bana tusifanyiane hivyo bana hela yako ntakuletea pia nishamweleza bimkubwa kuwa saiv siko vizuri ,kwahio nikipiga piga kazi ntakuletea hio pesa yake ,
Mogy aliinuka na kuushika mkokoteni wake ,kisha akaangalia mahali alikokatiza latifa ,mogy aliwaza aende akamwone kisha mawazo mengine yalimjia akilini mwake na kucheka kidogo "hivi mimi nina hakili kweli mbona nataka kufuatilia mtu ambae hata hatujuani ,aaah ngoja nizunguke mitaani nitafute kazi zangu za kuzoa mauchafu majumbani nipate pesa maana nadaiwa kila mahali ,mogy alijiwazia na kuanza kusukuma mkokoteni wake na kuelekea kwa fundi kwa ajili ya kuutengeneza
Wakati huo kundi la akina rama walivuka bara bara upesi nia yao kumkamata latifa ili wamfanyie kitendo kibaya kwa mara nyingine ili kama ametoa taarifa polisi ili asiweze kuwataja
"Oya beni na chidi fanyeni chapu yule dem yule pale anakata kona hivyo tukamvizia pale kwa muha anakouza mkaa najua atapita maeneo hayo tuweze kumdaka ni maneno aliyoongea rama akiwaambia wenzake " walipita shoti kati na kwenda kutokea maeneo ya kwa muha na kumsubiri latifa wakiamini atapita maeneo yale ili waeze kumkamata
Wakati huku latifa aliendelea kutembea pasina kuhisi kama kuna watu wanamtafuta tena wenye nia mbaya ,alikuwa akitembea taratibu tena akiwa peku ,mikono yake alishikilia gauni lake ili kuzuia maziwa yake yasitokeze kwa nje,latifa alizidi kutembea na kujiona hana furaha na kuzidi kulichukia sana jiji la dar ,
Farida aligeuza macho upande wa pili mwa ile bara bara aliweza kuona fremu kubwa na kuana baba mmoja kakaa akiwa anashona na cherehani nguo za wateja wake ,fundi alikuwa kawasha tv yake pale akiendelea kupata burudani za vipindi mbali mbali huku akiendelea kushona taratibu
Latifa aliwaza japo hana pesa kwa kuwa yule ni mwanaume akamwomne amushonee gauni lake ili aweze kutembea kwa uhuru ,latifa akiwa na uoga kutokana na ugeni wa yale mazingira alifika kwa yule fundi alimsalimia na fundi nae aliitikia kisha akaendelea na kazi yake ya kushona wakati huo latifa kasimama mlangoni na kushidwa jinsi ya kuomba ashonewe
"We dada karibu mbona unashangaa? Ingia ndani nikuhudumie ni maneno aliyoongea fundi akiwa anamwambia latifa,wakati huo latita akiogopa ataanzaje
,fundi alimtupia jicho latifa maeneo ya kifuani na kushangaa kumwona latifa kaweka mikono kifuani alivyomwangalia miguuni aliona latifa akiwa peku peku ,fundi taratibu aliendelea kumchunguza alivyoangalia gauni alilovaa latita lilikuwa limechafuka ,fundi aliguna na kujisemea moyoni yaani dar kwa omba omba hawajambo yaani binti mrembo hivi atakuwa omba omba ,na mimi simpi pesa labda anipe pale kati patam
Latifa alijikakamua na kuita kwa unyonge "fundi samahani kwa kukusumbua sina hela na gauni langu limechanika kifuani naomba unishonee " latifa aliongea huku macho yake kaangalia chini ,fundi kabla hajajibu chochote alimwambia
Halafu we binti unazingua ,haya vua hilo gauni nikushoneee shika hii kanga jifunike ,halafu uvue hilo gauni nikushonee ,latifa alipokea ile kanga kisha alielekezwa chumba cha kujaribishia nguo kisha aliivua ile gauni na kujifunga kanga moja kibaya zaidi kanga aliyopewa na fundi ilikuwa ni fupi hivyo akijifunga juu ya kifua chake itaishia kati kati ya mapaja yake hivyo hataweza kutoka nje sehemu mahali watu wanapita .
Pia kutokana na mazingira aliyolelewa latifa hakuzoea kuvaa nguo fupi ama nguo za kileo ,yeye hupenda kuvaa nguo za kujisitiri ,
Latifa alisimama mlangoni na kumwita fundi kisha alimrushia ile gauni yake ili aweze kuishona ,wakati huo fundi alikuwa akishona huku akitabasamu ,"yaani huyu mtoto wa kike simwachi anachuchu konzi kama kawaida yangu lazima anilipe tu ,sitaki kuelewa ni masikini ama omba omba ila mi najua anakitu cha kunilipa sina muda wa kuchezea hapa na nguo nyingi za wateja nimeacha kwa ajili ya gauni yake
Fundi aliendelea kuishona gauni ya latifa taratibu ,wakati huo upande wa pili kundi la akina rama walikaa wakimsubiri kama wataona latifa anakatiza maeneo yale lakini hawakumwona ,ikabida rama atoe wazo "oya chidi huyu dem atakuwa kaenda sehemu nyingine kama vipi tuachane nae kwanza inaonekana ni chizi sijui kichaa yule hebu tuachane nae tukawinde pale masikani huenda tutapata hata washamba watatu tupige roba tukikaba wapuuzi watatu najua hatuwezi kosa simu tatu na pesa hivyo maisha yetu yatakuwa poa
Rama aliongea huku akipikicha rasta zake alikubaliana na wenzake kisha wakarudi mtaani kwa ajili ya kuvizia watu ili wawakabe wapate pesa
Wakati huo mogy nae alienda kwa fundi kwa ajili ya kutengeneza mkokoteni wake alifanikiwa kutengenezea kisha alianza kupita mitaani kwa ajili ya kutafuta watu wenye uhitaji wa kuwatolea mataka taka majumbani na kwenda kutupa ili apate pesa
Wakati huku kwa latifa ,fundi alimaliza kushona gauni la latifa na kumwambia we binti gauni lako tayari nimemaliza njoo lichukue uvae ,latifa kabla hajatoka kwenda kulichukua akiwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo ,aliwaza nitatoka vipi na hii kanga fupi hivi jamani mapaja yako wazi nami sijazoea ,latifa alimwambia fundi "naogopa kutoka huko hii kanga fupi inanionesha nusu uchi" yale maneno ambayo alimwambia fundi ,pale pale fundi aligundua kuwa huyu binti ni kuku wa kienyeji ,(yaani bado mshamba hajazoea kuvaa kimjini mjini),fundi alijilamba midomo yake na kumwambia we toka uje uchukue gau lako inamana nimekushonea bure na bado unataka nikuletee huko huna adabu we binti.
Yale maneno kweli latifa aliyasikia na kufanya ajione uoga wake unaweza ukamsababisha fundi akakasirika ,alichokifanya ni kujikaza na kuondoa aibu ,alijisemea moyoni "naenda hivi hivi kuchukua gauni langu,
Ki ukweli fundi alikuwa bado kijana kabisa hata ukiambia hajaoa ni sawa maana umri wake ulikuwa bado unaruhusu ,
Wakati latifa anapiga hatua kutoka kwenye kile chumba cha kubadilisha nguo alishangaa kukanyaga kitu chini "latifa aliguna mmmm jamani nimekanyaga nini hicho?
Latifa ilibidi atoe mguu na kutizama chini alikanyaga nini ,latifa alishangaa na kubaki mdomo wazi baada ya kuona kikaratasi kidogo kime andikwa dume kondomu ,lahaulaah latifa aligeuza macho upande wa pili kwenye kile chumba alishangaa kuona maganda mengi ya kondomu yamezagaa kwenye kile chumba ,kibaya zaidi zote zilikuwa zimetumika
Latifa alihesabu haraka haraka zilikuwa zinafika nane ,latifa aliguna na kujisemea nani ametumia kondomu zote hizi kama si huyu fundi "uwi mungu wangu nisaidie nitoke salama kwenye kwa huyu fundi ,wakati latifa amapata mshangao baada ya kuona makaratasi ya kondomu zilizotumika alishangaa anaitwa na fundi
"We binti ntaichana hii gauni yako ohooo sinaga muda wa kubembeleza mimi njoo chukua gauni lako mie niendelee na kazi yangu ",ki ukweli fundi aliongea kwa ukali na kumfanya latifa kutoka nje ya kile chumba akiwa na kanga fupi , na kukutana na macho ya fundi yakiwa yamemkodolea ,latifa aliona aibu na kuinamisha macho yake chini
Kisha fundi alimpa lile gauni lake na kumuuliza "we binti unamataatizo ee asa ulikuwa unaogopa nini mbona umejifunga vizuri tu . Latifa alipokea gauni lake na kulikagua mahali alikoshona fundi kisha alimshukuru "fundi asante sana mungu akubariki "
Kisha latifa aligeuka na kurudi kwenye kile chumba cha kubadilishia nguo ,wakati anatembea fundi alimtizama nyuma jinsi latifa anavyotembea huku sehemu za nyuma zikirindima ama kutikisika taratibu ndani ya kanga ,fundi alitabasamu na kusema "huyu mtoto balaa nahisi kama ndani hajavaa kitu chochote ki ukweli si muachi kama kawaida yangu ,
Wakati huo latifa aliingia kwenye chumba cha kubadilisha nguo ,huku fundi aliinuka na kurudishia mlango kwenye ofisi yake ili kama mteja akija ajue fundi hayupo
Fundi hakupenda kuchelewesha muda wake alifunga mlango upesi kisha akaanza kupiga hatua kuelekea kiliko chumba cha kubadilisha nguo,wakati huo latifa alishituka baada ya kuona giza limetanda kwenye kile chumba baada ya fundi kufunga mlango ,wakati huo alikuwa tayari ashavua kanga na kuitupa pembeni na kubaki na nguo ya ndani kwakuwa alikuwa kwenye chumba cha kubadilisha hakuwa na shaka sana alitoa kanga yake upesi
Mara anasikia hatua za miguu za mtu akitembea kuelekea mahali aliko yeye wakati huo latifa alikuwa ameinama chini ,aligeuka na kuhamaki nani anaingia kwenye hicho chumba angali yeye yupo uchi
Ndipo alishangaa kumwona fundi akiwa anazidi kusogea mahali aliko mkononi kashika pakiti moja ya kondomu ,
Fundi aliongea kwa sauti ya upole "we binti usipige kelele tafadhali wakati huo latifa amejifunika kifua chake na gauni lake alikuwa bado hajalivaaa ,fundi tayari ashafika na kumsogelea latifa alimgusa bega na kumwambia "sikia we binti kazi ya kushona ni ngumu hivyo sishonagi buree mimi nitaka tumalizane tulipane hapa hapa .........
Je nini kitaendelea?
