Notification texts go here Contact Us Buy Now!

CITY LIGHT SEHEMU YA 02

Tulipoishia jaana baada ya kundi la wamama kuamua kuungana kwa pamoja ili waweze kuvuka yale maji ili kuunda nguvu wasiweze kusobwa na maji ,ila kutokana na wingi wa maji na jinsi mvua ilivyonyesha kubwa ,pia kutetemeka kwao kuliwafanya wasobwe na maji
Story :CITY LIGHT
BY: mogy shine
Mahali: dar
No.;0659746098
///////////////

CITY LIGHT SEHEMU YA 02

EPISOD YA 2 | CITY LIGHT


Mzee lisu alipiga kelele na kusema bahashaaaa ,wakati huo mogy ashajirusha kwenye maji na kwenda kuwaokoa wale wanawake ,huku juma na hamis nao wanaenda kuwasaidia kuwatoa kwenye maji maana walianza kusobwa
Kibaya zaidi latifa aliangukia pa baya sehemu kwenye shimo la daraja ,....

SONGA NAYO .......
Walianza kukokotwa huku wakijaribu kuomba msaada ,maji yalikuwa na kasi mno ,juma aliwahi nae na kuwashika wamama watatu kisha aliwainua huku hamisi nae kawashika wengine watatu waliwainua na kuanza kutoka kwenye maji. wakati wanawake wawili washakokotwa na maji na kuingia kwenye kina kirefu cha mto ,kutokana na kasi ya maji kuwa kubwa hata mogy alishidwa kuogelea nae alijikuta anasobwa na maji wakati huo kulikuwa na mti mmoja umening'inia kwenye mto ,mogy alizamishwa ndani alivyoibuka alidaka tawi la mti kisha akapangusa maji usoni mara bahasha ya mzee lissu ,ikaenda mahali aliko mogy ,pale pale mogy alivuta kumbu kumbu kabla maji hayajawasomba wale wanawake aliona binti mmoja alikuwa kashika ile bahasha ambae ni latifa
Mogy aliichukua ile bahasha wakati huo mzee lisu anahaha mara anataka kuvua koti la suti ki ukweli alionesha kuchanganyikiwa ,yawezekana ile bahasha ilikuwa na umuhimu mkubwa mno.

Mogy aliweza kuwaona wanawake wawili wakiwa wanasobwa na maji alisimama vizuri na kuwashika mikono kisha akawatoa nje
Alivyowafikisha nje ,mogy aliangalia tena kwenye maji ,mogy alijikuta akitaja "MUNGU WANGU ANAKUFA HUYU MDADA "!!

Mogy alizama tena kwenye maji kiukweli alishangaa kuona miguu juu ya bibie latifa huku kichwa kimeingia kwenye tundu la daraja ,latifa kutokana na njaa aliyokuwa nayo hakuweza kujiokoa alianza kunywa maji taratibu hadi akawa kinywaa
Mogy alimtoa nje ,kila mtu akiwa na hofu huenda latifa ashapoteza maisha.

Mwili wa latifa ulikuwa tayari umelegea kabisa walimtoa nje na kumlaza chini ,wakati huo mogy akiwa anahofu mzee lisu alisogea hadi kwa mogy alimwona akiweka ile bahasha chini ,mzee lisu aliinama na kuchukua ile bahasha kisha akatoa nailoni upesi ili kubaini kama haijaloa ,ukweli alikuta makaratasi ya ndani yako safu ,mzee lisu alitabasamu na kuweka miwani yake vyema kwenye mboni zake ,kisha akaelekea kwenye gari

Jamani mdada wawatu mbona mzuri kafa au inakuwaje hapa ?" Ni maswali ambayo walikuwa wanauliza watu pale darajani huku wale wanawake wengine ambao walikuwa wamesobwa na maji wapo walikuwa wanakamua nguo zao
Wengine wanalia simu zao zimedumbukia kwenye maji na mikoba yao imelowa .wengine wanalaumu mekapu zao zimeharihika usoni basi ni vichekesho vilizidi kutokea huku masikitiko yametawala.

Mogy alimtizama latifa ambayo tayari kalazwa chini ,watu walisema jamani tayari ameshafariki mpelekeni hospitali ,kuna mama mmoja alivua kitenge chake na kumfunika latifa na kusema pumzika vyema kisha alimfunika vizuri ,akina hamisi na juma walianza kumlaumu mogy ,
" we mogy unazingua umeshidwa kumwokoa mdada wawatu ona kapoteza maisha ,sasa inabidi ukaitafute familia yake uwape taarifa ,ni maneno ya juma aliongea huku akivua shati lake na kubaki na bukta .

Wakati huo mzee lisu ambae ndio chanzo cha latifa kuzama kwenye maji wala hakukumbuka tena aliwasha gari yake na kugeuza kisha safari ya kuelekea kwake ikaanza ,wakati darajani anamwacha latifa ambae kasababisha hadi kasobwa na maji hakukumbuka tena

Hamisi alisema oya " huyu binti hajafa ngoja nimpulize mdomoni ataamuka tu ,hamisi alifanya vile ,kiukweli latifa alikuwa bado mzima ila alizidiwa na maji na baada ya kuingiza kichwa kwenye shimo la daraja alikosa pumzi na kunywa maji mengi ,walimpuliza mdomoni na kumkandamiza tumboni ,

Siku zote mungu huwa ni mkubwa latifa alianza kutapika yale maji aliyokunywa taratibu huku akifumbua macho ,baadhi ya akina mama walianza kulia na kujuwa mwenzao amefariki ,ila alivyoanza kutapika yale maji walinyamaza na kuangalia kwa umakini

Mzee lisu hakufika umbali mrefu alikumbua ,alimwona kijana anamtoa binti kwenye maji akiwa kalegea ,mzee lisu alijikuta akikanyaga breki za gari yake na kusema ,"masikini hii bahasha imesababisha yule msichana amekufa ,"haa ,ngoja nikamchukuwe nimuwahishe hospitali ,mzee lisu aligeuza gari upesi na kurudi hadi darajani alifika pale na kuomba yule binti apakiwe kwenye gari aweze kumuwahisha hospigali ,
Mzee lisu alimwangalia mogy na kumuuliza wewe kijana nilikuona unamwokoa huyu binti ,je unamfahamu ama unafahamu familia yake iliko?

Mogy alitikisa kichwa kuashiria hamjui wala haijui familia yake ,ki ukweli latifa alikuwa hajitambui hata kidogo na alibaki na gauni lake tu ,ndala zake tayari zishasobwa na maji ,
Mzee lisu alimpakia na kuwaambia akina mogy na wenzake anampeleka hospitali ,

Ki ukweli mzee alikuwa na busara alimpeleka hospitali na latifa alipokelewa upesi ,maeneo ya mbezi beach moja ya hospitali iitwae massana , wakati huo mzee lisu alibaki mapokezi na kumsubiri yule binti atibiwe maana hajui hata anaitwa nani wala familia yake ,lisu aliamua kumpatia matibabu kwakuwa alijua yeye ni chanzo hadi latifa kukubwa na hayo maafa ,wakati latifa anaendelea kutibiwa ,akina juma,hamisi na mogy waliendelea na kazi yao ya kuwavusha watu huku wakiendelea kupata pesa,

Hadi inafika mida ya saa nne asubuhi ndipo mvua ziliisha na maji kuanza kupungua barabarani na kwenye mito ,watu walianza na pilika pilika zao za kila siku ,
Wakati huo ,latifa alikuwa ashapona ila alikuwa akitetemeka sana kwa baridi ,mzee lisu alifanikiwa kulipa pesa ,kisha latifa akaruhusiwa ,mzee lisu alikosa mahali kwa kumpeleka latifa kwasababu walikuwa hawafahamiani ilimubidi amuulize jina lake na wapi anaishi

Wakiwa ndani ya gari lisu aliuliza "binti unaitwa nani na unaishi wapi?lisu aliuliza huku kashikilia usukani wa gari ,latifa alimwangalia lisu kwa uoga kisha akaanza kuongea huku anang'ata ng'ata meno yote sababu ya baridi na nguo zeke zilikuwa zimeloa "
"Mimi naitwa latifa naishi ... latifa hakumalizia aliishia kusema naishi naishii,mzee lisu alimwangalia na kumuuliza latifa unaishi wapi nikupeleke nyumbani kwenu maana nachelewa kwenye kikao ofisini ,
Latifa alifikiria kwenye kichwa chake atamwambia nini lisu yeye hana mahala pa kulala wala kuishi anasiku tatu toka atoroke mahali alipokuwa anafanya kazi za ndani ,na mahali alipokuwa akifanya kazi za ndani alitoroka baada ya kuzidi kuteswa na kufanyishwa kazi kama punda ,huku matusi na kupigwa kila siku ,kili mfanya atoroke sasa hana rafiki wala hafahamiani na mtu yeyote kwenye jiji la dar na hajui hapo waliko ni sehemu gani

Latifa alisema mimi naishi mbali sana baba ,hivyo naomba unishushe mimi nitaenda mwenyewe ,latifa aliongea na kuangalia kwenye dashi bodi kwa juu aliweza kuona ile bahasha ambayo alipewa ampelekee lisu ambaye ndio yuko nae ,

Latifa aliuliza ,"hii bahasha nilipewa na baba mmoja aliniambia nikuletee na tulivyosobwa na maji sikujua niliitupa wapi ,lisu alimwangalia latifa na kubaini latifa hana sehemu ya kuishi inayojulikana aliingiza mkono mfukoni alitoa elfu 30 alimpa latifa na kumwambia
Binti latifa ,mimi naitwa mzee lisu ,samahani kwa kukuponza kusobwa na maji ,shika hii pesa ,ukanunue nguo ubadilishe maana hizo zimeloa ,ununu na viatu maana viatu vyako vilisobwa na maji ,pia hela ikibaki utachukua usafiri na kurudi kwenu ,hivyo kwakuwa umesema nikushushe hapa utaweza kwenda nyumbani mwenyewe ,mimi sina kipingamizi kila lakheri latifa ,

Mzee lisu aliongea na kumkabidhi latifa pesa ,latifa kwakuwa nae alikuwa na njaa pia hana mahala pa kuishi aliipokea ile pesa na kuamini itamsaidia ,alifungua mlango wa gari kisha akashuka na kuondoka ,wakati huo wapo maeneo ya goigi ,mzee lisu aliondoka zake na kumwacha latifa ,

Latifa aliziangalia zile pesa na kujisemea moyoni "mungu amubariki huyu baba kaniokoa hii pesa inabidi ninunue ndala za elfu mbili pesa itakayo baki kesho niende ubungo ,niweze kupanda magari ya mikoani nirudi kwetu singida ,

Latifa aliondoka maeneo yale na kuanza kutembea maeneo ya kando kando ya barabara ,kuu (bagamoyo rodi , ) na alitembea akiwa anaelekea lugalo ama mwenge (kichwani latiifa alizidi kuwaza atakula nini ,na atafanyeje ili asiichezee pesa yake kesho arudi kwao singida ,pia aliendelea kuwaza ,sina mama baba sijui aliko nikienda singida nitaenda kukaa wapi? Wazo lingine lilimjia bora kuteseka kijijini kuliko hapa mjini ,nikifika singida nitaenda hata kwa mjomba nitaishi ivyo hivyo

Alitembea umbali mrefu na alikuwa akisoma magari yameandikwa ,simu 2000 na watu wakisema mawasiliano ubungo ,alijuwa fika kuwa yale magari yanaenda ubungo ,kutokana na ugeni aliokuwa nae ,toka afike dar hakuwahi kutoka wala kwenda sehemu yeyote zaidi ya kufungiwa ndani ya geti na kufanya kazi za ndani kama mfugwa

Latifa alizidi kutembea huku akifurahia jiji la dar lilivyozuri,licha yq kupewa pesa na mzee lisu hakutaka kabisa kuitumia aliamua aifanye nauli aweze kurudi kijijini ,aliziweka zile pesa ndani ya brazia akabana vizuri aliendelea kutembea hadi nguo zake zilikauka .
Hatimae alifika maeneo ya mwenge kwenye mataa alishidwa kuelewa ni barabara ipi ndio inaelekea ubungo ,kutokana na wingi wa magari maeneo ya mwenge pia kilichomchanganya ni njia panda ya pale mwenge barabara zilipishana hivyo hakuelewa
Latifa aliwaza sasa hapa ubungo ndio wapi wakati huo ishatimia saa tisa jioni alihisi tumbo linawaka moto na njaa ,
Latifa kichwani mwake alikwa anamawazo mengi alikumbuka wosia ambae alikuwa akipewa na marafiki zake ambao walishawahikufika dar ,walikuwa wakimsimulia yaani ukipotea dar ,imekula kwako utakapo muuliza mtu akuelekeze ,anaweza kukuelekeza sehemu mbaya unaweza kuibiwa pesa ,au kubakwa ama kufanyiwa kitu chochote ,yaani ukipotea maeneo ya dar na hujui mahali unaelekea

Usije ukamwomba mtu yeyote barabarani akuelekeze utapotezwa yaani dar wamejaa matapeli wa kila aina iwe mwanamke mwanaume au hata mtoto ,endapo utapotea nenda kwenye duka ,au kwa muuza maji barabarani ,au mama ntilie hao ukiwaomba wakuelekeze wataweza kukuelekeza vizuri ,kibaya zaidi hawawezi kukuelekeza bila kununua kitu ,
Hivyo lazima utajifanya unanunua maji ,au soda au hata vocha ,hapo ukimuuliza atakuelekeza vizuri ,lakini dar ukiuliza hivi hivi hamna atakae kuelekeza hata siku moja

"hayo ni maneno ambayo anayakumbuka marafiki zake walivyokuwa singida walishawahi kumwambia hivyo ,basi latifa aliangalia kulia na kushoto ,aliweza kuona mama mmoja pale barabarani akiuza maji akiwa kasemama kando kando ya bara bara
,latifa alisogea hadi kwa huyo mama alimwamkia "shikamoo mama naomba juic na biskuti " latifa aliongea huku akiingiza mkono kwenye brazia na kutoa noti ya elfu moja ,wakati huo ,mama alishaitikia salamu na akatoa juic ya embe na biskuti
Latifa wakati anatoa zile pesa ,kuna mkaka alikuwa kasimama pembeni kavaa kitanashati anaonekana msafi shati jeupe na tai chini kavalia kiatu cheusi
Ukimwangalia ukiambiwa anafanya kazi benk kiukweli huwezi ukabisha ,yule mkaka aliweza kumwona latifa akirudisha pesa zingine kwenye brazia ,alimwangalia upesi latifa aligundua huyu binti mshamba wa jiji ,yule kijana alitoa simu hake na kuanza kubonyeza bonyeza

Latifa baada ya kupokea juic na biskuti alilipa hela kisha akamwambia " mama samahani mimi ni mgeni naomba unielekeze mahali iliko stendi ya ubungo ," wakati latifa anamwambia yule mama muuza maji na juic ,yule mkaka mtanashati alisikia na akawaza kwa haraka ,yes nimemkamata mshamba ngoja nitege dili
Mama muuza maji alimwangalia binti kisha akamwambia ubungo unakatisha na hii bara bara inayoelekea kusini utaenda moja kwa moja hadi ubungo utaona sehemu kuna mataa basi hapo utaweza ulizia mtu yeyote atakupeleka hadi getini
Mama alimaliza kumwelezea latifa na akaendelea kupanga maji yake vizuri kwenye meza ya kuuzia

Latifa alisema asante kabla hajaondoka yule kijana mtanashati aliweka simu sikioni na kujifanya anaongea
Alianza kuongea taratibu akiwa anajiamini
"Halo mdogo wangu tayari ushafika ubungooo ,oooh pole na safari mdogo wangu nakuja sasa hivi ubungo kukuchukua nakuja nakuja
"
Ni maneno aliyoongea yule kijana mtanashati huku akimwita dereva wa piki piki ili aweze kuwaishwa ubungo ili akampokee mdogo wake jinsi alivyosema
Latifa nae alimsikia yule mkaka akiongea kuhusu kwenda ubungo ,na yeye latifa anataka kwenda ubungo akaona huyu mkaka mtanashati wanaweza kwenda nae ili iwe rahisi asipate kusumbuka kuuliza uliza
Yule kijana mtanashati alipanda kwenye piki piki kisha akamnong'oneza dereva ,oya mwanangu na buku unamwona yule dada pale nampeleka mahali hivyo hatutaenda ubungo naenda sinza mabatini "dereva wa boda boda alimwambia sawa hamana neno

Yule mtanashati alisogea hadi aliko simama latifa "kwa kujiamini alimwambia wewe dada si unaenda ubungo? Twende nikupeleke hata mimi naenda huko kumchukua mdogo wangu kafika sasa hivi katoka dodoma "
Latifa kusikia maneno ya yule kijana hakuwa na kipingamizi kwakuwa alimsikia anaongea na simu kuwa anaenda ubungo
"Latifa alisema asante mungu nimepata msaada napelekwa ubungo ,latifa akajikuta anapanda ile piki piki alopamda kijana mtana shati

Yule kijana alijisemea moyoni "we dada kumbe boya wakuja ee sasa utaisoma namba ..piki piki ikawashwa na safari ikaanza


Je nini kitaendelea?

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.