Notification texts go here Contact Us Buy Now!

CITY LIGHT SEHEMU YA 01

CITY LIGHT: Ni kwa uwezo wa mwenyezimungu pakiwa pamepambazuka kabisa alfajiri huku manyunyu madogo madogo ya mvua yakiendelea kumiminika taratibu ,katika jiji la dar es salaam.ilikuwa siku ambayo kila mtu hakutamani kuamka kabisa kitandani yote sababu ya kaubaridi kalichoambatana na mvua ndogo iliyokuwa ikinyesha , manyuny yalibakia baada ya mvua kubwa kunyesha usiku kucha ,katika jiji letu la dar ,kutokana na miundombinu kujegwa pasina kufuatisha mikondo ya maji ,basi jiji zima lilitapakaa maji ,
Story : CITY LIGHT
BY : Mogy shine
Mahali ; dar
No. 0659746098
//////////////
CITY LIGHT SEHEMU YA 01

Episod ya 1 | CITY LIGHT

-----------------------------------------
Ni kwa uwezo wa mwenyezimungu pakiwa pamepambazuka kabisa alfajiri huku manyunyu madogo madogo ya mvua yakiendelea kumiminika taratibu ,katika jiji la dar es salaam.ilikuwa siku ambayo kila mtu hakutamani kuamka kabisa kitandani yote sababu ya kaubaridi kalichoambatana na mvua ndogo iliyokuwa ikinyesha , manyuny yalibakia baada ya mvua kubwa kunyesha usiku kucha ,katika jiji letu la dar ,kutokana na miundombinu kujegwa pasina kufuatisha mikondo ya maji ,basi jiji zima lilitapakaa maji ,

Maji yaliyojaa majumbani hasa kwa wale waishio mabondeni ,kuna wapo ambao hawakufanikiwa kulala kwa raha yote sababu ya maji kuingia ndani ya nyumba na kuloanisha baadhi ya vyombo magodoro ,makochi na vinginevyo vingi .
Hamna hata mtu yeyote aliyefurahia kabisa kunyesha kwa mvua ile ,kila mtu alitamani ikatike ili waendelee na shughuli za uwajibikaji makazini wapate kusaka pesa .

Wenye uwezo afadhali waliwabeba watoto wao kwenye magari na kuwapeleka shuleni yote sababu ya kujaa kwa maji mengi sana bara barani ,foleni kubwa ya magari nayo iliendelea kusogea taratibu na kufanya siku hiyo kila mwenye gari kuchukia sana ile siku pasina kukumbuka kuwa mvua hailetwi na mwanadamu bali kwa uwezo wake mungu.

Iliendelea kunyesha huku vyombo vYa habari vikiendelea kutoa taarifa kwa wahanga wa mafuriko walio kubwa na adhaa hio hasa wale wamabondeni ,serikali iliwaomba watu wahame mabondeni lasivyo watapoteza maisha kutokana na kukadiriwa na wanasayansi kunyesha mvua kubwa mno kwa kipindi cha wiki moja ,hasa waishio nyanda za pwani ,na nyanda za juu ,zaTanzania.

Maeneo ya madale ,kulikuwa na sehemu zenye mabonde makubwa yalisababisha maji kujaa na kusababisha watu kushidwa kuvuka hasa watembea kwa miguu na wa piki piki hata wale watembeao na magari walishidwa kuvuka kabisa
Kulikuwa na kijimto ambacho kilikuwa kimetengenezewa daraja dogo la aina yake ,ila kutokana na ukubwa wa ile mvua maji yalifurika na kufanya watu waogope kabisa kuvuka .kuna gari zuri la kisasa na ndio magari pekee yanayotembelewa na matajiri na yenye uwezo wakutembea katika matope hata maji ,kwani magari yao yametengenezwa kwa utalamu wa hali ya juu ,

Ilikuwa range rover ilipaki maeno yale ya darajani ambako watu walishidwa kuvuka kutokana na maji kufurika .yaonesha yule mtu ama mmiliki wa ile gari alitaka kuvuka lile daraja aweze kwenda kwenye shughuli zake ,ila hali aliyoikuta pale alibidi apaki gari pembeni na kusubiri maji yapungue aweze kupita ,

Hakika siku hio wanaume walipata pesa kwa ajili ya kuwavusha watu kutoka upande mmoja hadi kwenda upande mwingine ,,
Sauti ya vijana watatu waliongea huku wakipangusa maji kwenye nyuso zao yote sababu kuloanishwa na mvua ndogo ama manyunyu ambayo yaliendelea kunyesha taratibu

"Nyie wamama na wadada leteni buku moja moja kila mmoja tunawavusha kwenye haya maji muweze kuwahi makazini ,"ni maneno ya wale vijana waliojifanya ni wazoefu wa kuvuka maji walianza kuwavusha watu taratibu huku wakipokea pesa tu ,

Vijana hao waliomba walau mungu aendelee kushuusha neema ya mvua ili waeze kujipatia pesa ,kuna wamama waliomba wavushe bure ,ila wale vijana waligoma kabisa kata kata kumvusha mtu bila malipo.wao waliweka sheria pesa mkononi unavushwa kwenye maji.

Oya we mogy acha uduanzi tatizo lako unajifanyaga msamaria mwema sasa leo tuna sema hamna kumvusha mtu bure hapa bila pesa endelea kukaa hadi maji ya pungue ili uweze kuvuka ,ni maneno ya juma alimuonya mogy asivushe watu bure ,oi hamisi wavushe hao wa dada wawili ,ni maneno ya juma alimwambia hamisi awavushe wadada wawili ,hamisi nae alifanya hivyo aliwavusha kisha akapewa pesa na kutia mfukoni ,

Mogy aliwaangalia baadhi ya watu ambao hawakuwa na pesa ya kulipa ili waeze kuvuka pale ,japo watu waliomba sana wavushwe bure ila juma na hamisi walikataa kata kata na kusema haitawezekana ,

Upamde wa pali ile gari ilikuwa imepakiwa tu pale huku mmiliki akiendelea kuchati na simu bila shaka na alikuwa kavalia mavazi yake safi suti nyeusi safi kabisa ,yule mtu alibonyeza simu yake na kuweka sikioni alianza kuongea na simu akiwa ndani ya gari na mazungumzo yao yalienda
"Mzee omari hapa maji yamejaa siwezi kuvuka nije huko hivyo naomba umwagize mtu alete hadi hapa kwenye hili daraja mpe hio bahasha mzee wangu ,"upande wa pili nae alijibu

"Lakini lisu ni vizuri tungekaa wote tuzipitie hizi nyaraka halafu tuone tutafanya vipi biashara yetu au unaonaje lisu ," mazungumzo yao yalichukua muda mrefu ndipo mzee omari alimjibu lissu ,ambae ndio kashidwa kuvuka maji yale
"Lisu hapa mimi sina mtoto wote washaenda shule sasa sioni ngoja nitoke nje nikikutana na mtu yeyote anaekuja huko nampa hizi bahasha aje nazo "akuletee

"Lisu aliitikia ni vizuri ila utume mtu mwenye hakili timamu ,mzee omari alikata simu kisha akatoka nje barabarani na kuanza kutafuta mtu wa kumpa ile bahasha ampelekee mzee lisu ,hawa wazee zaidi ya marafiki japo mzee lisu yeye kwake ni mambo safi hela anazo ,na anaishi maeneo ya sinza ,

Mzee omari aliifunga ile bahasha na nailoni vyema ili isiweze kuloa na maji ,alitoka nje na kumwona msichana mmoja akiwa anatembea haraka haraka huku amejifunika nailoni kichwani ili asilowe na manyunyu ya mvua

Mzee omari aliita ,we binti samahani naomba nikuagize hii bahasha pale darajani utamkuta mzee mmoja kapaki gari pale kashidwa kuvuka kutokana na maji kujaa sana hivyo utampa hii bahasha na atakupa hela walahu ya kunywa chai ,mzee omari alimwamini yule binti si kana kwamba wanafahamiana lahasha alikuwa ni mpitaji hivyo aliamua amwagizie aweze kumpelekea lisu ile bahasha ,
Yule binti alifika kwa omari alisalimia ,shikamoo"marhabaa mzee omari aliitikia huku akiseti vizuri mwamvuli wake .yule binti alimwangalia mzee omari kwa jicho la kuibia ,kisha akaipokea ile bahasha,mzee omari alimwambia
"Binti ukifika pale utaona gari imepaki pale pia kuna vijana wanavusha watu maji pale hivyo atakuvusha pia utamkuta lisu amepaki gari pale utampa hii bahasha

Binti yule aliitikia kisha akaanza safari kuelekea liliko daraja ,kwakuwa halikuwa mbali sana alianza kutembea huku yule binti akionekanika kuchoka mno ,alianza kuwaza yule binti ,mungu nisaidie huyo mtu nikimpatia bahasha yake akinipa hata elfu moja nitafurahi niweze kupata walau chakula ,nahisi kizungu zungu yote sababu ya njaa niliyonayo mimi jamani

Binti yule ambae hatujamjua jina lake aliendelea kuwaza ,mama yangu alivyokuwa hai alishawai kuniambia ,mwanangu ukikua ogopa kutumwa na mtu usiyemfahamu ,utaweza ukakutana na matatizo au unaweza ukatumiwa kisha wakakudhuru ama kukufanyia ukatili wa aina yeyote ,"yale maneno yule binti aliyakumbuka na kutaka kugeuka amrudishie aliyempa ile bahasha lakini alivyogeuka hakumkuta omari alikuwa tayari asharudi kwake ,

Yule binti aliendela kuwaza ,kwanini nimemwamini yule baba ,mmmmm kisha akaguna na kusema mungu nisaidie ila yote nafanya hivi ili nipate pesa ya kula mama uliniambia nikiwa mjini nisiibe ,wala kujihusisha katika matendo mabaya ,bint alitabasamu na kuangalia miguu yake ambae alikuwa kavaa ndala mbili tofauti ,nyingine ya blue nyingine nyekundu ,aliangalia gauni lake ambalo lilikuwa limeloa alitikisa kichwa na kujisemea

Mungu kwanini nateseka mimi ,naomba unioneshe njia nzuri niweze kupumzika ,binti aliangalia mkono wake ambao ulikuwa umeungua na moto alitikisa kichwa kisha na kujisemea ,mama nimemiss ungalikuwepo kwenye hii dunia nikuoneshe mapito ninayopitia

Wakati huo binti ashafika pale darajani aliangalia upande wa pili kweli aliweza kuona gari imepakiwa ,yule binti alianza kujiwazia
"Mimi latifa nitavukaje haya maji ,mungu wangu halafu mwili wangu hauna nguvu sijala siku mbili mmmmh hapa si nitasobwa na na haya maji ,"ni mawazo ya yule binti ambaye kwa jina anaitwa latifa ,aliwaza huku macho yake yameangalia yale maji yalikuwa yamejaa pale darajani ,watu walikuwa wamejaa wakivushwa na akina juma na hamisi huku mogy yeye alikaa pembeni akiangalia watu wakivushwa

Kuna kundi la wanawake saba waliamua washikane mikono waweze kupita kwa pamoja kwenye yale maji kwakuwa hawakuwa na pesa ya kuwalipa akina juma na hamisi wawavushe ,walikubaliana wafanye vile ,
Latifa alilitizama lile gari ambalo ameagizwa apeleke ile bahasha ,hakuweza kumwona mtu ambae kaambiwa ampelekee hiyo bahasha ,kutokana na lilegari kuwa va vioo vya giza ,

Latifa aliwaza ,ukiwa huna pesa hamna kuvuka sasa mimi sina hela na hii bahasha ya watu nitaifikishaje? ,latifa aliwaza wacha niungane na hawa wanawake tuweze kuvuka kwa pamoja kwenye haya maji na nikifanikiwa kufika upande wa pili nimkabidhi huyo mwenye hii bahasha niendelee na safari zangu za kwenda kutafuta vibarua

Wakati huo mogy kasimama karibu na latifa alimwangalia latifa nywele zake zilikuwa zimekaa kihasara hasara alimwangalia miguuni na kugundua amevaa ndala mbili tofauti ,hata alivyomwangalia gauni alilovaa lilikuwa limeloa halafu lilionekanika kuwa ni chafu ,
Mogy alijisemea mmmmh huyu binti mbona yupo rafu hivi ila ... mogy hakumalizia tayari wale wanawake saba pamoja na latifa waliungana ili wavuke kwa pamoja

Wakati upande wa pili hamisi na juma wamesimama kuanza kuwatisha wale wanawake kuwa mkifika kati kati mtapiga mweleka na mtasombwa na maji hamisi alianza kuhesabu mojaaa ,mbiliii nikifikisha tatu kama bado hamjasobwa na maji nitakuwa sio mimi hamisi ,acheni ubahili leteni hizo buku buku tuwavushe
Mnajifanya mnakazaa ee sasa ngoja muone

Wakati huo mzee lisu alishuka kwenye gari huku akiangalia binti ambae kapewa ile bahasha na omari ,maana ashapewa taarifa kuwa kamtuma binti kavalia gauni la blue ,
Ukweli lisu alitizama alimwona yule binti latifa akiwa anavuka maji pamoja na wanawake wengine mkononi alikuwa ameshikilia ile bahasha

Lisu alisema ooh yule pale kisha alitoa waleti yake na kutoa shilingi elfu kumi ,sijui ndo anataka aje ampe latifa ,
Wale wanawake walifika kati kati ya daraja ambae alikuwa anawaongoza alijaribu kupiga hatua bahati mbaya maji yalikuwa na kasi sana yalimzoa taratibu mama aliyumba na kusababisha wanawake wengine kudumbukia kwenye maji wakati huo

Hamisi na juma wanapiga miluzi uwiiii wameeenda na majiii uwii
Mogy kucheki aliona bahasha inaelea kwenye maji ,wanawake nane walidondoka wakaanza kuserereka na maji walianza kunywa maji taratibu huku wakizidi kuelekea kwenye sehemu yenye kina kirefu kwenye huo mto

Mzee lisu alipiga kelele na kusema bahashaaaa ,wakati huo mogy ashajirusha kwenye maji na kwenda kuwaokoa wale wanawake ,huku juma na hamisi nao wanaenda kuwasaidia kuwatoa kwenye maji maana walianza kusobwa
Kibaya zaidi latifa aliangukia pa baya sehemu yenye shimo la daraja ,....


Je nini kitaendelea?

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.