.SUBIRA UVUTA KHERI.
HANCY KUMBILO
0715364116
SEHEMU 15.
ASMA YULE NA SEFU...
ENDEREA..
Watu walishangaa sana hasa kumuona asma ni mzima tena wa afya tele bila kua na kofu wala donda lolote.
Mzee tope nae akamgeukia mkewe na kuanza kuludisha majibu huku akimuita mnafki na ni mtu wa kuigiza .
Asma alifika na kumkumbatia mama ake kisha kumuambia mama ake akutegemea kama wataonana.
Mama alilia kwa furaha kisha kumuuliza kijana alieingia ndani ndo alikuokoa na yeye yuko wapi na mlipitia wapi.?
Mama mimi nimejishtukia tu niko kwake pia huyo kijana ni mzima ingawa yuko amelazwa hospital na huyu ni rafiki yake anaitwa sefu.
Mama alikua akimfahamu sefu na alimshukulu na kuweka wazi hisia zake kwamba anataka kumuona kijana aliemsaidia mwanae.
Upande wa mganga alijiuliza aanzie wapi juu ya msaada wa kijana hassani juu ya kumsaidia.
Aliomba apewe mwezi ili mambo yawe sawa anacho taka kukifanya ni juu kumvuruga akili na kila kitu kwake kiwe juu ya jina la aisha tu na sio mtu yoyote.
Mama asma alimuoma kijana maliki pia mzee tope.
Na kijana maliki alijitolea kujenga nyumba upya ya mzee tope tena kwa kisasa zaidi.
Ilisimama nyumba na ikawa ya kisasa na maisha kidogo kwa kina asma yalikua mazuli.
Kijana maliki aliweka wazi hisia zake juu ya mrembo asma kuwa kwamba ana mpenda na anaitaji awe mke wake ikiwezekana wakaishi wote daresalam.
Hilo swala kwa asma lilikua likimchanganya akifikilia kwamba yeye yuko mtu ampendae aitwae hassni.
Na anakili kwamba kila mtu ana mchango kwake lakini hassani ndie ampendae.
Siku zilienda na hatimae ilifika mwezi.
Kituoni hassani alikuja kuonwa na mama ake .
Mama shikamoo..
Marhaba pole baba.
Nishazoea mama ila zimebaki siku tatu mimi kuenda mahakamani lakini mbona asma simuoni kuja huku anaumwa au anatatizo gani.?
Mwanangu asma yuko mzima likini mambo anayo yafanya siku hizi bola ufute jina lake kwenye akili yako.
Maana mda wowote asma anaolewa na kijana aitwae maliki alikuja kupata umaarufu kijijini hapa pia kufunika jina lako.
Maliki ?. *asma kuolewa mama bhna acha utani*
Mama ako yuko sawa baba angu aliongea mama asma na kufanya hassani akibali kwamba kinacho ongelewa ni kweri.
Mzee tope upande wake akiwa na mwanae asma.
Yaani asma umenifurahisha sana mwanangu kwa kumkubali maliki si unaona mazingilia yame badilika si unaona mwanangu .
Naona baba maana tuna nyumba nnzuli tuna kula tutakacho na kijiji kizima kinajua sisi ni wakina nani chezea TOPE FAMIRY.
achana na mama yako anae kushauli mambo ya hassani eti vuta subra utapata kheri.
Siku hizi mwanangu *SUBIRA AVUTI KHETI* BALI *SUBIRA UVUTA BANGI*
Baba na wewe mimi nishamsahau kabisa na hapa naenda kituoni. Kumludishia vitu vyake hassan na kuhusu mama na yeye kama anampenda sana hassani aolewe nae yeye.
Usiseme hivyo we mtoto.
Anaudhi sasa ana acha kuwa na sisi mda wote yeye na mama HASANI wakidai nyie wabaya na mzee sanadi wakati mmbaya ni kijana wao.
Mimi naenda huko.
Itaenderea