.SUBIRA UVUTA KHERI.
HANCY KUMBILO.
0715364116
SEHEM 11.
ASMA ALIJIULIZA APIGE AU LAA.
ENDEREA.
Asma alikua akijiuliza sana apige simu au asipige akashindwa kupiga nakuamua kutulia ikiwezekana wataonana kesho.
Asubuhi ilifika na asma aliamka nakukuta mama ake amepooza sana ilibidi amuulize mama kuna tatizo gani.?
Mmh mwanangu uyu baba ako mimi simuelewi kabisa juu ya mambo yake.
Kafanyaje tena kweni ujamzoea tu mmeo mzee tope vituko vyake.
Amana bhna hii sasa mpya unakumbuka jana alituambia kwamba ikifika asubuhi furaha yako itapoa na utakua na uzuni.
Nakumbuka mama lakini mbona bado nna furaha maana nna rafiki mpya na amefanya kidogo ata mawazo nisiwe nayo kweni ana mpya gani?
We mwanangu asma tatizo ni hassani..
Mama hassani tena uyu baba simpendi ata kumuona kamfanya nini mpenzi wangu.
Akumfanya kitu ila ni kwamba yule mama ambae ilikua ni mtu wa kuongea ukweri juu ya kesi ya hassani amefariki ndo taarifa zilizo kuwepo.
Baaada kusikia hivyo asma alianguka na bahati mbaya mkono wake uligusa taa iliyo kua ikiwaka ya kibatali.
Hatimaye moto ulianza kushika katika baadhi ya sehemu na mama asma asione.
Alitoka nnje mama asma ili kutafuta msaada kuhusu mwanae.
Kijiji kizima cha chanika kilipata taarifa juu ya msiba wa mama mdogo wa aisha.
Na wengi kiliwagusa kwa wakati tofauti wapo walio amini kutokana na kubakwa imeperekea kufa.
Na wapo walio amini kuperekea kifo chake ni tatizo kubwa kwa hassani.
Hali ilikua sehemu mbili tofauti kubwa zaidi watu walishaanza kuwa na matabaka juu ya tukio hilo walio kwa hassani na wasio muamini.
Watu walikusanyika kwa tajili mzee sanadi ili kuzika na walikua wakisubili mwili tu uje.
Baada ya mda kidg gali lilifika likiwa na mwili huku ndani akiwa mzee tope pia yule mganga akiwa amevaa nguo za kawaida azimuoneshi kama ni mganga.
Walifika na harakati zilianza lakini mda huo huo .
Mganga aliingia upande wa wanawake nakumkamata mama mmoja nakumuuliza samahani kuna kijana namuulizia sijui una mfahamu.
Ni kijana gani huyo baba naweza mjua maana mimi ni mwenyeji hapa.
Anaitwa hassani?
Hassani wako wengi hassani yupi huyo.
Au unakusudia hassani anae singiziwa kwamba kambaka huyu mama aliefariki.
Kwanini mama umesema kasingiziwa.
Mimi ni mama mzazi wa huyo hassani na nnamuamini mwanangu awezi fanya hivyo
Mungu kweri mkubwa na anataka nimsaidie hassani mpaka kukutana na wewe mama mzazi basi kila kitu kitakua sawa.
Kweni wewe nani.?
Usijali mama wacha msiba uishe usitoke mpaka unione tufatane.
Upande wa maliki na yeye alikua njiani kuerekea kwenye msiba na baadhi ya wana kijiji.
Wakati anatupa jicho ili amuone asma ghafla aliona moto ukiwaka kwenye nyumba ya mzee tope nakuwaambia wenzake motoo.
Motooo mottoooo kijiji nacho kikasikia kauli ya moto na baadhi wasio fika msibani walitoka na maji ili kutoa msaada.
Mama asma nae wakati ana ludi aliona moto nakusema mwanae asma yuko ndani.
Itaenderea