.SUBIRA UVUTA KHERI.
HANCY KUMBILO
0715364116
SEHEM 10.
TAFUTA MEMORY CHUMBANI MWANGU HASSANI..
ENDEREA...
mganga alizidi kuchanganyikiwa na kutoa simu kisha kuwapigia simu mzee sanadi na mwenzie.
Walivyo pokea walipewa taarifa kwamba mgonjwa walie muacha ameshafariki.
Walifurahi sana nakujibu kwamba kesho watafata msiba .
Mganga aliitikia nakuomba kesho wakimfata marehemu na yeye awepo kwenye mazishi.
Walimkubalia lakini walimpa shart la kuto kuvaa nguo za uganga avae kawaida tu.
Sawa walikubaliana.
Kjana maliki aliongea sana na asma adi mida ya jioni na asma alimuambia maliki.
Ujue mda umeenda kama vipi nenda kwako mkeo usikute ana wasi wasi na wewe.
Mmmh usinifanye nicheke asma mimi umri huu niwe nimeoa acha utani uyo mpenzi tu sina.
Heee acha uongo maliki kwa ulivyo HB na umaili wa kuongea unakosaje we nambie.
Sena best kwann niwe muongo siku ya kwanza tu kukutana na wewe.
Sawa maliki mimi wacha nikapike maana mzee tope akija chakula bado itakua balaa.
Sawa asma nipe namba yako basi kama autojali rafiki.
Mmh mimi sina simu mwenzio labda nikupe namba ya mama upige uniulizie.
Haaa haaaa alicheka maliki nakuingia mfukoni kisha kutoa simu yake laini zake nakumpa asma pia pesa kidogo ya kusajili laini.
Asma alikataa kata kata lakini maliki alifanya juu chini mpaka asma alichukua nakuondoka.
.uliingia usiku na mganga alikosa kabisa usingizi mala kwa mala alikua akiota juu ya marehemu kuomba msaada wa kusaidiwa hassani.
Mzee tope aliludi kwake nakua nafuraha sana wote walishangaa kwann mzee anafuraha.
Alikaa nakusema mke wangu leo nna furaha sana tena sana na keshi asubuhi ndo nnta waambia lakini mbona ata asma nae kama leo anafuraha.
Walimaliza kula na mzee alimuaidi asma kwamba bola afurahi leo maana kesho lazma auzunike.
Asma alikua wakwanza kuinuka na alivyo fika kitandani aliitoa ile simu nakuanza kujiuliza ampigie simu Maliki au laaa...
*itaenderea*