*SUBIRA UVUTA KHERI*
HANCY KUMBILO
0715364116
Sehemu 8.
Tuombe dua apone..
Endereaa...
Wakati hassan na watu wanao mzunguka wakiomba dua mgonjwa apone upande wa pili wanafanya mpango mama afe.
Basi siku ya pili asubuhi na mapema mzee sanadi na mzee tope walimchukua mgonjwa wakiwa na lengo la kwenda kumuua kwa mganga pia kujionesha kwa watu kwamba wana mpeleka hospital.
Majilani walishuhudia ilo nakujua uenda akapata nafuu mgonjwa ili ukweli ujulikane.
Mama akiwa njiani hali yake ilikua mbaya sana yaani alikua tayali kabisa kuiaga dunia maana alikua apewi huduma za kimsingi kama mgonjwa.
Walifika salama kwa mganga kisha walitoka nae nnje ili wamjuze ni kipi kifanyike.
Mganga sisi atukai sana shika pesa hii huyu mama tunataka umpe ule ugonjwa kama wa wazazi wake ili akifa tuseme ni magonjwa ya kurithi.
Lakini mzee sanadi wewe si ulikuja ili wazazi wa huyu wafe muishi kwa amani.
Ndio ila sasa nataka mali zake ziwe rasmi kwangu ivyo ifanye hiyo kazi kesho tumfate kesho kutwa tufanye yetu.
Yale maneno yule mama alikua akiyasikia nakuanza kulia bila kuongea chochote maana hali ilikua mbaya sana kwake ni kama samaki tu akilia bahalini.
Baada ya kuondoka mr sanadi na mzee tope mganga aliingia ndani nakuanza kufanya mambo yake.
Ila alishikwa mkono na yule mama kisha akajikaza uku akiwa ana ongea kwa tabu.
Msaidie HASSANI nakuomba sana.
Hassani ndo nani..?
Asma mambo yalikua magumu sana kwake akipita mitahani wenzake mda wote wanamcheka na wengine wakimuona kama ana kasoro katika mapenzi nakusema . *bwana ujamtimizia ndo mana kafata vikongwe*
Alikua anaumia sana siku hiyo alikua amekaa barazani akiwaza nini afanye juu ya yeye na maneno ya jirani ghafla alikuja kijana mmoja hivi kwa sura ni mgeni machoni mwa asma
Mambo...dada.
Safi nikusaidie nini..?
Upande wa mganga mama alichukua karatasi kubwa nakuandika kitu na pia akampa kile kikaratasi mganga na hapo hapo akakata roho.
Mganga alishtuka sana nakujiuliza maswali mengi kubwa zaidi ni kujiuliza juu ya yeye kumsaidia HASSANI.
HASSANI NI NANI.?
Alianza kusoma barua ni iliandikwa hivi.....
Itaendere