Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SUBIRA HUVUTA HERI SEHEMU YA 02

.SUBIRA HUVUTA KHERI.
  HANCY KUMBILI
    0715364116
     SEHEM 2.

ALIKUFA NINI PALE KISIMANI..... 

ENDEREA...

Heee ulijuaje mme wangu kama hassani alipata ajali kisimani.?

Mimi nimebahatisha haya nauo msiba kuzika saa ngapi?

Hivi wewe ni baba wa aina gani kwa mtoto wako mimi nnayo yasikia ayo maneno yanayo miminika juu ya mpenzi ambae ni mpendae.

Alafu na wewe mshenzi mimi naongea na mama ako wewe paka wa hassani nenda kwa nyau mwenzio mshenzi.

Aliinuka bibie ASMA na akiwa analia sana huku akiona kama katengwa na familia yake juu ya mapenzi yake kwa alie sahihi kwake.

Upande wa HASSANI alikua kwenye wakati mgumu juu ya kuamua kutoa msaada alianza kunyata huku akimuuliza alie chooni .. mama nini kime kukuta huko mpaka una omba msaada .

Wewe ni nani kwanza unaetaka kunipa msaada .,

Mimi ni HASSANI KUMBILO. na bila shaka wewe ni mama ake AISHA mdogo si ndo hivyo.

Ooh kumbe wewe mkwe wetu ila ili tatizo ina bidi aje mtoto wa kike mwanangu maana niko uchi alafu nimepatwa na ugonjwa wa kuanguka.

Hassani ilibidi atoke ili amtafute bint aje kutoa msaada ghafla alisikia sauti ya yule mama ikitoka chooni akiwa analia pia aliona damu nyingi zikitoka kutokea chooni.

Hassani aliinama nakugusa ile damu kisha kunusa akagundua si damu za ada ya wanawake bali ni damu uwenda mama kapasuka baada kudondoka na anajikaza tu kwakua anaetaka kutoa msaada ni mwanaume.

Kijana akauliza mama uko sawa kweri.?

Mamaaaa. Mama.. we mamaa. Aliita sana lakini kimya ilibidi apitishe mkono kisha ajalibu japo kujua nini afanye.

Alianza kupapasa chini ya choo atimae aligusa mwili wa yule mama maeneo ya kichwani nakuisi kashika damu ambayo inatoka kichwani.

Aliinuka nakuanza kujiuliza ataingia vipi kutoa msaada na mlango umejifunga kwa ndani kuna nafasi tu kidogo kupitisha mkono wake chini.

Aliangalia pembeni kisha akaona shoka nakuchukua ili kuvunja mlango .

Alianza jitiada hizo kisha kufanikiwa kuvunja mlango .

Alimkuta mama kalala chini uchi alijikaza kijana hassani nakutoka nnje ili atafute nguo za kumfunika yule mama.

Upande wa mzee tope na familia yake nako .

Hivii mzee tope mambo gani haya ambayo wamfanyia asma na hassani kweni wamekukosea nini?

Yaani ata wewe mke wangu nikisikia upo pamoja na asma juu ya mahusiano na hassani wala sioni tabu kukuacha tena taraka tatu.

Mmmh mme wangu kweni kisa nini .?

Unataka kujua kisa nini...?

Kwa hassani mambo yalikua mabaya sana.
Kweni wakati anatoka tu mule chooni ili afate nguo za kumstili yule mama.

Alikutana uso kwa uso na MZEE SANADI akiwa na mwanae aisha pamoja na mke wake mkubwa.

Na mda huo HASSANI alikua ameshika shoka mkono wa kulia.

Mlango ulijifungua kwa upepo na walio nnje waliona mtu ndani akiwa anatoka damu pia akiwa uchi.

Hassani umeua...?


   Itaenderea .

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.