Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SITO ISAHAU SEHEMU YA 04

*SITO ISAHAU*
HANCY KUMBILO
0715364116
  SEHEMU YA NNE.

ILIPO ishia .. ghafla azizi aliona wale watu wenye shuka nyeupe wakitokwa na damu midomoni.

Enderea sasa...

Wale watu walikuja nakumbeba azizi .

Alvini mda huo alikua kalala na hata ajui kinacho enderea. 

Upande wa kikeni maria aliamka nakutupa macho yake.

Kumtafuta mama ake na salome lakini akuwaona na alivyo muangalia khadija au ummy.

Nae pia alikua amuoni na msibani alibaki yeye tu upande wa wanawake alianza kua na hofu kisha kuchukua simu yake nakumpigia kaka ake alvin. 

Alvin simu iliita lakini alikua kwa usingizi.
Alivyo piga kwa azizi nako simu iliita tu.

Akawa na wasiwasi mkubwa na mda huo ulikua ni usiku sana na alisikia sauti za ajabu.

Kama mtoto wa kike hoffu ilimjaa na akikumbuka kilicho semwa na azizi usiku wa jana ndo kabisa.

Aliona bora ampigie shoga yake ummy.
Simu iliita na akapokea .

Maria ungejua sehem niliko usinge piga.

Mhh ummy na wewe ungejua nilivyo ungewai kupokea.

Heee makubwa mwenzio niko njiani nakuja kwenu maana usingizi auji kabisa nna Hoff kubwa na mume wangu.

Bora shost uje maana ata mimi nimeaamka simuoni mama wala salome.

Na leo wanawake awajalala hapa.

Nakuja maria.
Fanya haraka naogopa etii maana mumeo adi kaka awapokei simu.

Upande wa azizi hakika alijuta kuzaliwa maana alifikishwa makabulini nakupewa kazi ya kufukua maiti za walio kufa dhamani.

Na alikua akimuona kwa macho yake mr robbat. 

Alifanya kazi usiku kucha na alivyo fukua maiti kama ya kike anaambiwa akate ziwa.
Na kama yakiume anakata sehemu nyeti.

Ili asipigwe ili mladhimu afanye huku akiwa anajiuliza kua anaota ama kweli.

Baada ya zoezi hilo alipandwa kama farasi na bibie Salome nakumuamulu amludishe kwao.

Dada salome tuachie sie uyo kijana maana tulipewa adhabu na mkuu kulima heka saba sasa akatulimie dhamu yetu.

Mama alvin alimuambia salome awaachie azizi.
Lakini aliwapa sharti kwamba wamludishe asubuhi na wamueke sehemu ambayo watu wakimuona wata shangaa.

Ummy alifika mpka kwa kina maria. Nakumkuta maria kweri yuko peke yake.

Aya wewe mwanamke wivu gani mpka mda huu usiogope kukabwa.

Amna maria ila tuache hayo uyu mama ako na mwanae wako wapi?

Mi ata sijui lakin ummy ujue mimi siwaerewi erewi etii.

Basi tuwatafute . Walianza kuwatafuta valandani holaa.
Ukumbini hollaa.
Barazani hollaa.

Sasa maria watakua wapi hawa viumbe .?
Embu twende tukamuamshe mumeo na kaka tutapata akili za wanaume na tutajua ni nini kinaenderea.

Walifika lakini walimkuta alvin tu kalala na pembeni kuna shuka la azizi.

Ghafla shuka la azizi likapotea na wao walishuhudia . Wakapiga kereree.

Ndipo alvin na wanaume kadhaa waliamka nakuuliza kulikoni.?

Kaka nimeshuhudia kitu kina potea kama upepo hapa kweni shuka lilikua hapa lakini ghafla Amna.

Haaaa haaaa haaaa haaaa walicheka watu nakusema maria unavuta bangi nini..?

Alvin akawauliza na hapa kwa wanaume mumefata nini pia shemeji si ulilala kwako wewe. 

Kaka ummy nimempigia simu mimi maana kule uwani mama na salome siwaoni sasa peke yangu naogopa.

Alafu shemeji mbona ata mume wangu azizi simuoni .

Jaman mbona munanichanganya akili. Aliomba majirani wapumzike yeye anaenda huko uwani.

Akiwa anajiamini alvin alifika mpka uwani kisha kuwasha taa ilivyo waka akawaona mama ake na ndugu yake salome wako wamelala.

We shemeji na maria mama si huyu hapa.

Walishangaa mtu na rafiki yake . Swali likabaki moja azizi yuko wapi.

Alvin alitoa simu nakumpigia azizi ajabu simu iliita katika mfuko wa alvin.
Alitoa nakuuliza kwa sauti imekujaje mfukoni mwangu hii simu.

Alivyo kata alvin ikaingia namba ngeni.
Alipokea hallo haloo.

Ummy alicheka nakumuambia weka loudspeak simu kimeo hiyo.

Alivyo weka ilisikika sauti ya kike ikisema. *HELLO SHEMU ALVIN NINA KUPA TAALIFA KWAMBA AZIZI NIKO NAE GUEST MUEKEE SIMU YAKE VIZULI NA ASUBUHI AKIJA KIDUDU CHAKE UMMY MDANGAJE LOLOTE*


...ITAENDEREA..
IN COMMENT KWA MAONI RUHSA.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.