TAXI DRIVER SEHEMU YA 18
Shemeji amekubana nini naona kimya?" alianza hivyo Roi mara baada ya simu hiyo kupokelewa. "Hapana sina mtu wa kunibana kwanza sijakufahamu ni nani mwenzangu?" ukajibu upande wa pili wa simu. "Roi hapa naongea," "waoh! Samahani bwana, unajua kazi zetu hizi ukirudi nyumbani nako nyumba inakutazama uifanyie usafi, ukimaliza vyote vinavyokuhusu uko hoi,"
"Pole sana, kwa hiyo utakuwa umechoka sana hadi sasa?" akatupa chambo. "No, leo sikuwa na kazi za hivyo na hapa pia sina kazi yoyote naangali sinema tu,"
"Ooh! Njoo basi Mtendele Hotel tubadilishane mawazo,"
"Muda huu?"
"Ulikuwa unapendekeza muda gani mtoto mzuri, nadhani kwa majukumu yetu huu ndiyo muda wa kujiachia, nina siku nyingi sana sijauchangamsha mwili kwa vinywaji vikali nadhani kampani yako itafaa zaidi,"
"Ni vinywaji tu au kuna mengine?"
"Kama yapo mengine pia itakuwa si dhambi maana inaruhusiwa na jinsia zetu," Akasema Roi na kumfanya SP Asna acheke kasha akasema ndani ya dakika tano atakuwa amekwisha kufika hapo tayari. Simu hiyo ikakatwa lakini simu nyingine ikaingia na alipotazama ilikuwa ni ya Cat akaguna mh! "Anataka nini naye huyu saa hizi mbona amekuwa na hisia kali hivi?" akajisemea Roi akaipoke. "Kuna kazi bila shaka babu anataka kunipa maana tangu anizuie kushirikiana nawe hakutaka kuniruhusu kuondoka hapa mjini lakini leo amenitaka niwe tayari kwa safari ya kurudi Morogoro na ni muhimu. Hii inaweza kuwa kesho kutwa hivyo hakikisha kesho ukimaliza ratiba zako unakutana nami nikuage kabla sijaondoka maana sitaki umpe mwingine penzi langu," Ulisema upande huo wa pili wa simu hiyo. Roi akamwambia asiwe na shaka ifikapo kesho jioni wataonana maana asubuhi kuna kazi ni lazima aitimize kwanza. Maongezi yao yakafika tamati, Roi akatabasamu na kucheka kabisa baada ya kuona kuwa kile alichoambiwa asikifanye anakwenda kukifanya kwa wakati huo na mtoto mzuri.
Saa mbili usiku iliwakuta maeneo ya Mtendele Hotel, wakatafuta mahala pazuri kwanza wakaketi wakipiga soga za hapa na pale kabla ya muhudumu kufika hapo kusikiliza mahitaji ya wateja hao. Roi alimgeukia muhudumu mara baada ya kufika mahala hapo kasha akamwambia kuwa amsikilize huyo dada hitaji lake huku yeye akinyanyuka hadi mahala pa kupokelea wageni. Akafanya taratibu za malipo ya huduma ya chumba alipomaliza akarudi mahali pa unywaji na maakuli kwa ajili ya lile na hili. Jicho la kijana huyo lilikuwa likimtazama dada huyo kwa kumtamani kabisa kuanzi usoni kuja kifuani hadi maeneo ya kiunoni ambapo ndipo alipokomea na hivyo ni kwa kuwa pia alikuwa haoni vizuri kutoka na meza kukinga lakini kama angelikuwa anaona hadi chini basi komeo lake lingekuwa ni mapajani mwa binti huyo. Sifa na simulizi za hapa na pale zilipokwisha wakanyanyuka na kuelekea ndani ya Hoteli hiyo tulivu ndani ya Chuda pembeni kidogo ya mishemishe za jiji hilo la Tanga. Walikuwa watu wazima hivyo hawakutaka kuzitesa nafsi zao kwenye jambo la hamu kama hilo, kama wewe hutaki ni wewe na roho yako ya mkono wa birika lakini watoto wazuri kama SP Asna hawana choyo na Mungu alichowatunukia bwana.
Hatua zao za taratibu ziliwafikisha mahala ngazi zilipo wakazikwea taratibu kuelekea juu, hawakutaka kutumia lifti kwani chumba chao hakikuwa mbali sana ni eneo la mwanzoni mwa ghorofa hiyo. Wakaingia kwenye chumba hicho na kijana huyo akamkaribisha binti huyo kwa ukarimu kabisa huku akimkumbatia kwa nyuma na kumuangushia kitandani ambako alianza kubingilia nae huku wakigusana hapa na pale na kutekenyana hatimaye mchezo huo ukatoka kwenye utani na kuingia kwenye ukweli thabiti kabisa, mzunguuko wa kwanza ukachezwa vema kitandani hapo na walipomaliza wakakimbilia bafuni ambako walioga na kurudi tena chumbani. Wakiwa wanataka kuanza mtanange mpya wa kuzimaliza hamu zao za kukutania hapo, simu ya SP Asna ikaita kutokea kwenye begi lake la mkononi. Akalivuta begi hilo na kuitoa, mh! Akagumia baada ya kuitazama simu hiyo kiooni. "Vipi?" Roi akatupa swali akiwa anamtazama binti huyo kwa umakini zaidi. "Mkuu ananipigia simu saa hizi! Saa tatu hii kuna usalama kweli na si kawaida yake na pia mimi sina kazi tena kazi zote zinazohusiana na kesi hii ya mauaji imehamishiwa kwa Ispekta Musa!" akasema akiwa na hofu kidogo machoni mwake. "Ifahamu kazi yako kuwa unaweza kuhitajika mahala popote na wakati wowote haijalishi kuna nini ama jambo gani, pokea simu," akasema Roi huku akimtoa wasiwasi binti huyo. SP Asna alipotaka kuipokea simu hiyo ikakatika kutokana na kuita kwa kitambo kingi. Muda wa kama dakika moja nzima ukapita bila hiyo simu kuita tena kiasi mwili wa SP Asna ukaanza kupata baridi asijue nini kimejiri. "Nimpigie?" akauliza lakini Roi akampa ishara ya kutokufanya hivyo akamtaka awe na subira kwanza. Kweli baada ya sekunde kadhaa za kusubiria, simu ikaita tena. Akaipokea. "Halo mkuu!" akaongea baada ya kupokea. "SP nini tatizo, unataka kuniambia muda huu tayari umelala? Kwanini napiga simu masaa yote?" Ikauliza sauti hiyo iliyokuwa inafanana kila kitu na Kamanda Mwakisalu. "Sikuwa nimelala mkuu...."
"Kwanini simu inaita masaa yote?"
"Nilikuwa bafuni mkuu na niliporudi ndipo nikaikuta simu inaita, samahani sana afande!" akajibu SP Asna. "Ok, achana na hilo, nimekupigia simu nikuulize kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha yule jaji mstaafu....!"
"Si nimekabidhi kila kitu kwa Inspekta mkuu na ukaniamrisha nikae pembeni na uchunguzi ule ungefanywa na yeye, kuna nini tena....!" alikatisha sentensi ya upande huo wa simu uliokuwa ukiongea lakini hata yeye kauli yake haikufika mwisho ikakatishwa. "Sikia sasa, najua kuwa kila kitu hakiko mikononi mwako ila ninachotaka kutoka kwako ni kuhusu mahojiano ya ndugu wa dereva Taxi aliyeuawa sawa na jaji, maana ndugu zake jioni ya leo wamekuja hapa kituoni na kutoa lawama juu ya upelelezi wa kesi ya ndugu yao na wanaona nguvu zote zimeelekezwa kwa jaji mstaafu, njoo kwenye ukumbi wa polisi (Polis Mess) utanikuta hapa nje nakusubiri kwani hadi sasa mambo yanaonekama kuwa magumu zaidi," aliongea mtu huyo. SP Asna akasimama kitandani na kumfanya Roi amshangae na hasa macho yake yakiwa chini ya mapaja baada ya mtoto huyo mwenye umbo tata kusimama kwa kutanua mapaja yake. "Lazima nitii sauti ya mkuu wangu," akasema SP Asna na kushuka tokea kitandani pale na kuvaa nguo zake lakini Roi akamkumbatia kwa nyuma. "Sijakufaidi lakini mpenzi?" akalalama huku mikono yake ikiminya matiti yaliyovimba vema ya binti huyo. "Najua, wacha niende kama nikimaliza mapema nitakutaarifu unipeleke hata nyumbani na utakwenda kulala kwangu kwani hata mimi nakutamani zaidi, ni mtamu sana mwanaume," alijibu askari huyo na kuvaa kasha akaokota mkoba wake, simu akatoka. "Usafiri gani unatumia?" akauliza Roi. "Bodaboda," akajibu Asna. "Unauhakika lakini kuwa huyo mkuu ndiyo amekuita?"Ndiyo, ni yeye na anataka majibu ya kuhusu tuhuma za ndugu wa dereva Taxi aliyeuawa maeneo ya shule ya sekondari ya Mkwakwani maana hawaelewi hadi muda huo nini kinaendelea na hawajashirikishwa,"
"Wapi makutano?"
"Ukumbi wa polisi Forodhani mkabala na Maktaba," akajibu Asna kasha akaufungua mlango na kutoka kwa kasi kubwa huku akiwa anashuka ngazi kama anayefukuzwa kiasi cha kuwashangaza wahudumu wa hoteli hiyo. "Kwema dada?" akauliza dada wa mapokezi baada ya kumuona dada huyo akitoka mbio. "Usalama upo msijali ni majukumu tu ya kikazi," akajibu huku akiuvuta mlango wa kioo ulioweza kumtoa nje na kutoka kabisa nje ya uzio huo alipotoka barabarani, bahati ikawa kwake kwani kuna pikipiki iliyokuwa ikipita ikiwa tupu kabisa hivyo hakupata shida kuita bodaboda. "Wapi?" akauliza dereva huyo. "Ukumbi wa polisi tafadhali.
Kengele ya hatari ilikuwa ikigonga sana kichwani mwa Roi mara baada ya binti huyo kutoka na ilikuwa ikimnyima raha kichwani mwake, alijiuliza mengi sana kuhusiana na wito huo wa ghafula na jinsi matukio ya wito wenyewe yalivyoungwaungwa, akajiuliza mengi kuu likiwa ni madereva Taxi wangapi wamepoteza maisha kwenye mlolongo huo na hakuna taarifa kuwa watu hao wamejazana kituoni kuhoji kuuawa kwa ndugu zao. Hili likawa ni baya zaidi kwani kila akilijengea usawa apate kulielewa lilimkatalia. Akavaa fulana yake nyeusi na kutumbukiza raba zake nyeusi pia miguuni baada ya kuvaa suruali yake na kutoka kwa mwendo wa haraka lakini usio leta hofu kwa kila anayekutana naye. Aliingia kwenye gari yake na kuondoka kwa kasi kubwa kuelekea mahali binti alipoelekea. Alipofika mahali hapo Asna alimlipa dereva wa bodaboda ujira wake kasha akaangaza macho yake huku na huko kasha akapiga hatua kuelekea ndani ya ukumbi ambako kulikuwa kukisikika muziki wa kileo ukipigwa kwani siku hiyo ukumbi huo ulikuwa umekodishwa kwa shughuli binafsi za harusi. Wakati akiwa anazidi kupiga hatua, Roi naye akawa ameshafika mahala hapo na gari yake akijifanya kuitafutia maegesho gari yake, akaja hadi upande ambao kuna ofisi ya halmashauri ya jiji sambamba na benki ya CRDB na kutulia hapo lakini hakuzima gari wala kutoka nje. Tayari macho yake yalishamuona Asna akiwa anapiga hatua kuelekea ndani ya ukumbi lakini ghafula tu akasita na kupokea simu na kuiweka sikioni kasha baada ya muda mdogo akaonekana jinsi ambavyo akiangalia huku na huko hadi macho yake yalivyokomea kwenye gari ndogo 'Vitiz' yenye rangi ya nyeupe. Akaonekana akipiga hatua kulielekea lile gari, Roi akachukua kamera yake yenye nguvu na kuivuta ile gari kasha akaipiga picha kwa nyuma halafu akatulia. Asna akaonekana akiwa ameikaribia ile gari akafunguliwa mlango lakini akawa anasita kuingia kwa sekunde kadhaa ndipo akaingia. Zilipita takribani dakika kumi na tano bila mtu yeyote kushuka wala gari ile kuondoka, zilipotimia kama dakika ishirini na tano hivi tangu Asna kuingia garini mule, mlango ukafungulia na kushuka mwanaume mmoja, Roi akamvuta na kumpiga picha. Alikuwa mweupe lakini mikononi mwake kukiwa na soksi nyeusi. Roi nywele zikamtikisika kichwani mara baada ya kuona jambo lile na mtu yule akivuka barabara na kuja upande wa pili kama ajae kijiji cha ishirini na moja kasha akapanda gari iliyokuwa imeegeshwa mahali na kutoweka lakini pia kijana huyo alifanikiwa kuipiga picha gari ile. Akateremka garini mwake na kukimbilia kule ambako kulikuwa na ile gari ambayo mtu yule alishuka, alikwenda kwa umakini mkubwa sana hadi alipoikaribia. Akachungulia ndani kupitia kioo lakini kwa macho ya kidadisi zaidi, hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya SP Asna aliyekuwa amelalia kiti kama aliyetopea usingizini. "Shit!" akang'aka baada ya kuona jambo lile akarudi garini mwake na kuondoka huku akitoa maelekezo simuni baada ya kujihakikishia kuwa SP Asna hakuwa hai tena. Akatoa maelekezo mahali yalipofanyika mauaji hayo kasha akanyoosha goti hadi majengo mahali lilipo jingo lake jipya kwa ajili ya kazi.
****
Hali ya hatari si kwa jeshi la polisi tu pekee bali hata kwa upande wa pili wa sarafu hali ilikuwa ya hatari zaidi. Kulikuwa kuna taarifa moja nzito sana iliyofika mezani kwa Hasheem nayo ni kupoteza maisha kwa Hudah baada ya kuchezea kipigo kutoka kwa Moni na alipotaka kuharibu hali ya hewa, dereva Taxi Tom mwenye uchungu na hasira dhidi ya mauaji ya watu wanaojihusisha na kazi yake yanavyozidi jijini hapo, akamkung'uta risasi ya paji la uso kwa kutumia silaha iliyoachwa garini mule. Kifo hiki kilikuwa ni ishara mbaya sana kwao na walijua kwa vyovyote vile hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwao. Walipanga mikakati ya kuwamaliza maafisa wa jeshi la polisi ambao wamekalia kiti cha uchunguzi wa vifo vilivyokuwa vikiendelea jijini hapo lakini kumbe wakati wao wakiwa wanapanga na kubahatika kutekeleza kifo cha SP Asna aliyepata kugusa upelelezi wa kifo cha Jaji mstaafu, huku kuna kijana aliyekuwa akimtegemea kwenye kazi kwa umakini wake amedondoshwa. Na nani? Hapo ndipo palipokuwa na kitendawili kizito sana katika kukifumbua maana hata wategaji hawakujulikana ni akina nani. Hasheem, mzee mwenye ngozi iliyoanza kusinyaa kwa ajili ya kusurubiwa na uzee ulionza kuomba makazi mwilini mwake, weupe wake wa kufifia kutokana na kuchangia damu mbili tofauti akiwa na mama Mshirazi mweusi na baba mwarabu wa huko Pemba. Pua ndefu iliyochongoka macho yake yenye mboni nyeusi huku yakiwa yameingia ndani kidogo, mashavu yaliyoingia ndani na nywele zake za maboya kama paka asiye na afya njema. Vilitosha kumfanya asiwe na muonekano wa kupendeza hata kidogo. Roho mbaya aliyokuwa nayo na tamaa ambayo alipata kutunukiwa na Shetani mara baada ya kuonekana si mtu wa kuridhika kwa kile apewacho na Maulana, vikamfanya azidi kuogopesha maradufu. Kamasi nyembamba kuashiria hasira zilimtoka kama maji. Hatua za viatu vya mchuchumio zilizokuwa zinakuja hapo alipo, zikamfanya azivute kamasi ndani kwa nguvu na kuzimezea kooni kasha akajikohoza na kutulia maana alijua fika ajaye ni binti yake.
"Kuna simu yako baba, sebuleni," alisema binti huyo mrefu mwenye nywele ndefu nyeusi huku akiwa amevaa mavazi meusi tupu. Hasheem akasimama na kuelekea mahali alipoambiwa kuwa simu yake ipo. Alikuwa ni mzee lakini mwendo wake ulikuwa ni wa kikakamavu sana kama vile hakuwa mzee, waweza sema ni ngozi tu ya kizee ndiyo imevishwa mwilini mwake lakini alikuwa ni kijana. Akafika mahali simu ilipo akaikuta inaita akainyakua na kuiweka sikioni. "Vijana niliowatuma kazi wamefariki wote hakuna hata mmoja aliyebaki na nyumba imebaki tu kwa sasa haina hata samani moja huwezi amini!" ilisema sauti ya upande wa pili wa simu hiyo. Inamaana Roi baada ya kutoa kichapo, Kasa akaibuka na vijana wakasafisha nyumba na kuacha maiti kama zilivyo. Ngoma nzito.
Mbona mapema hivi inamaana huyo mtu au watu hakuna hata mmoja aliyekufa?" akauliza kwa sauti ndogo kiasi cha upande wa pili kutokusikia vizuri mtu huyo anachokiongea. Hadi kupelekea kuuliza ili apate kusikia vema.
ITAENDELEA