CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)
MTUNZI: Minnah De Embaccas
SEHEMU YA KUMI NA NNE (14)
Whatsapp :0656282898
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU: "kimempata nini mwanangu jamani".aliongea huku analia akielekea alipokuwa anapelekwa na wazazi wa vicent, wakamweka kwenye benji na wao wakakaa ili waanze kumueleza. Dokta baada ya kuona mambo yamekuwa sawa akafungua mlango wa ofisi yake ili aingie, mara akamsikia nesi anakuja mbiombio huku anamwita "doctorrrrrrrrrrr".. ENDELEA.....
Anamwita "doctarrrrrrrrr". Ilibidi dokta yule asitishe ile lile zoezi la kufungua mlango ili aingie ofisini kwake, akasimama ili asikilize kilichomfanya nesi kumuita kwa nguvu kama vile. "doctar yule mgonjwa wa kiume ameamka".sio daktari tu hadi wazazi wa vicent, pamoja na ndugu wakiwemo rafiki zake wakachomoka mbio kwenda kumuona. Ila daktari akawaambia kwamba wasubiri nje kidogo ili aangalie afya yake alafu ndio hata waruhusu wapite. Muda wote mama niram, alikuwa amekaa kimya pembeni ya benji alikuwa mlinzi wake akizidi kumliwaza na kumpa moyo. Mara kule chumba cha vicent daktari akatoka. "sasa jamani inabidi tufate utaratibu,mgonjwa ameamka na yuko vizuri ila hairuhusiwi kuingia wengiwengi inabidi waanze wazazi wake kwanza". Aliongea daktari, lakini kabla ya kauli kumaliziwa, mama na baba yake vicent walichoropoka na kuingia ndani kwa mtoto wao. Ilibidi wakina suma na richard na wengineo wafuate utaratibu walioambiwa. Walimkuta vicent amefumbua macho huku akatabasamu baada ya kuwaona wazee wake. "mwangu jamani siamini".alisema mama yake huku anambusu mashavuni. "pole sana kijana wangu ".alisema baba yake huku anamtazama kwa macho ya upendo wa hali ya juu. "baba na mama niram wangu yuko wapi".lilikuwa swali la vicent mara baada ya kuamka kutoka kwenye usingizi wa kifo ndio kwanza alikuwa anaongea. Wazazi wake walitazamana kisha baba yake akasema. "ajambo na alikuwepo ila amesema kaenda kubadilisha nguo na kukuletea chakula". Vicent alivyosikia hivyo akatabasamu na kujawa na furaha moyoni, wala hakumkumbuka Vanessa hata kidogo na hakumuzia . "marafiki zangu wako wapi? ". Aliuliza vicent. "wako hapo nje ngoja nikakuitie ".alisema mama vicent huku anachomoka mbio kwenda kuwaita. Vile alivyokuwa anakimbia ungesema binti wa miaka kumi na sita. Mara baada ya sekunde chache wakina suma wakaingizana . "aisee siamini mshikaji kama upo nasi ni jambo lakumshukuru mungu".aliongea richard na wote wakaitikia " emeeeeen". "pole sana Kamanda wangu Mungu Atafanya wepesi wake utapona tu".aliongea suma na vicent akaitikia kwa kichwa kuonyesha, amekubali maneno ya rafiki yake huyo. Basi ndugu nao ilipo fika zamu yao waliingia kwenda kumuona vicent.
*********
Saa sita juu ya alama. Baba yake niram alifika hospitalini, nakumkuta mkewake amekaa pamoja na watu wengine tofauti ila akawa ameshajua watakuwa ni wakina nani maana mkewe alimuhadithia kila kitu kwenye simu baada ya yeye kuelezwa na wazazi wa vicent yaliyotokea. Mama niram alipomwona mumewe akaanza kulia huku ananyanyuka kumfuata kule alipokuwa anakujia.mzee Popati nae akubaki nyuma akawa anamfuata mkewe wakakutana kati,wakakumbatiana kwa muda huku baba niram akimpigapiga mkewe mgongoni kumtuliza. "pole mama nyamaza, mkewangu kila kitu kitakuwa sawa ".aliongea baba niram, huku akimkokota mkewe na kwenda kumuweka kwenye benji. "mmewangu toka jana mpaka sasa ajaamka naumia mimi".alisema mama niram huku analia japo sasa hata machozi hayakutoka kwa wingi maana macho yalivimba kupita kiasi, na sauti ilimkauka. Wazazi wa vicent walienda kumlaki mzee popat maana walishakuwa kama ndugu, na baba niram wala hakuonyesha chuki kwakuwa alijua ni mitihani tu japo ni vigumu kwa familia yao kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na jamii nyingine lakini niseme tu kuwa mzee huyu alikuwa na busara sana. Vicent alipelekewa chakula na mama yake kilicholetwa na msichana wa kazi. Lakini akashangaa niram amuoni ikabidi aulize. "mama niram yuko wapi".mama yake akawa kimya asiwe na chakumjibu. "mama mbona unijibu ".aliuliza tena vicent huku akiwa amemkazia macho mama yake bila kupepesa. akamuona mama yake analia hapo Vicent akajua mambo ayakuwa mazuri, kwanini mama yake alie baada ya kumuulizia niram.alijiuliza lakini jibu alikosa."mama mbona sielewi unanivuruga ujue".aliongea vicent,akionyesha kupanic kwa kutoeleweshwa kitu kinachomuhusu mpenzi wake huyo. Baba yake alivyoona vicent amepanic akaona asije akafanya mshono ulioshonwa ukapata kufumuka. Haraka sana mr ngosha akaketi pembeni ya kitanda cha mwanawe nakuanza kumuelezea hali halisi hakumficha chochote alimwambia kila kitu. "nataka nikamuone baba".aliongea vicent, lakini mama yake akamuwahi "bado ujapona vizuri utatonesha kidonda".aliongea kwa kusisitiza mama vicent. "nimesema nataka kumuona mpenzi wangu anaepigania uwahi wake sasa hivi kwaajili yangu nataka kwenda kumuona ".aliongea vicent huku akimaanisha alichokuwa anakiongea. "vicent tulia kwanza".aliongea mama vicent,lakini baba vicent akaingilia. "mwache akamuone huyu ni mtoto wa kiume usimlee kama yai".aliongea baba vicent huku akimsaidia mwanae kumnyanyua na kumpakiza kwenye baiskeli za walemavu ili kumpa msaada wa kuweza kuenda kumuona mpenzi wake. Vicent tayari alikuwa ameshaketi chini kwenye kile kiti baba yake akaanza kumkokota. Nyumba akifuatiwa na mama mkewake ambae alionyesha kutokupendezwa na lile tukio la kutoka ndani kinguvu. Walipofika nje watu walikuwa wamepungua hata wakina richard hawakuwepo,walienda majumbani kwao ikiwa kubadilisha nguo au kupata chochote kitu ili kupasha tumbo. Pale kwenye Benji alibaki baba niram na mkewe wakiwa wametulia nje ya chumba cha binti yao. Sasa wakati vicent na wazazi wake wanawakaribia mara kile chumba cha niram akatoka nesi mbiombio huku anamuhita daktari .hakuna aliyebaki nyumba si wazazi wa niram wala wazazi wa vicent pamoja na vicent mwenyewe aliesaidiwa na baba yake kwenda chumba cha niram .wakamkuta anarusharusha miguu huku macho kayatoa na baada ya dakika akatulia vilevile. Mama niram alizimia palepale vicent alinyanyuka mwenyewe kwenye kitu sijui hata nguvu alizitolea wapi akaenda mpaka kwenye kitanda alicholala niram, akamnyanyua huku anamtikisa tikisa, lakini wapi niram alitua vilevile. Vicent alikuwa anaangaika kumuita huku analia kwa sauti maana hakutaka kuamini kile alichokiona. Ila ghafla akaingia dokta mkuku mkuku, akaenda mpaka alipo vicent akimuomba amwachie niram ili amfanyie vipimo,lakini vicent alikuwa mbishi alimng'ang'ania asitake kumuachia. Ila baba yake niram na baba yake mzazi walimchukua kwanguvu maana alikuwa ashikiki na baba yake akamvutia kwake huku ana mtuliza.dokta baada ya kumpima akaganda asijue, atumie lugha gani kuongea ili aeleweke. "dokta nini mbona uongei?".aliuza mzee Popati huku mkewe akiwa ametolewa nje apate hewa. "tuambie basi niramu kimempata nini? ".aliuliza vicent huku anamtazama daktari. "nananana.. nasikitika kusema kuwa mgonjwa ametutoka".aliongea daktari kwa kigugumizi lakini aliongea kwakutimiza wajibu wake. "whaaaaaaaaaaaaat".vicent aliongea uku akijibwaga chini kama gunia puuuuuuuuuuuuh!! gonga like, kisha toa maoni au mtazamo wako kupitia comment..... Itaendelea ......