Notification texts go here Contact Us Buy Now!

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA KUMI (10)

CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu)

MTUNZI: Minnah De Embaccas

SEHEMU YA KUMI (10)

Whatsapp :0656282898

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA: Sasa alijiuliza ilikuwa mpaka shetani akapita katikati yao.kiukweli alijilaumu sana alijuta kwa alichokifanya "daah mshikaji yupo poa sana yule hanaga tabu na mtu mzungu sana yule sijui hata ntaanzaje kumtafuta ili nimuombe msamaha".alijiwazia suma ila wakati anawaza sana mara simu yake ikawa inaita akaichukua ile kutazama kwenye kioo akajikuta anaachia tabasamu pana usoni...... ENDELEA.....
Alijikuta anatabasamu na kukenua meno yote thelathini na mbili yakawa nje. Kiukweli alijisikia furaha ya ajabu alipoona kwenye kioo jina la mpigaji. Haraka haraka akapokea. "hello mshikaji wangu vicent inakuwaje? ".aliongea kwa uchangamfu suma hata huku akionyesha kutoamini kama alipigiwa na mtu huyo. "poa tu niaje mzee baba?".aliongea kwa uchangamfu vicent uwezo amini kama walikwaruzana. "niko poa mwanangu sema nimefurahi kwakunipigia nilikuwa sina amani kwakweli, nisamehe sana wangu".aliongea suma huku akionyesha kujutia alicho kifanya. "aaaah potezea mshikaji wangu ndo maana nimekutafuta ili kila kitu kiwe sawa usiwaze mchizi wangu".aliongea vicent kumtoa wasiwasi mwenzie basi walipiga stori za hapa na pale tofauti zikawekwa pembeni mambo yakawa sawa. 

***********
Ilikuwa imepita wiki, na hiyo ilikuwa weekend mawasiliano kati ya niram na vicent yalikuwa yamepamba moto. Kwakweli walikuwa na urafiki mkubwa na wenye ukaribu zaidi. 
Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Ijumaa vicent alikuwa amesharudi kutoka shuleni. Na walibakiza siku chache ya kufanya mtihani wa kuhitimu kidato cha sita. Vicent alikuwa chumbani kwake kwenye kitanda akiwa amejipumzisha akitafakari mawili matatu. Ila ghafla akachukua simu yake akabonyeza namba za niram nakuweka sikioni. Simu haikuita sana ikapokelewa. "mambo kipenzi "aliongea niram mara baada ya kupokea simu yake. "poa mzima wewe? ".akijibu vicent nakuuliza swali. "mi mzima sijui wewe wangu?".aliuliza niram. "niko poa nimekumisi tu wangu".aliongea vicent kwa utaratibu. "ooh nimekumisi pia mpendwa ".alijibu niram kwa upole zaidi. Kikapita kimya kifupi kama sekunde nne hivi alafu vicent akaongea. " niram naomba nikuombe kitu tafadhali".aliongea vicent kwa sauti ya upole na busara zaidi huku akisikilizia jibu upande wapili. "kitu gani hicho vicent?".aliuliza niram. "aaah!! Nilikuwa naomba kesho tuonane nina mazungumzo na wewe kama huijali? ".aliongea vicent kwa kubembeleza huku akiwa na mashaka na jibu ambalo atalitoa Niram. "Oooh!! Sawa kwa kesho ntakuwa na nafasi maana Jumapili nna safari, je tutakutania wapi labda? ".aliuluza niram ili ajue na kujua atapanga ratiba zake vipi. "aaah!! Nilipenda tuonane beach hata hapo kunduchi beach itakuwa poa".aliongea vicent na kumfanya niram ajifikirie kwa muda. "Ook siyo mbaya itakuwa muda gani?".aliuliza tena niram. "kama saa tisa jioni kama hutojali" " oooh sawa ntafanya hivyo usijali".alijibu niram vicent alifurahi sana yani kupita maelezo. Wakahama pale huku vicent akiwa aamini kwa niram kumkubalia ombi lake. Hakiwa katika hali ya furaha mara ikaingia msg kwenye simu yake. Alikuwa ni Vanessa sasa sijui ni kwanini alibadilika hafla, vicent maana furaha yote iliyeyuka na kukunja sura ni kweli hakumpenda Vanessa hata kidogo. Japo Vanessa alikuwa msichana mrembo sana japo hakumfikia niram hata robo .baada tu ya kukaa kimya sana bila ya kujibu msg kwenye simu yake akaamua afungue asome. " baby mbona kimya sana mwenzio nimekumisi".ilisomeka msg ya vanessa. "hamna wangu si unajua imebaki siku kadhaa mitihani ianze ndo maana nakuwa bize".alijibu msg ile vicent "oooh ok Sawa jisomee mpenzi naimani mitihani ikiisha kila kitu kitakuwa sawa".alituma tena msg vanessa. "kabisa wangu kila kitu kitakuwa kiko vizuri ".alijibu vicent ndo ukawa mwisho wa chatting maana vicent akapitiwa na usingizi, mpaka alipo kuja kushtuka saa tatu za usiku mama yake alipokuja kumwamsha akale chakula*******
Vanessa japo na yeye alikuwa ni mtu anayependa kusoma. Lakini alikuwa na mashaka makubwa na mambo anayoyaona kwa vicent.kiukweli alianza kuingiwa na mashaka Akujua ni kwanini anawaza kuwa kuna kitu hakipo sawa. Aliona mabadiliko makubwa kwa vicent,alikuwa amebadilika kwa kiasi fulani na hakuelewa ni nini sababu ya yote hayo. "mmmh!! Mbona kama kuna kitu kinaendelea, na mimi sikijui inabidi nifatilie nijue ni nini kilicho mbadilisha vicent wangu".alijisemea kimoyomoyo huku anavuta shuka ili alale. Japo usingizi ulichelewa kuja ila baada ya muda alilala. 

***********
Ilikuwa ni siku ya Jumamosi tulivu, kijua hakikuwa kikali sana hakika kulikuwa na mwanga wa kuvutia siku hiyo. ambayo ilifanya siku izidi kung'aa. Niram alikuwa sebuleni na mama yake,wakikaa sehemu ya kulia chakula wakijinywea chai yao nzito ya maziwa na mikate ya ufuta. Baada ya kimya cha muda, niram aliamua kukatisha ukimya huo. "mama nilikuwa nakuomba ruhusa leo saa tisa nataka kutoka ". "mmh!! Mbona jioni sana itakuwa, unaenda wapi mida hiyo?". Aliuliza mama yake huku kipande cha mkate kikiwa mkononi akisubiria jibu kutoka kwa mwanae . "rafiki yangu anauguliwa na mjomba wake hivyo naenda kumuona ntawahi kurudi".alijibu niram huku akisikilizia jibu kwa mama yake amtamjibu nini. "rafiki yako gani?". Akiuliza mama yake. "anaitwa shira nilishawahi kuja nae hapa".aliongea tena niram. Mama niram kumuangalia Kwa umakini mwanae .maana hakutaka kuona mwanae anapotea au kuharibikiwa ndo maana alikuwa makini sana na binti yake. "sawa nenda ukamuone mgonjwa ila uwahi kurudi mapema ".aliongea mama yake niram."asante mama nashukuru nakuahidi ntawahi kurudi mama yangu ".alijibu niram kwa furaha ,basi walikunywa chai wakamaliza niram akaelekea jikoni kuandaa chakula cha mchana. Siku za weekend niram hupendelea kumsaidia sana dada wa kazi na ndiyo maana msichana alimpenda sana niram. 

**********
Ilishahitimu saa tisa na robo jioni. Vicent alikuwa ameshafikia, alikaa kwenye viti vilivyokuwa mahali hapo alichagua sehemu ambayo niram hata akija atamwona kirahisi. Basi aikupita muda sana vicent akiwa anakunywa juice taratibu huku akivuta muda ili niram aweze kuja ghafla mbele yake alimuona niram akiwa anakuja.moyo ukampiga paaaaah!! Kwa kweli niram alipendeza sana kwa jinsi alivyo vaa. Alikuwa amepigilia jinzi ya bluu iliyopauka, tishet ya pinki iliyo mkaa vizuri kwenye mwili wake na ilikuwa imeandikwa (i can't leave you) ikiwa na maana kuwa siwezi kukuacha.chini alivalia visimpo vya pinki vyenye ufito mweupe, na kichwani alizimwaga nywele zake zilizofika hadi mgongoni, na mawani meusi yakizidi kuupambisha uzuri wake. Siyo vicent tu aliye shangaa, bali wanaume wote hata wanawake macho yaliwatoka kwa jinsi Mungu alivyofanya kazi yake nzuri ya uumbaji kwa binti huyu. Basi niram alitembea taratibu mpaka alipokuwa vicent maana alimuona huku tabasamu usoni mwake lililomfanya kuwa mzuriii maradufu. Niram nae alishtuka japo aliuficha mshtuko wake maana vicent alikuwa kapendeza vibaya kwa tishet yake nyeupe alioivaa na pensi nyeusi na raba kali nyeupeee, huku mkononi akivalia saa kali ya silver. Wasichana macho yote yalikuwa kwa vicent,wavulana macho yote kwa niram kwakweli walipendeza sana na walivutia. Niram alivuta kiti akakaa mara akaja muhudumu akaagiza maji. "mambo vicent sorry kwa kukuweka sana".aliongea niram."aah!!usijali karibu sana".aliongea vicent huku akionyesha kuwa akujiamini kabisa kutokana na mtoto mzuri kuwa mbele yake tena mzuri kama malaika. "asante my" .alijibu niram huku ameachia tabasamu pana lililomfanya vicent azidi kupagawa. "mbona ujaagiza chakula vipi umeshiba".aliongea tena vicent ."nipo full kipenzi".alijibu niram.kikafata ukimya wa hali ya juu, huku kila mmoja akinywa taratibu kinywaji chake. Ila vicent akakatisha ukimya na kuanzisha maongezi. "niram mimi nimekuita kuna kitu nataka nikuambie ila utanisamehe sana kama ntakukwaza".alianza kuongea vicent kwa sauti ya taratibu na ya upole.
Niram alimuangalia kisha akaongea ."sawa nakusikiliza rafiki yangu ".paka pita ukimya kidogo na vicent akaanza kuongea japo alikosa ujasiri ila akajikakamua na kuanza kuongea. "kiukweli niram tangu siku ya kwanza nimekuona sijawahi kuacha kukupenda, umenikaa sana moyoni kiukweli nakupenda sana na sijui niseme nini ila umenifanya nijue nini maana ya kupenda tafadhali naomba uwe nami".aliongea vicent kwa huruma na kwa kubembeleza hakika ungemuona ungeamuonea huruma. Niram sura yake ikawa ya kawaida hata lile tabasamu likaporomoka na akawa amekunja uso gafla. "vicent mimi nilikuwa nakuchukulia kama rafiki au ndugu wa karibu, leo unasema hivyo mbona sielewi, sikia nikaambie mimi kuwa nawewe ni ndoto naomba huu ndo uwe mwisho wa ukaribu wetu kwaheri".aliongea niram huku ananyanyuka na kuondoka. "niram".alijaribu kuita vicent ila hakujibiwa. Niram alikazana mpaka alipofika kwenye gari lake akapanda gari akawaasha na kuondoka. Kwakweli vicent alichoka mtoto wa kiume alitokwa na chozi la maumivu hakutegema, hakuamini kama yametokea yale. Alichukua lesso akafuta machozi, alisimama na kuanza kuondoka ila ghafla....... Itaendelea.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.