
TANGAZO LA KAZI
Wananchi Wote,
TANZANIA BARA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo anawatangazia wanachi
nafasi za kazi kama ifuatavyo:-
KATIBU MAHSUSI III (nafasi moja)
Mwombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-- Awe amehitimu na kufaulu Elimu ya kidato cha nne.
- Awe amehudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu.
- Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Masharti ya Kazi:-
- Kazi hii ni ya masharti ya kudumu na malipo ya uzeeni
- Kazi hii ina ngazi ya mshahara TGS B kwa viwango vya Serikali.
WASAIDIZI WA HESABU (nafasi 2)
Mwombaji anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-- Awe amehitimu kidato cha nne
- Awe na Cheti cha ATEC level II au ‘’Foundation Level’’ kinachotolewa na NBAA au awe na Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
Simu Na.: 028 2225003
Fax Na.: 028 2225216
E-mail: ded@biharamulodc.go.tz
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P. 70
BIHARAMULO
HALMASHAURI YA WILAYA YA BIHARAMULO
03/07/2019
Masharti ya Kazi:-
- Kazi hii ni ya mkataba wa miaka miwili na mkataba huu waweza kuuhishwa
- Kazi hii ina ngazi ya mshahara TGS B kwa viwango vya Serikali.
MASHARTI YA JUMLA.
Mwombaji anatakiwa kuambatisha:-- Nakala za vyeti vya mafunzo
- Maelezo binafsi (Curriculum Vitae)
- Picha ndogo za rangi mbili (2) za mwombaji za hivi karibuni.
- Cheti cha kuzaliwa.
N.B. Maombi yote yatumwe kupitia posta kwa anuani ya Mkurugenzi Mtendaji
waWilaya S.L.P 70, Biharamulo.Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17/7/2019 saa 9:30 alasiriWende I. Ng’ahala
MKURUGENZI MTENDAJI (W)
BIHARAMULO
[/lock]
[/lock]