Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA TISA (09)

SAFARI YA KUZIMU
NA ZUBERI MARUMA
09
Whatsupp: 0767433106
Walikuja kutokea nyumbani ambapo bi Seli alimrudishia kijana yule roho yake aliyoiweka ndani ya chupa akamnywesha dawa Kali ya kumzuzua,baada ya hapo akamfunga kamba akisubiria mida ya kafara ifike ili amtoe!
Chris alikuwa ni Kama mbuzi aliyosubiria muda wake achinjwe!....
Na masaa yakazidi kukatika hatimaye muda ule wa kutoa sadaka ukawadia!....
Ambako kama ilivyokuwa kwa mwanaye bi Seli alimsogea akiwa na kisu chake kile na kumchuna ngozi ya kichwa mpaka akaukuta ubongo aloula yeye na viongozi wenzake kisha damu ilokuwepo maeneo Yale akaimiminia katika kikombe na kwenda kuinyunyuzia katika mvule ule!
Kwa lengo la kutoa sadaka kwa waruvaa,baada hapo akawapa ishara kundi lile la wachawi walounyanyua juu juu mwili ule!
Wakafika katika kichaka kimoja wakaushusha ule mwili wakawa wameuzunguka vile vile wakashikana mikono! na kuanza sala zao.
walipoitimisha wakajiteua mtu mmoja kazi ya kuucharanga charanga ule mwili! wakakata mapande ya nyama yalozungushwa katika mafurushi ya vitambaa vyeusi.,kwa kuwa pale apakuwa na moto nyama kila mmoja angeenda kupika kwake kwa aloitaji na wengine walikula ile ile mbichi.....
Sasa kilichobakia ni kimoja tu!
Vita vya kupambana na malkia wao Irene
***
Ilikuwa ni usiku wa manane!,kila mmoja alikuwa katika usingizi mzito katika chumba kile,
Ndani walikwepo wasichana watatu Irine akiwemo mmoja wapo
Wakiwa wamelala ghafla IRINE akafumbua macho yake,baada ya kuskia kama jina lake likiitwaa ,alippfumbua tu akashtuka kuskia mlango ukigongwa kwa nguvu...
"IRENEEE! IRENEEE! IRENE FUNGUA MWANANGU!"
ilikuwa ni sauti ya mama yake Irine alizidi kutetemeka!..
akakaa kitako kitandani pale ghafla mama yake akatokea katikati ya chumba akiwa kashika kibuyu kilichozungushiwa shanga nyeusi na nyekundu,
Kibuyu kile kile alichokabidhiwa akakikataa ,mama yake alikuwa kajifunga kaniki nyeusi usoni akiwa kajichora chora
irine alitingisha kichwa ishara ya kukataa wito ule...
mama yake akatabasamu ghafla bila idhini yake alishangaa mwili wake ukianza kunyanyuka wenyewe!
"nifateee mwanangu!...."
mama ake akamwambia huku akigeuka nyuma irene akawa anamfata wakafika mpaka katika kingo,pembe ya chumba wote pamoja wakatoweka....
Walikuja kutokea katikati ya pori katika mti mbuyu ule mkubwa watu walokuwa maeneo yale wote walivaa nguo nyeusi na kucheza kichawi! IRINE akuelewa kitu alibaki akishangaa huku akitetemeka....
mama yake alimshika mkono...
huku naye a lichens kwa bashasha, kabla alokuwa katikati yao mbibi alozeeka mwenye macho ya njano,ngozi yenye mikunjo mikunjo kuonesha mkono juu ngoma zile zisizo onekana zinanyamaza.
"Kinzungu uvinza nzae" ( udumu utawala wa kizungu)
"Nzaeeeeeee" ( udumuuuuuuuu)
"Kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeeeeeee"
"Ahsanteni wana kinzungu kwa kuwa pamoja tena katika usiku huu,usiku huu wa Leo ukiwa ni usiku mtakatifu kwa kuwa bi Seli kafanikiwa kutuletea malkia wetu kirahisi tu....
yule mama alitamka,baada ya kimya kutawala maeneo yale
Wachawi wote wakashangilia
"seleeeeeeeeh"
Bi Mwadawa akaendelea "lakini pamoja ya yote mkuu mzimu wa mizimu Waruvaa kakasirika! ajali amsababishi,kafara amtohi,ugumba wanawake amuwapi,amlogi kama mwazo kwanini?"
Wachawi wote wakabaki (kimya!)
Bi mwadawa akaendelea "Naitaji kazi!,na siku zijazo kuna safari ya kwenda kuzimu kuongeza mafunzo kwa ambao watakuwa ni wachawi hodari kati yetu ni juu yetu kufanya kazi kwa bidii
Wachawi wakashangilia baada ya mkuu wao kusema vile...mkuu wao akawaonesha usinga ishara ya kuwatuliza! wakatulia akaendelea!
"Sasa ningependa kumkaribisha bi Selina atutambulishie mgeni"
(bi Selina akamshika mkono irine mpaka katikati ya duara! palipokuwa na mkusanyiko wa watu)
:"Kinzungu nzinga nzaeeeeee!"
Akatamka kwa ukali!......
"Nzaeeeeee!" Wachawi wote wakaitika bi Seli akarudia.....
"kinzungu nzinga nzaeeeeee"
"Nzaeeeeee"
Taratibu bi Seli akakisogelea kile kibuyu ambacho Mara nyingi ujaribu kumpa mwanaye bila mafanikio na kukinyanyua wakati huu kilikuwa kinafoka moshi na kumwelekezea Irene angekipokea tu ingekuwa na maana kakubali agano
Naye bila kujielewa maskin Irene akanyoosha mkono tayari kukipokea!...pasina kujua ndo anaingia rasmi katika utawala wa kishetani.......
Je Nini kitaendelea baada ya Irene kupokea kibuyu?!
TUONANE KESHO KWA MWENDELEZO

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.