Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SAFARI YA KUZIMU SEHEMU YA SABA (07)

SAFARI YA KUZIMU
NA ZUBERI MARUMA
07
Whatsupp: 0767433106
'Ndo maana napendaga kuwa na tandboy mambo kama haya huwa yanapungua'
Akawaza akijaribu kuwasha gari ila ghafla akahisi anaguswa began,akageuka kwa woga!
Mwili ulimsisimka kwa kile alichokiona,akaanza kutetemeka akataka kusema kitu mdomo ukawa mzito!,
'Huu sasa ndo mwisho wangu'
Wazo lile likapita katika kichwa chake akizidi kutazama kile kilichomuibukia mule ndani ya gari!....
Macho yakamtoka Pima,akashindwa Kuamini kile akitazamapo,pembeni yake aliketi kiumbe ambacho kilikuwa na umbo la kutisha!,
Usoni alijaliwa tobo moja upande wa kushoto ambalo ndilo lililo kuwa kama jicho lakini akuliona jicho zaidi ya tobo lile na upande wa kulia palikuwa flati
Chini ya jicho lile alikuwa na pua na chini ya pua alikuwa na mdomo ulobeba meno mawili yalochongoka
Ukweli kiumbe kile kilitisha, alijaliwa mkono ulobeba kucha ndefu!,mwili wake ulioza na kutoa midamu pamoja na kutembelewa na mafinyofinyo!
Dereva yule anataka kujaribu kupiga kelele akashindwa,sauti inakataa kutoka kiumbe kile kikaupeleka mdomo wake shingoni , na kumng'ata akamnyonya damu na alipoakikisha dereva yule katokwa na uhai akamchoma kifuani kwa kucha zake kubwa na kuutoa mkono ule ukiwa ukeshika pande la nyama akalitupia mdomoni!
"Atakaye kuingilia mipango yangu hii ndo zawadi stahiki himpasayo"
Kiumbe kile kikasema taratibu na kupotea akatokea nje ya gari lile akalisukuma kusudi lionekane limepata ajali naye akatoweka akiacha kicheko kikali nyuma yake
****
Mwangaza wa asubuhi ulianza kummulika machoni jua lile lenye vitamin d lilimpiga japo kwa shida kutokana na kuzuiwa na miti mingi!
usingeamini kama usiku wake kulikuwa na mvua kubwa ilonyesha kulipambazuka vizuri! japo tope lilisanifu uwepo wa mvua muda mchache ulopita!
Taratibu IRINE akafumbua macho yake! akapokelewa na maumivu makali katika sehemu zake za siri ilomlazimu kupeleka mkono maeneo hayo!
akakutana na damu iloganga akukuwa na kizuizi chochote! kumbukumbu ya yaliyotokea yakamrudia katika kichwa chake! uchungu ukamkaba kooni,kilio kikafatia!
Kumkufuru MUNGU kukaendelea!
akajiinua na kuchukua nguo zake zilizochanwa na kutupwa akazivaa kwa dhumuni la kujistiri...
Bado aliendelea kulia umbo lake changa dogo bado lilionekana waziwazi mapaja yake makubwa yalokuwa kitamanio kwa mwanaume yoyote rijali ambaye angepata kuyaona matiti yake madogo yalimzidishia uzuri maradufu....
kwa kujivuta akaanza kusogea barabarani kwa lengo la kuomba msaada kwa msaada wowote utakaojitokeza.
***
MR Z FILM PRODUCTION kikundi cha kisanii kinachoongozwa na msanii ZUBERI MUSA wakiwa wametoka kushout movie yao katika pori ilo wakiwa katika gari aina ya costa ndani shamrashamra ziliendelea utani mwingi! ghafla dereva akapiga breki na kusimamisha gari,wote macho waliyakaza mbele kumtazama Dada yuke alokuwa akiomba msaada
mjadala mzito ukazuka baina yao
Baadhi ya wasanii wakidai yule ni jini kutokana na jinsi alivyo!
"binadamu gani atakuwa katikati ya pori ili na nguo izo MASOUD tuondokeni tusije tukaingia katika balaha"
BONGE aliongea mmoja wapo wa wasanii akimuhimiza dereva aliondoe gari!
"no ni binadamu yule tukamsaidieni!"
Msichana MERRY naye alitoa hoja yake muda wote ZUBER kiongozi ( director) wao akusema kitu akashuka na kwa tahadhari akasogea eneo ambalo IRINE alikwepo!
"wewe ni nani? na unafanyeje katika msitu huu!"
"naitwa IRINE nsaidie kaka yangu mi natoka kijiji cha jirani nlikuwa naenda mjini nkapata lift kwenye fuso huyo alonipa lifti tulipofika hapa....akan badilikia"
irine akashindwa kuendelea kilio kikamkaba
"kwa hiyo mjini unaenda kuishi kwa nani?"
"sijui sina ndugu naenda kutafuta kazi"
"unaweza kuigiza?"
"nini? kuigza nini"
"ok embu ngoja"
"TAYANA! TAYANA! MERY" (Akaita kwa nguvu) wakashuka wanawake wawili wakamsitiri mwenzao wakaingia naye kwenye gari SAFARI IKAENDELEA
***
ZUBERI MUSA alikuwa ni msanii mzuri na maarufu ukanda ule wa Ganja wilaya ya Rununu akiwa bado ajaoa ndo kwaza alikuwa kaamia kwenye nyumba yake mpya aloijenga na kuishi na wasanii wake walokuja gonja kwa ajili ya sanaa
waliingiza gari ndani ya nyumba ilofunguliwa na mlinzi,ilikuwa ni nyumba kubwa ambayo hata IRINE mwenyewe aliishangaa
"Vipi kaka ZUBERI unaishi kwenye nyumba hii peke yako?"
"no naishi na baadhi ya wasanii wenzangu wawili walotoka mikoani MERY na JACK! utashirikiana nao na mtafanya mazoezi pamoja ya sanaa mpaka utakuwa mzoefu wewe ni mzuri IRINE utakuwa star mapema sana."
aliongea ZUBER wakati wakiwa wamekaa sebuleni,zuber akamwita jack na kumkabidh IRINE
"mwenzenu huyu mpeni ushirikiano..."
"sawa dairekta" watoto wale wa kike wakaitika na kuondoka na irine
***
KATIKATI YA USIKU
Katika mkusanyiko wa watu walovaa kiasili katika kikundi kile cha Kinzungu chini ya mbuyu ule bi Selina na wenzake walikuwa wakicheza kama kawaida yao kichawi!
"Kinzungu uvinza nzae" ( hudumu utawala wa kizungu)
"Nzaeeeeeee" (hudumuuuuuuuu)
"Kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeeeeeee"
"Ahsanteni wana kinzungu sasa ningependa kuwajulisha jambo uongozi wa wana kinzungu umesikitishwa na ulichofanyiwa na malkia ambaye kama si nusra za Waruvaa tungeshamla siku nyingi nyama! ila lazima tumfundishe kwamba hawezi kutukimbia sisi abadani kinzungu uvinza nzaeeeeee"
Kundi lote la wachawi wakaitikia
"nzaeeeeee"
ngoma ikaendelea kupigwa huku wachawi wakicheza kabla awajastopishwa tena na bi Selina ambaye kwa hapo alikuwa ni mkubwa ukiongozi kuliko hata bi Chau na bi Mwadawa
"Kinzungu uvinza nzae"
"Nzaeeeeeee"
"Kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeeeeeee"
"Ahsanteni wana kinzungu kwa kuwa nami katika majonzi haya makuu kama alivyosema kitwana wetu bi Mwadawa tumeingia katika vita na malkia ya kuakikisha anakuwa katika himaya hii nadhani nafasi ya kupata malkia katika himaya yetu si kazi nyepesi na yapaswa tutumie nguvu zetu hasa
Irene ni mwanangu namjua fika yupo sana kiimani nalazima tuipindue Imani yake kwanza ili tufanikishe kazi hii narudia tena wana kinzungu ili tupate heshima katika himaya yetu ya kuwa na malkia wa wachawi wote ulimwenguni ni lazima Irene akubali kushirikiana nasi tutumie nguvu zetu zote ushirikiano tufanikishe ile kwa sasa kakimbilia mjini tutamfata huko huko tuyafanye maisha yake yawe ya tabu mateso ,tumjaze mikosi misuko suko mpaka akubali kurudi huku kwao na kuungana nasi kinzungu uvinza nzaeeeeee"
"Nzaeeeeee"
"Kingine wana Kinzungu!, ili kazi iwe rahisi zaidi ni lazima tutoe sadaka!
"Mmmh!....."
Miguno ikatawala,...
Wengi walishtuka pasina kujua ni sadaka gani ilotajwa neno sadaka walijua ni damu na nyama ya binadamu je ni yupi sasa?!
Yupi angekubali kutoa mtoto wake kipindi ambacho si chake!
"Ha haaaa haaaaaa haaaaaaaaa na itakuwa hivyo lazima tutoe sadaka!"
Kicheko kikasikika na bi Seli akazidi kusisitiza!....
Wote wakakaa mkao wa kula kumsikiliza ni sadaka ipi ingetajwa....
"Basi bi Seli akaendelea.......
Je ni sadaka gani itatajwa
Watafanikiwa kumrejesha Irene katika him

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.