SAFARI
SEHEMU 12
whatsApp 0655585220
Pindi alivyokuwa akiwaza hayo kijana YOROBI alijitoa ufahamu na kuanza kuikoki siraha yake na kuirudisha tena sehemu za kiuno chake, kiukweli wenzake hawakujuwa kama alitaka kufanya jambo ambalo halikupaswa, hata kufanya kwa mda huo, basi nae aliendelea kumkazia macho NGUVA huyo, ambae bado aliendelae kupambana na PAPA, huku matazamio yake yalikuwa ni kumpoteza kabisaaa NGUVA huyo. wakatihuo akiwa hajuwi hili wale NGUVA huyo aliendelea kusafisha bahari, huku akiwatembezea visu wale PAPA, basi alijitaidi sana kufanya hivyo huku malengo yake ni yake ni kuokoa jahazi la watu hao, nakuwaelekeza njia yakupita, kwani hakupenda kuona damu ya mtu ikimwagika maeneo hayo, alipo maliza na aligeuka kwenye jahazi walilokuwemo binti pamoja na kijana YOROBI, huku akitaka kuwaelekez njia yakupita, na kuwatakia safari njema.kwani kazi ilikuwa imekwisha aliyokuwa akiifanya, kuangamiza wote waliokuwemo eneo la bahari hiyo. PAPA wote walipotea kwa kichapo alicho wapa NGUVA huyo huku wengine wakikimbilia mbali, ili wasije kulika kwa kitu chochote, nao walitimkia mbali sana.
Ndipo kijana YOROBI kuona nguva akiwatazama, uoga ukamshika akijuwa kuwa zamu yao imewadia, hakutaka hata kupoteza mda, nae alitoa mguu wa kuku (bastora) nakuielekeza alipo binti NGUVA, ile kuona viele binti BERALITA, kitendo cha YOROBI kumuoneshea NGUVA huyo aliye angaikia uhai wao walipokuwa ndani ya maji, basi alitoka speed mahari alipokuwepo na kumfata alipokuwepo kijana YOROBI, kuzuia kitendo hicho, lakini mbio zake hazikuzuia kile alicho kusudia YOROBI, kwani alipokuwa akikimbia binti huyo na alipofika tu! alikuta kaisha fyatua risasi, ambayo ilienda moja kwa moja mpaka kwenye bega la NGUVA huyo, huku nae NGUVA alishangaa sana kwa kile kitendo alichofanya kijana YOROBI, kiukweli hakikumpendeza, alishikwa na gasira kali sana, akajiuliza "nawafanyia haya yote kwaajili yao, bado wana nitendea haya"
Basi binti BERALITA alipoona hivyo, alimsukuma kijana YOROBI pembeni na kumtazama sana NGUVA, kama ame dhurika kiasi gani, alimwona akipiga kelele kuashiria risasi ile imempata barabara. Binti BERARITA alimlaumu sana kijana YOROBI, kwa kitendo hicho huku kijana YOROBI, akijiona kafanya jambo la kishujaha, ndipo alipokaa chini akimsikiliza binti BERALITA akifoka sana juu ya tukio, yeye hakumjari zaidi aliwaimiza vijana wake wazidi ku piga makasia nakuinuwa tanga ili jahazi liongeze mwendo, haya sasa ni atuwa gani atachukuwa Binti Nguva? isome kisha nijulishe ili nikujuze kuamuzi alio chukuwa Binti Nguva, hapa hapa kwa mdau wako Ahmad Mdowe