SIMULIZI:-CHOZI LISILOFUTIKA
#PART__________01
MTUNZI; @dayo_de_Amos
Place:- University of dar es salaam,Tz
Cont;-0752677424/0625614133
Naitwa Nasra nina miaka ishirini na tatu, ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watano ,katika familia yetu tulizaliwa watano ambapo nilikuwa na kaka zangu mapacha na wadogo zangu wawili mmoja wa kiume na mwingine wakike, kaka zangu walifaliki mara baada ya ajali ya ndege iliyotokea miaka kumi na sita iliyopita wakati wakielekea nchini Marekani, ajali hiyo ilitokea katika nchi ya Nigeria ambapo inasemekana kuwa mnamo majira ya saa tisa nchini Nigeria kulikuwa na mvua kubwa iliyoambatana na radi kali hivyo wakati ndege ikijiandaa kutua ndipo itirafu ilitokea ya kupigwa na radi abiria wote walikufa hapakuwa na majeruhi sababu ndege ililipuka moto baada ya kujibamiza chini, Wadogo zangu wanaonifuata mmoja yule wa kiume alizaliwa akiwa kiwete, na mwingine alizaliwa akiwa mlemavu wa ngozi yaani albino. Wazazi wangu kabla ya kuachana waliishi kwa upendo mkubwa lakini baada ya baba yangu kupata ukilema akiwa na miaka arobaini na tano ,ndipo mama alipoamua kumkimbia baba,Ilinibidi nichukue majukumu ya kuwatunza wadogo zangu na baba yangu, niliishi nao huku nikiendelea na masomo yangu ,baada ya kumaliza darasa la saba nilipata mda wa kutosha kuhakikisha wadogo zangu pamoja na baba yangu nawalea katika malezi bora, Nakumbuka ilikuwa tarehe kumi mwezi wa saba ambapo baba yetu kipenzi alipotutoka duniani siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwetu hasa kwa wadogo zangu kwani kila Mara waliniuliza "Dada baba bado amelela Leo haamki?" moja ya maswali yaliyonipa ugumu katika kuyajibu.Matoke ya mtihani yalitoka nikiwa nimefaulu vizuri, nilifurahi sababu niliona ndoto zangu zimeanza kutimia sikuwahi kuwaza iwapo maisha yatakuja kuwa magumu kwani niliamini kabsa iwapo ntakuwa na juhudi katika masomo nitaishi maisha rahisi sana, Ilibidi nimpe mama yangu hizi taarifa lakini hakuzipokea kama nilivyotarajia badala yake alinijibu hana pesa za kunisomesha ,wakati baba alituachia kila Mali zilizokuwapo hivyo sikuchukulia uzito sana maneno ya mama yangu, Baada ya kuona maisha ninayoishi sio mtoto bali ni mama pia ni baba nilijipa majukumu ya kuhakikisha Mali zilizo achwa na baba zinakuwa miliki yetu Mimi na wadogo zangu ,niliamua kufuatilia hati miliki ya mali zote bahati nzuri nilipata mdhamini wa kufuatilia hiyo hati mahakamani,kesi hiyo ilichukua takribani miezi sita kutokana baadhi ya vielelezo vingine sikuwa navyo.Nilipofika kidato cha pili niliamua kuuza baadhi ya Mali nikiwemo gari bovu lililokuwepo hapo nyumbani, wadogo zangu kheri na Musa wao walikuwa bado wananitegemea pamoja na kuwa na mfanya kazi lakini bado changamoto nyingi zilikuwa zinanikumba ikiwemo walimu kunitaka kimapenzi, hii ilitokana na umbo kubwa nililokuwa nalo lakini bado nilikuwa sijua kama kuna mapenzi katika dunia, nakumbuka siku moja nikiwa kidato cha tatu wakati narudi nyumbani mida ya jioni nilishangaa yule wakili aliyenisaidia kudai Mali za marehemu baba yangu alikuwa ameleta wanunuzi wa nyumba na shemu yote iliyokuwa inazunguka maeneo , ilibidi nimuulize "Kaka ni kitu gani kinaendelea?" mbona sikuelewi? umeamua kunisaliti unataka tukaishi wapi wakati unaona hali ya wadogo zangu hawana uwezo wa kujitegemea " Nataka niwahamishe hapa muende kule karibu na soko" Thomas alizungumza lakini sikumuelewa kauli yake ilikuwa na maana gani"
Nasra:- kaka hizi mali ni zako au ni za wazazi wangu?
Thomas:- nimeamua tu sababu naona hapa hapafai na ukidhingatia hali ya wadogo zako mazingira hayaruhusu lakini wakiwa kule watapata baadhi ya mahitaji hata kama haupo.
"Kaka thomas hiyo sio sababu kama unataka kuuza nyumba ya wazazi wetu unajindanganya wewe huna undugu na sisi kunisaidia kudai mali hizi isiwe kigezo cha kutaka kutunyanyasa " nilizungumza kwa ujasili kabsa kiasi kwamba watu aliokuja nao walibaki wakinishangaa tu ,"Nimesema hii nyumba ni urithi wangu na wadogo zangu sasa unataka kuuza nikaishi wapi au kwa sababu wazazi wamefarik ndo umeona mwanya ! Niliondoka pale na kuelekea ndani niliwakuta wadogo zangu wakiniangalia kwa jicho la hudhuni, Musa yeye aliamua kuvunja ukimya "Dada mbona anko anataka kuuza hii nyumba ? Swali hili lilisababisha nikae kimya kidogo kisha nikajiribu kujibu " Musa bwana hapana hawezi kuuza anataka kuwatafutia mwalimu awe anakuja kuwafundisha"
Niliendelea kuwalea wadogo zangu katika mazingira magumu kidogo kwani sikuwa na uwezo wa kujigawa ,majukumu yalikuwa ni mengi wakati mwingine yalinifanya kutokwenda shuleni kwa baadhi ya siku katika masomo nilijitahidi sana lakini kutokana na majukumu ilifikia kipindi nikawa nashuka kimasomo na ndipo Mwalimu ATHUMAN alipochukulia udhaifu wangu kuniadhibu kila Mara alifanya hivyo kwa ajili ya kunikomoa kwani alisha nitaka kimapenzi nikamkataa .
"Yaani wewe mjinga kabsa nakuita unanifanyia kiburi ? Mwalimu Athuman alizungumza maneno hayo Mara baada ya mwalimu mkuu kupita karibu na pale nilipokuepo, " unatatizo gani wewe mtoto?kiburi ndo kinakufanya ufeli mitihani na sizani kama utafauli,"Mwalimu Athuman alimaliza kuongea, aliniruhusu kwenda darasani lakini moyoni nikuwa nimejawa na hasira, nilimchukia Mwalimu huyu kwani kila jambo nililifanya lilonekana baya kwake,
Ilifika mda sasa hela ya kumlipa mfanya kazi zikawa zinakosekana kutoka na maisha tuliyokuwa tukiishi tulikuwa tunategemea Mali zilizo achwa na baba na zingine kuchukuliwa na mama yetu, Ilibidi nimwachishe kwanza ili kunusulu pesa ambazo zilikuwapo kwa mda ule, ugumu uliokuwepo kwa wadogo zangu kuwa wanashinda njaa.niliwasihi wavumilie kwani mda huo nilikuwa kidato cha nne
"Jamani munivumilie sawa wadogo zangu?, jaribu kutumia chakula tutachokuwa tumebakiza," Shuleni mambo yaliendelea kuwa magumu kwani Mwalimu Athuman bado alizidi kunisumbua sana,
"Unajua nini MAGRETH yaani nakosa raha kabsa kila siku mimi ni wakupigwa kama punda kweli ? Ntaishije mimi " machozi yalianza kunidondoka kwa uchungu" hebu fikilia nyumbani mateso na shuleni pia jamani mungu nimemukosea nini lakini?"
MAGRETH "Nasra usilie kwani ni matatizo madogo tu haya usha jaribu kumweleza madam mwajuma?
" MAGRETH wewe unajua kabsa ,maadam mwajuma anashirikiana na sir ATHUMAN kunitesa kiasi ..........
MAGRETH;- usilie sasa jikaze
"Mateso yamenizidi sana nimejaribu kujizuia lakini kadri siku zinavyoenda ndo nayaona machungu ya dunia
[lock]
,,wakati maongezi yakiendelea Mara kengere iligonga kuashiria mda wa kurudi madarasani umefika, niliachana na MAGRETH amabaye alikuwa anasoma mkondo A na mimi nilikuwa C , nilikimbia kuelekea darasani lakini wakati nataka kuingia ,Mwalimu Athuman aliniona " Nasra njoo hapa "nilienda huku nikikimbia baada ya kufika .
" Piga magoti hapo "niliitikia wito huku Mwalimu akiangiza fimbo ," Nasra unamatatizo gani wewe kengere inagonga wewe unafanya mambo yako sio?"
"Mwalimu Nili....." Kimya sitaki kusikia kelele zako Mwalimu alidakia. Mara yule aliyeagizwa fimbo alikuwa ameshafika , bahati nzuri mkuu washule aliniona kisha akamuita Mwalimu Athuman, "Mwalimu nakuhitaji Mara moja ofisini " baada ya Mwalimu kuondoka niliona kama mungu amesikia kilio chagu nilinyanyuka na kuelekea darasani, nilimkuta madam mwajuma akiwa anafundisha "please Madame may get in? " nilibisha hodi, "toka unatupigia kelele ,hebu njoo kwanza, darasa munamuoana huyu!? .darasa liliitikia "ndioo madam" mbona umechelewa? Nimechelewa kwa sababu nilikuwa kwa mwalimu athumani
Mwalimu :- kufanya nini?
"Nilikuwa na adhabu.
Mwalimu:- unaona binti mpaka saizi hujitambui makubwa yaani wewe utafeli.Nilijitetea lakini mwishowe alinipa adhabu ya kufuta ubao mzima.
" Mwalimu athuman ,nimekuita hapa kwa sababu nimegundua kunajambo linaendelea kati yako na NASRA,na jambo hili limefikia pabaya sana tena sana, wewe ni Mwalimu kumwadhibu mtoto wa watu kiasi hicho nni maana yake?"
Mwalimu athuman. :-eeeeee... Mkuu bilashaka mtoto huyu amekuwa na kiburi sana,kwanza darasani hatulii, mitihani anafeli,kengere ikigonga anakuja mda anaotaka yeye, kwa hiyo nimechukua majukumu ya kiualimu zaidi kuhakikisha sheria za shule zinafuatwa"
"Mwalimu sizani kama hayo unayoyasema ni kweli, nimekuoana siku nyingi sana kama kunatatizo fimbo hazisaidii,pengine kunajambo linaendelea chini chini lakini nakusihi acha hiyo tabia kwanza huyu mtoto tushukuru mungu anajitahidi kuja shule ,majukumu aliyonayo ni mazito sana,narudia tena acha kabsa iyo tabia.
Mda wa kurudi nyumbani ulifika,nikiwa na marafiki zangu MAGRETH, Neema ,Sarah na zuhura tukiwa tunatembea njiani kwa pamoja huku stori zikiendelea,ghafla tulishitushwa na mlio wa kengere ya baiskeli wote tulikimbia kupisha njia,Alikuwa ni Mwalimu athumani mapigo ya moyo yalinienda kasi sana, baada ya kutupita alisimama mbele yetu,tulipo taka kumpita aliniita,ikabidi nimfuate alipokuwa amesimama,
" NASRA unajifanya mjanja sana!?""
"" Mwalimu me unanionea bure tu sinakosa lolote"
"" Anhaa huna kosa sasa utajua mi ni nani!?""Alipanda baiskeli yake akaendelea na safari, aliniacha huku wenzagu wakiniuliza alichonambia
MAGRETH:- nasra amekwambia je ?
"" Nisha zoea kama kuniua aniue tu sina jinsi lakini sio kumkubalia anachotaka"
ZUHURA:- mbona sielewi kwani kuna nini kati yako na huyu Mwalimu? maana kila Siku anakunyanyasa sana!
"Haya ni mambo ya kijinga sasa amekomaa kunitongoza Mimi wakati wanawake wengi wapo saizi yake, sasa mi nitampeleka wapi "?
Wotee walicheka hahahahahaha eeeeeh" tulindelea na safari ambapo tuliachana baada ya njia kutawanyika kila mmoja alienda nyumbani kwao, Baada ya kufika nyumbani niliwakuta wadogo zangu wakiwa wananisubilia huku wakilalamika wana njaaa,
Musa:- Dada ninanjaa sijala tangu Jana!"
"Pole sana baba ngoja nipike haraka mle sio" niliingia ndani kisha nikachukua mikaa nikaiweka kwenye jiko, baada ya kuliwasha niliendelea na kuchambua mboga nilizochukua gengeni.wadogo zangu wao waliendelea kuchezacheza pale ndani wakisubilia chakula, baada ya kumaliza kupika ,tulikula huku nyuso za wadogo zangu zikijawa na furaha,.
Siku zikazidi kusogea ambapo mtihani wa kumaliza kidato cha nne ulikuwa umekalibia sana! nilijitahidi kuweka mipango sawa ili angalau nipate maandalizi ya mazuri ya mtihani, changamoto za Mwalimu Athuman na madam mwajuma niliwaogopa sana kwani kila siku walikuwa wakinitukana hasa matusi yaliokuwa yakinachia kidonda moyoni.Hatimaye siku ya mtihani ikawadia ambapo mtihani wa kwanza ulikuwa civics, tuliufanya asubuhi, mchana tukafanya hesabu na mwisho tukamailizia na English, katika mtihani huu wa mwisho niliona kama nimetua mzigo mkubwa sana maishani mwangu kwani mateso na masimamngo ya Mwalimu athumani na mwajuma yalifikia kikomo, baada ya kumaliza mtihanil mkuu wa shule alihitisha mkutano wa wahitimu wote, ambapo takribani walimu wote walikuepo, mkuu wa shule alianza kuzungumza kwa kutupa mpole na baadaye alitoa mawaidha ya namna tutakavyoishi tukiwa uraiani, "" wanafunzi mmehitimu hapa si kwamba ngazi zenu za kimasomo zimeishia hapa, bali mnayo nafasi ya kuitumia elimu yenu mlioipata hapa kusaidia jamii zenu katika mambo mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, sasa mi nawatakia mkaishi vizuri na wazazi wenu ,labda nikaribishe kama huna Mwalimu yeyote anataka kutoa mawaiza kidogo juu yenu."
Alinyanyuka madam mwajuma .................
Usikose sehemu pili
[/lock]