SPHAGETTI BOLOGNESE
MAHITAJI YA KUPIKA SPHAGETTI BOLOGNESE:
.
1. Tambi mfuko mmoja
2. Nyama ya kusaga nusu kilo
3. Nyanya 4
4. Kitunguu swaumu 1
5. Kitunguu maji kikubwa 1
6. Njegere glass ndogo 1
7. Karoti 1 na Hoho 1
8. Chumvi kiasi
.
JINSI YA KUANDAA SPHAGETTI BOLOGNESE
- -Weka mafuta yachemke,kisha kaanga kitunguu swaumu kilichopondwa pamoja na kitunguu maji,hoho na karoti.
- -Weka nyama katika mchanganyo huo na ikaange hadi itakapobadilika rangi kuwa ya brown.
- -Weka tambi zilizochemshwa na njegere.
- -Koroga kisha ongeza nyanya(ni vizuri zikawa zimesagwa kuliko kukatwakatwa) kisha ongeza maji kidogo.
- -Funika acha ichemke,kisha weka chumvi.
- -tayar kwa kuliwa, inaweza kuliwa kama chakula cha wakati wowote,pamoja na kinywaji chochote. Enjoy