Kwa nini usumbuke kupote hela kununua JAM wakati huitaji pesa nyingi kuitengeneza! Hebu pata maujanja hapa!JINSI YA KUPIKA JAM YA NANASI
MAHITAJI
♦Nanasi kata vipandevipande
♦sukari nyeupe au yakawaida vikombe 2
♦ndimu vijiko 4
♦maji kikombe 1
1.Chemsha nanasi hadi likiwa laini lipondeponde
2.Tia sukari ktk sufuria na maji ukoroge mpaka iyeyuke
3.Iweke jikoni ichemke mpaka uone inanatanata ktk vidole tahadhari isiungue
4.Tia nanasi lako na maji ya ndimu changanya ,iwache ichemke kwa moto mdogo mdogo mpaka iwe nzito kama jam zengine kisha epua ,tayari kwa matumizi waweza kula na mkate,banzi nk.ENJOY! Je umeipenda?