Notification texts go here Contact Us Buy Now!

JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU SEHEMU YA 5

Estimated read time: 4 min
JINSI PAKA ALIVYOMALIZA FAMILIA YETU

      SEHEMU 5

        MWISHO

        WHATSAPP 0655585220

             ZANZIBAR

ILIPOISHIA:
Tuliishia pale pale paka akiwa amenitokea na wale viumbe wawili wenye maumbo ya kipaka na kutakiwa niingiliane nao kimwili, ingali mwenyewe hata mwanaume wa kawaida tu sitambui yukoje!!!
TUENDELEE SASA!!!
Sikuwa na la kufanya kabisa, zaidi ya kuomba mungu, nilikua naona kabisa huo ndiyo utakua mwisho wa maisha yangu, mwisho wa matumaini yangu, nilihisi kuliona kaburi mbele yangu, maana kwa maumbo waliyokua nayo wale paka watu ilikua ni kunibaka mpaka kufa!!
Wale paka wakaanza kunipapasa mwili wangu, nilikua sihisi chochote zaidi ya manyoya yao mengi yakianza kupita katika maungio yangu nyeti ya mwili.
Kwa niliyokua nayo sikuweza kupiga kelele wala kujigeuza, nilikua kama gogo la nyanya yani, linalosubiri mnunuzi sokoni. Oh!! Mola wangu naomba hali ile usimpe msomaji wa mkasa huu!!
Punde nikaanza kuhisi nafunuliwa gauni langu, paka mmojawapo akaanza kufungua zipu yake ili atoe soseji na aanze kunishughulikia.
Kabla hajafanya kitendo kile, mlango wa chumba nilichokuwemo ulifunguliwa, alikua si mwingine bali ni baba yangu. Alikua ameongozana na viongozi wa dini.
Ghafla!!! Wale paka na vile viumbe vingine vilipotea. Baba alikuja moja kwa moja na wale viongozi wa dini mpaka pale nilipokua nimelala.
Akiwa mwenye kukatwa kabisa na tamaa baba yangu, aliwaelezea baadhi ya mikasa iliyokumba familia yetu..
"..............Nahisi nimshirikishe mungu juu ya hili, natumaini atanisaidia". Baba alimalizia kuongea maneno hayo huku kijasho kikiwa kinamtiririka usoni mwake, mwili wake ukiwa umechoka kwa pilika za kuchosha zisizomuisha, nguo aliyovaa ilikua ni siku ya tatu hajabadili.
"... Usijali bwana Salisala haya yote kwa mungu ni mambo madogo sana, maana kwake hakuna linaloshindikana!!"
Wale viongozi wakaanza kufanya maombi, walifanya maombi kama dakika tano hivi, mara ikaanza kusikika sauti ya paka pale chumbani.
Nilihisi naisikia peke yangu kama nilivyozoea, lakini nilishangaa kumuona baba na yeye anaisikia sauti ile. Alikua si mwenye kutulia na kutafuta tafuta wapi inatokea.
"Vuuuuuuup!!!!"
Yule paka alitokea pale mbele yetu kimaajabu huku akijikunja kunja kuonesha yale maombi yanamuingia.
Baba alishtuka sana na nusu akimbie, wale viongozi wa dini hawakushughulika naye na badala yake waliendelea tu kuomba.
**
Sikutaka kuamini nilichokua nakiona mpenzi msomaji, yule paka alijigeuza na kuwa na sura ya dada wetu wa kazi (Dada mwajuma!!)
"Iiiiiinhh iiiiinhh naombeni msiniumize, nisameheni jamani!!! Nisameheni!!!".
..Mara akaanza kulia na kuomba msamaha.
Muda wote huo baba alikua ameduwaa tu na hatambui la kufanya, Wale viongozi wa dini wakaacha kuomba na kuanza kumuhoji dada Mwajuma aliyegeuka kutoka katika umbo la paka.
" Wewe ni nani na unatokea wapi??"...Walimuuliza
"Ni ni ni dada wetu wa kazi huyo!!", Baba alidakia na kuwajibu.
Kusikia vile wale viongozi walipigwa na butwaa kidogo kisha wakaendelea kumhoji.
" Kwa nini unafanya unyama wa kiasi hiki?"
Dada Mwajuma hakujibu chochote zaidi ya kuinamia na kuendelea kulia, huku akiwa amevaa kanga yashingo tu na nywele zikiwa timutimu!!!
"Sasa kama hutaki kusema, sisi tunaendelea kuomba ili uzidi kupata maumivu!!"
Wale viongozi walimtisha kidogo, ndipo aliponyamaza na kuinua uso wake juu, akaacha kulia na kuanza kuzungumza.
"Subirini nitasema!!!, Mimi ndiyo nilimuua Mama Naomi, mimi ndiye niliyemuua dada yake Mama Naomi na mimi ndiye ninayefanya mpaka Naomi anateseka kiasi hiko".
Baada ya kuongea maneno yale, hasira zilinishika nikanyanyua mkono na kutaka kuinuka.
Nilistaajabu sana kwa kweli, baada ya muda mrefu, nilijikuta naweza kunyanyuka pale nilipo kitandani. Baba alifurahi kwa kushangaa kisha akanikumbatia huku kilio cha uchungu kikimtoka.
Wale viongozi bado walikua naye yule mbaya wetu, wakaendelea kumuhoji...
" Kwa nini umefanya uchafu wote wa namna hii lakini? Huoni kama hutakua na msamaha mbele ya mungu wako aliyekuumba??"
Dada Mwajuma aliacha kulia kisha akaanza kucheka kwa nguvu...
"Hahahahahhhah!!!..
"Huruma?!! Huruma gani kwa mfano??, labda niwape historia kidogo!!!"
**
"Miezi michache iliyopita, ilikua ni usiku sana huyu baba huyu mnayemuona huyu!!( Alimnyooshea kidole baba), mkewe alikua ametoka na wanawe, nikiwa nimebaki mimi na yeye nyumbani kule tegeta, aliingia chumbani kwangu na kunibaka!!! Niliumia sana!! Zaidi ya sana yani!!!, nilimpigia simu bibi yangu nikamueleza yote!!..
.....Bibi akanipa nguvu na kunielekeza ya kufanya!!! Nilitaka niwamalize mmoja baada ya mwingine na familia yao yote iishe huku nikiwa nimejenga chuki kubwa sana baina yao. Halafu wewe unaongelea kuhusu HURUMA!!! Huruma ipi labda haswa??"
Kwa kweli maneno yale yalinikata maini, baba aliingiwa na aibu na kuinana tu chini huku machozi yakimtiririka. Hakuwa na la kufanya zaidi kuomba tu ya kukiri kosa na kuomba msamaha.
Nilimchukia sana Mwajuma, kwa kuhukumu familia yetu kwa kosa la baba lakini sikuwa na la kumfanya zaidi alifukuzwa tu nyumbani na kurudishwa kijijini kwao.
Kutokana na vifo vya utata vilivyokua vimetokea kabla, baada ya ushahidi tuliohitajika kuutoa polisi, ilibidi Mwajuma aende kutafutwa mpaka kijijini kwao ila HAWAKUWEZA KUMPATA KABISA!!!
Tumebaki kumuachia mungu, ndiye atakuja kuhukumu juu ya hili!!!!

MWISHO!!!!!

Ulikua nami mtunzi wako wa mkasa huu AHMAD MDOWE nami kwa simulizi yangu ijayo!!!
AHSANTENI SANAAAAAAAAAH!!!!!

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.