Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 25

Story ;SANGARE
BY ;Mogy shine
No.0621302436
///////////////////////

         SEHEMU 25
     TULIPO ISHIA JANA,Akacheka tena na kumwambia issa hebu njoo tuzichape ngumi sasa akili yangu imekumbuka maisha yangu ya nyuma

Issa aligeuka akamwangalia sangare kisha akamtizama minal ambae anashangilia peke yake anataja sangare ,sangare
Issa akajisemea moyoni sasa muda mwafaka wa kukumaliza wewe sangare ,akatizama saa zimesalia dakika mbili alinyanyua mguu akaupindisha akamfuata sangare kwa kasi ,sangare "akavuta hisia anakwapua mkoba wa mwanamke flani kisha akajibanza kwenye ukuta halafu anapiga sarakasi na kuruka ukuta
" iwakati sangare anavuta hisia hizo yuko kafumba macho ,alivyofumbua alimwona issa ameruka kuja kumpiga teke la kifuani 
"Mwanaume alinyoosha mguu mmoja wima mwingine akaupandisha juu issa akakutana na teke la tumboni akadondokea uko ,uwanja wote ukawa kimyaa 
,sauti ya minal ikisikika akisema sangare ,shujaa ,sangare nguvu moja.
Issa kwa hasira akaainuka tena na kukunja ngumi ,ili ampige sangare tayari ashakosea ,sangare alipiga sarakasi na kumpiga tena mateke manne mfululizo ,tumboni mawili kifuani mawili kisha akajizungusha na kumpa ngumi moja ya jicho
,issa akawa anaona nyota nyota ,kwanza akatapika damu aliyokunywa ,ile anainuka akakutana na ngumi mbili usoni ,akadomdoka chali yupo hoi.

Kwanza mzee langu aliinuka na kumwambia " jobwe unaona kitu anachofanyiwa sasa issa ,angali kwa makini ,mtemi nae akainuka akamwambia "issa inuka mmalizie huyo sangare ,zimesalia sekunde 49,issa kweli akajizoa zoa akainuka na wenge ili ampige sangare tayari ashachelewa 

Sangare alivuta hisia yuko ameiba simu ya mtu na wapo kwenye uchochoro anakimbizwa na mbele kuna ukuta mtefu " nini cha kufanya ni kuuruka ule ukuta ili kuwakimbia  watu wasimkamate ,alivyowaza vile 
Sangare alipiga tena sarakasi akapaa hewani na kujizungusha mara tatu juu kwa juu,
Si akampisha issa ,alichofanya alimpiga teke kwenye sikio la kushoto akampiga teke kwenye sikio la kulia ,akajizungusha tena akampiga teke kisogoni akatua chini 
Akampiga mateke ya kifuani alafu akajibinua na kumkandamiza ngumi ya kichwani akiwa chini akamkandamiza 
Halafu akainuka kengele ikalia ndiiii

Issa alikuwa amelala chali kanyooka.,yupo kimya haongei hata neno moja ,refa alihesabu hadi tatu ,lakin issa alikuwa amezimia kabisa  ,mtemi akiwa haamini alichokiona akamkimbilia mwanae na kusahau cheo alicho nacho ,kufika akakuta mtoto wake amezimia ,
Uwanja ukashangaa na kujiuliza sangare ametumia style gani hizi,mzee langu ndio kwanza anacheka ha ha ha ,akamsogelea sangare na kumpongeza kazi nzuri
,
Sangare akamtizama binti minal ambae alikuwa akimshabikia yeye peke yake  na kumpa nguvu alivyotizama sehemu aliyekuwa hamuona ,akatizama mahali amezimkka issa akamwona yuko amemkumbatia issa huku akimwambia inuka sasa issa ,
Issa inuka usife ,inuka nikuambie jambo la mwisho

,sangare akachukia na kuona minal haeleweki mara yupo kwake mara yupo kwa issa ,sangare alienda moja kwa moja hadi kwa mama yake alimfuta machozi na kumwambia "mama usilie bado niko mzima na ushindi nimeupata,

Walikumbatiana mama na mtoto wakalia machozi ya furaha ,issa akiwa amezimika.alibebwa juu kwa juu na kupelekwa sehemu ya kupatiwa matibabu.mtemi alisimama na kusema mshindi amepatikana ni sangare ila huu mchezo utarudiwa kwa leo sangare ameibuka mshindi  ameshinda ,
Mtemi akaondoka na walimzi wake huku mzee langu nae akaondoka na walinzi wake hadi kwenye boma la ng'ombe ,alihesabu ng'ombe mia tano na kumpatia sangare ,kisha akaenda na kwenye hekari za mashamba alimpatia hekari mia moja .

Aliondoka na kurudi nyumbani kwa hasira ,mzee langu aliita mtemi " kwa sasa huna sifa ya kuwa mtemi umebakisha ng'ombe mia tano tu na mimi ninao ng'ombe elfu moja na mia tano,nina hekari 150 achia kiti cha utemi.

Hapo ndipo mtemi akashituka kumbe alikuwa amewekewa mtego ,mtemi alijikuna kichwa na kusema ,subiri mtoto wangu apone kisha tupange mpambano mwingine akishinda mwanangu narudisha mali zangu akishidwa nakupa mali zilizosalia,

Langu alicheka na kuona hapa mtemi anajifilisi mwenyewe ,mzee langu alianza kuongea "kumbuka tukio la miaka50 iliyopita ulimuua mtemi ambae alikuwa anatoka ukoo wa itambu kisha mali zake ukachukua ,
Hivi inaumaje kuona mtoto wa ukoo wa itambu anazirudisha mali?,hebu niambie mtemi,
Mtemi kwa. Hasira aliondoka na kurudi nyumbani alirudi na kumkuta mwanae bado amezimika.

Siku tatu zilipita ndipo issa akazinduka akawa haelewi chochote na kipindi chote amezimika minal alikiwa nashinda nae ,minal alivyoona issa amezinduka ,kwanza alimtizama na kumwambia unakumbu kumbu ya mpambano kati yako na sangare.

Issa akavuta kumbu kumbu ,aliona sangare amepiga sarakasi akampiga ngumi teke kisogoni baada ya hapo nilizimika,
Minal akainuka na.kumwambia " nilikusubiri uinuke ili nikuambie si kana kwamba nilikuwa nakulilia sababu unakufa ,hapana nilikuwa nalia kwanini ulikuwa ukinidanganya kila kitu kuhusu sangare ,
Kwa sasa ndio nimegundua sangare ananipenda mimi na hana wivu kama uliokuwa nawe ,sangare ni mvumilivu ,na baba yako anasema mtarudia mpambano ,ila ahadi umeshidwa kuitimiza kwaheri.

Mtoto wa kike alitoka na kukimbia hadi ka akina sangare ,alifika na kukuta sangare anakula ugali kwa mlenda wa kusaga huku yuko na mama yake ,
Minal alivyofika hakusalimia ni kwamba alimfakamia sangare na kumpiga busu la mdomoni kisha akasogeza chungu cha ugali.
Minal akiwa anatiririsha machozi alianza kuongea 

"Sangare kwangu ni wathamani kuanzia leo nabaki kwako ,ni kweli nilikuumiza moyo wako kila kukicha kila unionapo mimi na issa iniona mwanamke nisiyekuwa na msimamo mwanamke njsiyetulia kwa mwanaume mmoja.,nilifanya hivyo kwa lengo la kukupa ujasiri wa kuishi kwenye hiki kijiji.

Laiti ningelikung'ang'ania wewe tu ,huenda tungekufa wote ,natambua moyo wako unanipenda ila uliamua kufanya siri ,nilienda kwa issa ili kumfanya asiwe na nguvu ya kukunyanyasa ,nilifanya vile sababu baba yake alikuwa na madaraka ,nilijifanya mjinga ili wewe uishi salama ,

Yotee nayatambua vilivyo ,sijalogwa mimi kama ulihisi huenda nimelogwa ili kila jambo analoniambia issa nimsikilize 
Kwangu nilijifanya mjinga ili kukulinda wewe ,sikuwa na ujasiri kama wa kwako kuweza kuua nyoka ,sikuwa na ujasiri kama wako kukaa bwawani siku tatu ,sikuwa na ujasiri kama wako wa kuhatarisha maisha yako kwenye korongo.

Ila uwezo wangu nilitumia unyonge kukulinda na sasa nataka tumalize kila kitu na tuwafanye wanakijiji wapate uhuru nabaki kwako sangare" ni maneno aliyoongea minal kwa hisia sana huku  machozi yakimtoka hapo ndipo mwanaume akaona minal anayo akili akamkumbatia kisha wakakumbatiana.

Mama yake na sangare alivyoona vile mwanae amemkumbatia minal aliinuka tu ili kuwapisha waendelee na mambo yao ,mama alitabasamu na kujisemea mwanangu amekua sasa .

 Basi sangare alimwambia minal ,nimekuelewa na kila siku jinsi ulivyokuwa unafanya vile niliamini huenda una maana yako,
Basi walianza kula ugali wa mlenda wa kusaga wakalishana hakika walipendeza na kuonesha matabasamu

Minal aliuliza "kumbe unakuwaga mzuri ukicheka namna hii ,muda wote mtu wa kukaa kimya hebu lete hilo shavu nikupige mabusu ya mjini mjini ,basi sangare alifanya kama mtoto wa kike alivyotaka
Sangare aliuliza " hukuona aibu kunishangilia peke yako?,
Minal alicheka na kumpiga sangare vikofi vidogo kwenye mashavu ni vikofi vya kimahabati kisha akamwambia "nilifanya vile kukushangilia sababu najua issa ananipenda hivyo nikishangilia anaona wivu najua nitamvuruga kichwa sababu atachukia ninavyokushangilia na hapo lazima apoteze mchezo na ndivyo ilivyokuwa.

Basi walizungumza mambo mengi baada ya kuanza penzi lao rasimi ,tukirudi upande wa issa aligombezwa na baba yake na kuambiwa mchezo utarudiwa na kuhakikisha anazirudisha mali ili aendelee kuwa mtemi.
Mimi baba yako nikiendelea kuwa mtemi hata huyo mwanamke wako unayemtaka lazima atakukubali kwa amri ya mtemi.
Issa alianza kufanya mazoezi kwa hasira mno ,akikumbuka jinsi alivyopigwa hakika aliumia sana.

 Kesho kutwa kutakuwa na mpambano tena wa issa na sangare kwenye uwanja wa maonesho ili kumtafuta shujaa wa kijiji ,ni taarifa ambazo zilizagaa kila mahali ,mzee jingi alivyozipata alimfuata sangare na kumchukua kwenda nae porini.

Mzee jingi aliikuwa ameshikilia fimbo mbili ,alivyofika porini alimpa fimbo moja sangare kisha akaanza kuongea " sangare wewe ni mtaalamu wa ngumi nimegundua hapo sitakufundisha ,ila siku ile nilishuhudia unapigwa sana kwenye mchezo wa fimbo na issa.
Issa unavyomwona anavyopambana ,hayo mazoezi nimemfunza mimi ,sasa nataka nikufundishe namna ya kupigana kwa kutumia fimbo ,je uko tayari?,
Sangare alitabasamu na kusema niko tayari tuanze sasa  basi mzee jingi alianza kumfundisha sangare namna ya kutumia fimbo.

Tukirudi kwa mtemi ,alishitukia dili anaweza kupoteza utemi wake kupitia mpambano japo anamwamini mtoto wake,alimwita issa njoo twende kwenye chumba cha uganga tukaangalie je mchezo tutaushinda?
Issa na baba yake wakaingia kwenye chumba cha uganga kwa ajili ya kuangalia mpambano watashinda ama watashidwa.walivyoingia mganga alipiga manyaga yake ili awapatie majibu ,kumbuka kila mganga anae tumia uchawi lazima ruhusa ya jini la kutibu apewe na malikia mweupe.

Basi mganga jinsi anavyopiga manyaga kwenye ulimwengu wa malikia wanawaona kabisa jinsi wanavyohangaika ,malikia mweupe alimtizama mwanae ambae alipewa jina sangare.
Na sangare alivyoendaga kwenye ule ulimwengu,
Alimwangalia mwanae toka amepewa lile jina hajawahi kulia tena ,na alianza kukua mwali ,maana yule mtoto toka amezaliwa na kupewa jina kipepeo mweupe hakuwahi kukua hata kidogo ,na ameishi miaka 90 akiwa mchanga

Kwa sasa ameanza kukua wala halii kama zamani akiambiwa lala mtoto analala na kutulia 
Malikia mweupe sasa aliwaza awape jini aweze kumloga sangare ashidwe mpambano au asiwape jini,na akimpa jini mganga anae mtumia mtemi basi sangare analogwa na lazima atashidwa mpambano.

JE NINI KITAENDELEA?

Usisahau. Kukoment ewe mdau wangu

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.