Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 24

Story ;SANGARE
BY:Mogy shine
No.0621302436
///////////////////////

          SEHEMU YA 24
       Tulipo ishia jana,Akishinda sangare ni kwamba mali za mtemi tunazichukua na tukizichukua hapo hapo anakuwa hanavigezo vya kuwa mtemi .
Mzee langu akacheka lakin jobwe alimtizama baba yake na kuona maamuzi yake si mazuri
Anamju issa anajua kupigana hivyo ataweza kumuua sangare

Zilipita siku mbili ndipo mtemi alimwita mzee langu wafanye makubaliano wasaini hizo mali mbele ya wanakijiji kisha waandae mpambano ,kama kawaida filimbi ya kijiji ilipulizwa wanakijiji walijikusanya kwenye uwanja wa maonesho ,ndipo mtemi alimwita mzee langu kwa nia ya kuweka makubaliano.

"Mtemi alianza kuzungumza mbele ya kijiji " nimewaita hapa kuwa mashuhuda baada ya kukaa kimya kwa muda wa miaka miwili bila kushiriki mapambano ya kupigana hatimae leo kapatiaka kijana ambae anatakiwa kupambana na issa,
Wangapi wanamjua issa kwa mapambano?,mtemi aliuliza na kufanya kila mwanakijiji anyooshe mkono na kusema tunamfahamu ,huyo hajawahi kushidwa anawapigaga hadi anaua ,wananchi waliitikia kwa nguvu na kumfanya mtemi atabasamu.

Kisha akaendelea "kwa kipindi kirefu tumekuwa tukizozana kuhusu nani awe shujaa wa kijiji naimani kupitia huu mpambano  tutampata," hapa mzee langu ametoa ng'ombe mia tano na hekari mia moja nami natoa kama yeye halafu tunaandikishana hapa na tunasaini mbele yenu wanakijiji sawa?

"Sawaaaaaaaaa!!" Wanakijiji waliitikia kwa pamoja huku kila mtu akijiuliza inamana issa anataka kurudia mpambano na jobwe au ni nani maana anataka kupambana nae ,kama ni jobwe ashawahi kupigwa na issa nusu auliwe sasa huu mpambano issa anapambana na nani?
Wanakijiji walianza kujiuliza 
Ndipo mtemi alianza kuongea tena "issa atapambana na sangare  kesho kutwa kwenye huu uwanja ,vile vile tutaalika vijiji vya jirani waje kushuhudia

Kila raia alikaa kimya ,maana wanamjua vizuri issa huwa ni mtaalamu wa kupigana hasa kwa kutumia fimbo.makaratasi yalitolewa mzee langu alisaini na sangare pia akasaini ,pia mtemi akasaini ,ilivyofika zamu ya issa alivyo na masifa 
Alitoa kisu kidogo kisha akachana kidole gumba chake chapu
Damu ilivyotoka akakandamiza kwenye karatasi hio ndio saini yake inaashiria kwenye mpambano atamwaga mtu damu,wanakijiji walishangilia sana.
Walivyomaliza kushuhudia ,kusaini ndipo mtemi alimalizia ,mpambano wa kwanza watapambana kwa kutumia fimbo na mpambano wa pili watapambana kwa ngumi tu ama kutumia viungo vya mwili ,basi wanakijiji walivyomaliza kushuhudia walitawanyika na walirudi majumbani

Siku hio  sangare alienda kwa mzee jingi kwa ajili ya kuomba ushauri " jingi alimtizama sangare na kumuuliza ushawahi kupambana kwa kutumia fimbo?,sangare akajibu hapana sijawahi
Mzee jingi aliinamisha kichwa kwa muda,alianza kuzungumza

 "kwenye hiki kijiji ,mtemi amekuchukia ndio maana anaamua kufanya jambo kama hili ,halijawahi kutokea pambano lenye kutoa mali nyingi kama hili ,huwa wanatoa ng'ombe kumi ama ng'ombe 30/lakin safari hii ng'ombe mia tano.
Halafu issa anautalaamu wa kupambana kwa kutumia fimbo alishawahi kupiga watu 54 kwenye mapambano yake na mapambano yake hajawahi kushidwa hata kidogo.

Sangare ukiona huwezi kupambana nakushauri toroka kwenye hiki kijiji,ondoka kabisa maana issa atakuua na anavyokuchukia lazima atakuua ,mzee jingi aliongea na kuondoka,hakutaka kabjsa kumwangalia sangare kwa maamu,i aliyochukua.
Sangare alikosa raha alirudi nyumbani alikuta mama yake amepika supu  uyoga na viazi vitamu,
Sangare alianza kula " mama alimuuliza "kwahio mwanangu kwasababu umeniona mimi basi umeamua ufe kwa namna hio?

,kwanini umekubali kufanya mpambano na issa ,yule ni hatari atakuua mwanangu achaa bora utoroke urudi dar sitaki kushuhudia ukiuliwa mbele ya watu.

Sangare hakumjibu mama yake alikula tu alivyomaliza akatoka akaamua azunguke maana kila mtu akimwona anamshauri asipambane na issa ni hatari akiwa anatembea aliwaona minal wamekaa mahali wanaongea na issa.

" issa alimwambia,nikimuua sangare kwa sasa tutaishi huru ,lazima nishinde minal nakuahidi ,minal alimtizama issa na kumwambia leo nakupa ahadi kutoka moyoni

"Najua unajiamin sana na kila mtu kijijin anasema wewe unaujuzi wa kupigana kwa kutumia fimbo ,usije ukajifanya wewe hodari wa kupigana ukashangaa unapigwa sitaki iwe hivyo nataka umpige sangare na umuue kama unavyosema utamuua.
Ukimshinda sangare hapo hapo nakubali unioe pale pale uwanjani kila mtu ajue

Maneno ya minal ,sangare aliyasikia kisha akawaza inamana hawa watu wameungana ili mimi niuliwe wenyewe wao waishi ,sangare akaamua kuondoka kabisa eneo lile

Minal aliendelea kumweleza issa ,ila sangare akikushinda hapana kunioa mimi na kuanzia siku hio usinifuate mimi nakuahidi hivyo,minal alimsogelea issa kwa mara ya kwanza akamubusu shavuni na kumwambia nakutakia ushindi mwema ,minal akaondoka na kurudi nyumbani
Maneno ya minal yalimfanya issa furaha izidi mara dufu nae alirudi nyumbani na kufanya mazoezi

Sangare wala hakufanya mazoezi hata kidogo zilikatika siku mbili hatimae siku ya mpambano ikawadia  wanakijiji waliwahia mapema uwanjani ili wapate nafasi za mbele za kushuhudia mpambano, kulikuwa na pande pili ,upande wa mzee langu pamoja na upande wa mtemi.

Watu wa vijiji vya jirani walipata mwaliko nao walifika kwa ajili ya kushuhudia mpambano.,muda wa kuingia wapambanaji uwanjani uliwadia ,issa kabla ya kuingia uwanjani alipewa damu ya ng'ombe kwenye kipeyu kisha akanywa baba yake akatabasamu na kumwambia kapamabe ,watu walimshangilia issa uwanja mzima maana ndio wanamtegemea kwenye mapambano.

Issa akiwa uwanjani alimwona minal amesimama hata hashangilii,alimkonyeza kisha akamwambia ushindi lazimaa na leo lazima nikuoe.
Ikafika zamu ya sangarekuingia uwanjani uwanja ulikuwa kimya hamna aliyeshangilia ,minal aliwaza ,toka anaatoka dar walikuwa na sangare ,amemsaidia vitu vingi akaona ametegwa hata mama yake hajamshangilia mama yake alikuwa analiamaana anajua mtoto wake anaweza kuuliwa uwanjani.
Minal aliona si vyema alianza kushangilia sangare shujaaa pambana kishujaa sangaree shujaa.

Issa si akasikia yaani mchumba wake anamshabikia adui yake hapo issa akachukia mbaya,muongozaji wa huo mpambano aliingia na fimbo mbili ngumu na kubwa ,alimkabidhi moja sangare na nyingine issa.

Akasimama kati kati ,akaongea "mpambano wa sasa ni wa kutumia fimbo " unaruhusiwa kupiga kokote ,hata kuua,huu mchezo unachukua dakika tano tu. Kwasasa unaruhusiwa mtizame adui yako.issa na sangare wakatizamana ,
Kengele ikavutwa ngeee
Mpambano ukaanza ,watu wanataja issa issa issa

Isa alikuwa mtaalamu wa kutumia fimbo aliruka kimasai na kumtandika sangare fimbo ya mgongoni sangare hajakaa sawa fimbo inatua kifuani.
Issa akatulia  akaanza kuonyesha mbwebwe baada ya kusikia watu wote wanamshabikia yeye ,
Alizungusha  fimbo sangare hawezi kupigana kwa kutumia fimbo alinyanyua na kumpiga shingoni ,
Sangare akawa anaugulia maumivu

Issa alimwambia sangare "mbona unatetemeka leo nakuua uje ,sangare alijibu twende kazi ,sangare akannyanyua fimbo ampasue kichwa issa akashangaa inakigwa na issa ,isa akainama akakwepa 
Issa akamtandika miguuni   
Refa akataja imebaki dakika moja ,hapo ndipo akachochea mto ,issa aliruka na kumpiga sangare fimbo ya kichwa sangare akashuka chini puuu,
Akalala chali ,sheria ya mpambano hata ulale chini unapigwa tu ,sangare akaanza kutandikwa kwa nguvu fimbo za tumboni kwa nguvu puuu ,mara anapigwa kichwani mahala popote.

Issa akikumbuka maneno ya minal " ukimuua sangare basi sisi tutaishi vizuri"hapo ndio issa akaongeza kutandika alimtandika sangare kama mtu anae ua nyoka

Sangare akatapakaa damu mwili mzima hata nguvu ya kukinga fimbo hakuwa nazo ,issa aliendelea kutandika tu ,mtemi akatabasamu na kujisemea moyoni
"Mzee langu hapa umechemka mali zako nazichukua kiulaini ,alisimama na kusema issa ua sasa  tumalize mchezo ,issa kusikia sauti kwa baba yake aliruka hewani ni kwamba akitua chini anapasua kichwa cha sangare na kumwaga ubogo ,

Wanakijiji wenye roho nyepesi walifumba macho wapo waliendelea kushangilia ,mama yake sangare machozi yamemtapakaa uso mzimaa
Sangare akiwa na hali mbaya alijiviringisha pale pale issa anatua chini akamkosa sangare akanyanyua fimbo ampige tena 
Kengele ikavutwa tayari dakika zimeisha issa alitulia 

Uwanja mzima ukashangilia " issa shujaaa isaaa uaaaa ,kipindi chwa kwanza kimeisha issa hajafanikiwa kumpasua kichwa sangare ,
Mzee langu na kundi lake waliingia uwanjani na kumwinua sangare akiwa ametapakaa damu ,jobwe alimtizama sangare na kumchukia sana baba yake ,yaani tamaa ya kutaka utemi anamponza mtoto wa watu ,sangare alikuwa anahema tu huku amefumba macho yaani ametandikwa fimbo za kutosha.

Upande wa issa wao walishangilia tu ,minal alivyoona vile alikimbia aliko sangare akiwa ameshikilia kitambaa alianza kumfuta damu ,huku akiita sangare ,sangares fumbua macho usifa ili urudi upambane tena na issa ,
Sangare alifumbua macho aliona mtoto wa kike anafuta damu ,alitabasamu huku anasikia maumivu makali mwilini
"Alimwambia minal unataka nishinde?,minal akajibu ndio nataka ushinde turudi wote dar es salamu.sangare akainuka na kuwaambia niko salama mimi si wa kufa leo kama mnavyodhani nitaingia mpambano wa pili.

Issa akatizama upande wa pili akamwona tena minal amehamia upande wa sangare ,hapo ndipo hasira zikamjaa ,alitaka kwenda kumchukua minal ,baba yake akamwambia tulia kisheria hauruhusiwi kwenda kwenye bechi la adui yako.

Issa akatulia huku anahasira alijisemea moyoni " sangare vyote ulinishinda ila kwenye kupigana nakuua ,halafu minal wangu nabaki nae ,issa akaendelea kukumbuka "mpambano unaofuata ni wakutumia ngumi ,mateke ,hedi viwiko kila kitu ,pia ashawahi kumpiga ngumi sangare basi akasema nakumaliza sasa hivi.

Muda wa mapumziko ukaisha kengele ikavutwa ngeee ,issa kama kawaida yake akapewa kipeyu cha damu akanywa kisha akaingia ,sangare nae akaingia.
Wakaamurishwa waangaliane kwa sasa ni kupigana ngumi kwa ngumi,
Issa alimwambia " sangare mbona huna ushujaa wowote kipindi  cha kwanza nimekuchapa vilivyo sasa nakumalizia ,issa alirusha ngumi akampiga sangare shavuni sangare akaserereka na kudondoka chini kabla hajatulia vizuri isa akamkandamizia na mguu kiunoni.
Sangare akadondoka chini ,kisha akainuka upesi ,sangare akataka kujibu mashambulizi issa akazipangua ngumi zake na kuzikwepe,
Issa akarusha ngumi na kumpiga sangare puani sangare akadondoka chali ,kisha sangare akacheka ha ha ha.na kufanya uwanja mzima watu wakae kimya,
Alimtizama issa ambae anawaambia watu shangiliaa ,shangiliaaa!!!

Sangare akatizama muda zimebaki dakika tatu ,akajisemea moyoni ,sangare tuliza akali ,kisha akaanza kukumbuka kipindi alikuwa dar es salaam alikuwa kibaka anae ugopeka mtaani ,alikuwa na uzoefu wa kuruka kuta ,kuvuka fensi za umeme pasina kugusa ukuta ,sangare alikuwa akikukamata anakupiga ngumi ya uso unazimika siku nzima ,akakumbuka alikuwa mtaalamu wa kupiga sarakasi.

Akacheka tena na kumwambia issa hebu njoo tuzichape ngumi sasa akili yangu imekumbuka maisha yangu ya nyuma

JE NINI KITAENDELEA?

USISAHAU KU COMMENT

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.