Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 23

Story ;SANGARE
BY;mogy shine
No.0621302436
////////////////////////

         SEHEMU YA 23
         Tulipo ishia jana,Jiwe linazidi kuteremka kwa chini kuna shimo refu ambao kuna mto umepita kwa chini pia kulia na kushoto pana jabali ambalo linateleza si rahisi kupita 
Na wakizubaa jiwe linawapitia na kuwatupia mtoni
Sangare alipaza sauti " angalieni juu jiwe limeporomoka.,ile wanageuka jiwe hili hapa
Minal alifumba macho huku issa akitafuta njia ya kujiokoa

"Issa alikuwa mwepesi alitizama pembeni aliona kuna mti ambao umeinamia kwenye jabali aliwahi na kuurukia kisha akaninginia 
Sangare aliona minal hatapa msaada aliwahi na kumnyanyua minal kisha akamweka kwenye jabali ambalo lina teleza halafu yeye akapitiwa  na lile jiwe ambao ni kubwa lilimsomba sangare na kumdondoshea mtoni puuuuu!!!!

Ukimya ukatawala issa akashuka mahali amening'inia aliwahi kwa minal na kuuliza uko salama?,minal akiwa anahema alimwambia niko sawa ila sangare je atakuwa salama?.

Issa hakutaka hata kuchungulia mtoni aone sangare amepona ama amekufa alimshika minal mkono na kumwambia twende hili eneo si salama,nishakuambia sangare si wa kumwamini ona alikuwa anataka kutuua ,halafu ndio akatujulisha eti jiwe linateremka.,yaani jiwe kalitega yeye ili atuue jinsi mungu anavyotupenda sisi hatujafa ,yeye amekufa.

Minal kusikia vile akauliza " ni kweli atakuwa amekufa?,issa alitabasamu na kusema."huu mto naujua vizuri kwa chini una miamba ya mawe sasa kama kadondokea basi atakuwa amedondokea kwenye mawe halafu jiwe la juu likamshukia kichwani basi atakuwa hatamaniki hata kidogo.

Minal akaingiwa roho ya huruma na kusema hata kama alikuwa anataka kutuua twende tukamuone bana .issa Ndio kwanza anazidi kumpeleka minal mbali waliondoka na kurudi nyumbani kabisa.

Tukirudi kwa sangare baada ya kusombwa na lile jabali aliteremshiwa kwenye mto hakuwa na ujanja kwa bahati nzuri chini palikiwa na mti ndipo sangare alidaka tawi la mti alijivuta na kujiokoa ndipo jiwe likapita na kutua chini puuu!
Hio ndio ikawa pona pona yake
Lakin alikuwa ameteguliwa kiuno baada ya kusobwa na jiwe.

Sangare alihangaika sana kwenye ule mti ndipo akafanikiwa kushuka chini kabisa kwenye ule mti ,alikuwa akitembea kwa shida halafu sehemu hio ilikuwa na mawe ,sangare kila akipiga hatua kadhaa alishidwa na kujikuta anakaa tu.

Sangare aliita minal,issa !! Ili kama wapo wamepe msaada wa kutoka kwenye ule mto.issa na minal walienda hadi nyumbani ila minal alikuwa na wasi wasi sana juu ya  sangare aliwaza nitamtoroka vipi issa ili nikamwone sangare kama kafa ama mzima.,
Minal akiitizama issa na kumwambia "nisubiri hapa kaa na bibi ngoja niende msalani mara moja ,issa akamjibu ondoa shaka na kusubiri ngoja niendelee kupewa hadithi na bibi.
Basi hapo ndipo minal alipata mwanya na kukimbia kurudi eneo lile ambao walikuwepo na issa.

Minal alifika na kuanza kuita sangare!,sangare ,sangare akiwa amepoteza matumaini alikuwa amelala kwenye mto ,ndipo minal alitafuta sehemu ya kupita alishuka hadi mtoni ndipo alivyoteremka alimkuta sangare amelala.

Minal akakimbia na kufika kwa sangare alimtingisha na kuita sangare upo salama?,sangare alifumbua macho na kumwambia niko salama ,kwa nini umekuja kwenye hili eneo la hatari namna hii.minal akamjibu nina wasi wasi na wewe nimekuja kukusaidia ili tutoke kwenye huu mto.
Sangare alitulia na kumwambia ,mimi sitaweza kupata msaada maana kutoka nimeshidwa kiuno changu kimeteguka ,
Minal alivyoambiwa vile,alimkumbuka mama yake kipindi alikuwa  ness pia alikuwa na uwezo wa kuwanyoosha watu walioteguka hata ukivunjika alikuwa mtaalamu anakunyoosha sehemu umevunjika kisha anakufunga na unapona,

Minal akasema lazima nitumie ujuzi wa mama kumtibu sangare ,alimwangalia sangare alivyo lala alimwomba alale kifudi fudi ili aweze kumtibu ,sangare wala hakubisha alifanya vile ndipo minal alipeleka mkono kwenye kiuno cha mwanaume ,alihesabu kisha akabinya mifupa kwa nguvu ,kitu kikasikika koooh
Minal alitabasamu na kusema hakika nimeweza nikirudi dar nitamwambia mama nami nimekuwa daktari.

Sangare alishangaa alijaribu kuinuka akasimama akajaribu kujinyoosha kidogo maumuvu akawa anayasikia kwa mbali,alimtizama minal na kumwambia asante ,kisha akamuuliza wewe ni dokta?
Minal akajibu " hapana si dokta na wewe ndio mtu wa kwanza kujaribu kukutibu na nimeweza ,tatizo muunganiko wa mfupa wa uti wa mgongo ulikuwa umepishana ila nimeunyoosha kwa sasa upo salama.

Japo sangare alikuwa akipata maumivu ila si kama mwanzo ,walijitahidi hadi wakatoka walivyofika nje ,minal akamuuliza sangare kwahio ulikuwa unataka kutuua mimi na issa?,kama hutaki kuniona na issa basi niambie ili tuondoke kwenye hiki kijiji na si kutaka kuwaua ,
Sangare alifikiria akaona tayari minal amejazwa uongo na issa kwamba nilikuwa na nia ya kuwaua.
Sangare alimtizama sana minal anampenda ila hajawahi kumwambia ,yaani mapenzi yake yapo ndani ya moyo na ogopa sana mtu anae kupenda ndani ya moyo penzi lake linakuwa tamu asikuambie mtu.
Sangare hakumjibu alimshika minal na kumpeleka sehemu jiwe lilikoteremka ndipo minal akajionea 

Mti mkubwa ulidomdoka eneo lile na kupiga jiwe likateremka ,minal akautizama ule mti shina lilikuwa limeoza halafu kwa ndani kuna shimo.hapo ndipo akagundua maneno aliyoambiwa na issa ni ya uongo.
Minal alimgeukia sangare na kumkumbatia alianza kuongea "
Sangare nashidwa kukuelewa hata kidogo ,nimepoteza kabisa hisia zangu kwako ,lakin ki ubinadamu kila ninapokuwa na tatizo wewe ni msaada wangu,
Sangare kwako mie mjinga ,ila kuna giza nene lipo kwenye mboni zangu halafu masikio yangu yanaamin na kusikia maneno ya mtu mmoja.
Aliongea mafumbo kisha akamwachia sangare ,sangare aliwaza yale maneno akayaelewa sababu yeye anae akaili ukimwambia  fumbo hapo hapo anaelewa.

Sangare nae aliwaza "kwa mtemi kuna mganga ambao wanamtumia kwa ajili ya kuagua mambo yao na kutibu watu,yawezekana issa amepewa dawa ambayo inampumbaza minal ndio maana hajawahi kumwona amefanya jema ,kila kitu anacho ambiwa na issa huona kipo sawa,
Ndio maana minal anasema kuna giza nene.

Sangare amegundua akatabasamu tu hakutaka kumwambia chochote minal,walitembea hadi kwa bibi yake na minal,ile wanafika walimkuta issa amesimama nje yaani amemtafuta minal hadi chooni
Kitendo cha kumwona minal yupo na sangare alimfuata sangare kwa hasira " nishakuambia minal ni mchumba wangu kwanini unamfuata fuata ,alimtandika konde zito la ngumi shavuni ,sangare akapepesuka kabla hajatulia alimpiga ngumi puani alimdondosha chini na kuanza kumdunda ngumi ,
Sangare nakuua acha kutembea na  minal wangu ,kwasasa nitamfanya hata jina lako asiweze kulitamka awe ananitaji mimi hata akikuona wewe ateme mate mpuuzi wewe ,unataka kutuua halafu ukajifanya unamsadia minal ili uonekanishe shujaa ,kwa sasa tushagundua mbinu zako hakika unajisumbua.

Sangare alijiinua chini maana kapigwa ngumi za kutosha sana na issa ,wakati anapigwa vile mzee langu pamoja na jobwe walikuwa wanashuhudia ,lakin mzee langu anayo mbinu anataka kumfilisi mtemi kupitia ugomvi wa sangare na mwanae.

Mzee langu alifika na kumsifia issa "hakika wewe ni shujaa dakika mbili umemdondosha sangare ," kama sangare anataka kuwa shujaa na anakufanya unakosa amani ,tunatambua wewe ni mpiganaji mzuri hapa kijijini ushashinda mashindano 54 umeua watu kwenye uwanja wa mapambano ,kwanini usimwambie baba yako ,mfanye mpambano wa kupigana na sangare atake mshinda mwenzake ndio anakuwa shujaa?

Eti issa hili jambo walionaje?,"hakika issa alivyoambiwa vile na mzee langu kwanza alitabasamu na kumwambia asante "umenikumbusha nilikuwa nawaza nitafanya nini ili niwaaminishe wanakijiji mimi ni shujaa ,basi sasa hivi naenda kumwambia baba tuandae mpambano " issa akazidi kukumbuka ashawahi kumpiga ngumi sangare mara mbili huwa anampiga tu na hawezagi kumpiga

Issa akaona hapa ndio penyewe "mzee langu  alimtitizama issa na kumwambia " tunajua sangare hana mali ,ila mimi nitamlipia nitatoa  ng'ombe miatano na hekari za mshamba mia moja ,ukishinda wewe unavichukua pia ukamwambie na baba yako atoe ng'ombe mia tano na hekari 100.

Issa yeye ni kutabasamu alisema nitaenda kumweleza sasa hivi ,nataka nimpige sangare mbele ya kijiji nimuue kabisa maana sheria zetu,zakupambana zinaruhusu kuua

Issa alienda moja kwa moja kwa baba yake akamweleza kuhusu kuandaa mpambano wa kupigana kati ya isa na sangare ili waweze kumpata shujaa"kwanza mtemi alicheka sana na kusema "mwanangu hilo wazo ni zuri sana na wewe ni mtaalamu wa kupigana hasa kwa kutumia fimbo ,umeua watu nane ,umewavunja miguu watu wengi ,kwenye kupigana mwanangu nakukubali ,hadi umefanya kijiji chetu kinaogopwa na vijiji vya jirani,
Mimi baba yako niko tayari ,kutoa hizo mali ili ushiriki,kama mzee langu anatoa hizo ng'ombe hapo tutakuwa tumememuweza ,najua atakuwa na mali chache hataweza tena kuniny'ang'anya utemi na sheria zetu ili uwe mtemi lazima uwe na mali nyingi kuliko mtu yeyote kijijin
Issa mwanangu anza mazoezi kuanzia leo ,ili baada ya siku tatu tufanye mpambano ,ukipata nafasi muue kabisa
Issa alicheka na kusema " baba tunavyozungumza leo nimetoka kupigana nae na nimepiga hawezi hata kurusha ngumi huyo nitamuua.

Tukirudi kwa sangare nae alielezwa na mzee langu "kuhusu mpambano ,sheria ya mpambano ukikataa kupambana wakati mpambano umeandaliwa unafugwa kwenye gereza ama kuuliwa kabisa,hivyo tunaomba ukubali sisi tutakulipia mali ,na ukishinda zinakuwa zako.
Sangare alimtizama sana mzee langu na kukumbuka siku alivyopata dawa ya kumtibu minal ,kisha issa ndio akatangazwa mshindi ,alimwambia mzee langu haina shida nitapigana nae
Kisha sangare akaondoka na kurudi nyumbani kwao

hapo ndipo mzee langu amecheka na kumshika mwane bega " jobwe kama huyu sangare anatoka ukoo wa itambu najua atashinda tambua huo ukoo haujawahi kushidwa sasa tusubirie hizo siku tatu tuone itakuweje.
Akishinda sangare ni kwamba mali za mtemi tunazichukua na tukizichukua hapo hapo anakuwa hanavigezo vya kuwa mtemi .
Mzee langu akacheka lakin jobwe alimtizama baba yake na kuona maamuzi yake si mazuri
Anamju issa anajua kupigana hivyo ataweza kumuua sangare.

Je nini kitaendelea?

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.