Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 22

Story ;SANGARE 
BY;Mogy shine
No.0621302436
///////////////////////

        SEHEMU YA 22
    Tulipo ishia jana,Sangare akakumbuka alivyopataga jiwe la namba sangare alimpiga mshale wa begani ,leo tena amepata dawa ya kumtibu minal ambae issa anampenda sana 
Huyu issa si ataniua leo ,sangare aliwazaa

Lakin alivyotizama aliona watu wengi hata mtemi pia alikuwepo akina ,jobwe akina runde watu wengi ,sangare akajisemea huenda usalama upo aliamua kutoka nje ya lile bwawa sangare akiwa ameshika kile kibuyu chenye maji ya baridi aliyopewa na malikia,

Mtemi alicheka ha ha ha ,hakika wewe sangare ni binadamu  wa ajabu ,umesababisha tumetolewa majumbani sababu yako,kwanini umekaa kwenye maji siku tatu ,umekaa tu ,tunakuita unatuangali au unataka kijiji changu kipate sifa mbaya?
Ni swali alilo uliza mtemi huku akimsogelea sangare,

Sangare aliwaza inakuweje aambiwe alikuwa amekaa kwenye maji siku tatu ,wakati yeye alijikuta ameenda kwenye ulimwengu mwingine,
Sangare aliwaza jibu la kumpa mtemi ndipo akasema "mtemi sikua na maana hio kwamba nimekaa kwenye maji sababu ya ile dawa ,na sikukaa ili nifie kwenye maji sababu ya ile dawa 

Lahasha nilizama kwenye tope na nilishidwa kabisa kutoa miguu kwenye maji hata kupiga hatua ,sangare aliamua kudanganya ,mtemi alichomoa sime yake na kusema  vijana wamehangaika kutaka kukuokoa ili wakutoe kwenye maji ila kila wakitaka kukukamata wewe unazama ndani ya maji na kuibukia upande wa pili,
Mtemi wa kijiji hiki cha lain chungu ametoa tamko kwangu kuwa wanga wanao wanga kwenye hili bwawa kama wanatoka kwenye kijiji changu wauliwe .
Haina budi kukunyamazia 
Mtemi alimfuata sangare ili amkate na sime ndipo sauti ilisikika ikisema " achaa achaa 
Mtemi aligeuka alikutana na mzee langu ,huyu ni baba yake na jobwe hakika anazo mali hadi mtemi anamwogopa ilibidi atulie na kumsikiliza anasemaje.
Mzee langu hakuwa peke yake alikuwa ameongozana na mzee jingi walifika na kusema."
Unahisi ukimuua huyu sangare kijana wako ndio atakuwa hana mpinzani?
Mtemi ki ukweli mimi nimefurahishwa na kujituma kwake sangare hanaga majivuno ,vijana wako ulio  watuma kazi waitafute dawa wamerudi wako hoi.

Leo hii sangare amekuja kwenye hili bwawa kavumilia kwa siku tatu hadi ameipata dawa naiona hio hapo anayo kwenye mkono ,
Mtemi semeni kama mnajambo lingine na si kutaka kumuua kijana wa watu.

Mzee langu aliongea na kumshika mkono sangare waondoke eneo hilo warudi nyumban.,lakin vicheko vilisikia kwenye bwawa vya watu ambao wanaishi kwenye ulimwengu wa malikia mweupe.
Ni bwawa ambalo lina maajabu yaani ulimwengu wa akina malikia wakiongea unawasikia ila hawaonekaniki kwa macho ,vile vile kila wakifanya jambo unawasikia ila huwezi kuwaona.

Sangare wakati anaondoka eneo lile alilitizama sana lile bwawa maana alivyokuwa kwenye ulimwengu wa malikia aliambiwa hilo si bwawa kama tunavyoliona hilo ni wingu ambalo linazuia jua ili lisimwathiri malikia mweupe.

Ni kwamba weupe wake hajawahi kuguswa na jua hata kidogo ,vile vile sangare alivuta kumbu kumbu ,watu ambao ni wafu ali waona kwenye ulimwengu wa malikia walikuwa na ngozi lain ni kweli kule hapanaga jua.

Mtemi alimwambia mwanae "huyu sangare sasa anataka kutawala kijiji kama ameweza kukaa kwenye maji siku tatu na ameipata dawa inaonekana ni mvumilivu na leo hii ameipata dawa unahisi nini kitatokea issa,
Inabidi tufanye jambo tumuondoshe kwenye hiki kijiji ,kama ameanza kupewa nguvu na langu ,tambua huyo ni tajiri mwenye mali nyingi na ndio alitakiwa awe mtemi ila ameniachia tu siku akitaka kuwa mtemi anauchukua sababu ana mali.
" baba usijali mimi bado naamini mimi ni shujaa na huyu sangare haniwezi ,issa bado aliendeleq kujitapa.

Walizungumza mambo mengi ,wakiwa wamepanda punda maana usafiri wao ni punda ,hakika walivyokaribia na kijiji cha mtamaa waliona wanakijiji wengi wamejikusanya huku wakiimba.Sangare shujaa ,shujaa wetu ,sangare shujaa nguvu moja ,waliingia kwenye uwanja wa maonesho ndipo alimwona mama yake amelia hadi macho yamevimba
Sangare alishuka kwenye punda na kumwona minal amesimama huku  analia amekumbatia masikio yake alitamani asikie ila amekuwa kiziwi 

Sangare alishangaa wanakijiji wanamshangilia."ndipo akakumbuka maneno ya malikia "chagua utajiri na si kuchagua kusaidia binadamu ,hakika binadamu ukimsaidia kesho anakugeuka.
Sangare alizidi kumtizama ndipo aliona vilema wa kijiji wakihangaika ,aliona vipofu wote wapo kwenye uwanja,sangare hakuongea chochote alichofanya alifungua kile kibuyu na kumimina maji kidogo kwenye mkono kisha akamwekea minal kwenye masikio yote. Mawili ,hapo hapo sangare akaita " minal unanisikia?
Minal kwanza haamini kama amesikia aliitika kwa nguvu "abee sangare kwa sasa nakusikia ,minal alitaka kumkumbatia sangare amshukuru kwa kumsaidia  kuponesha masikio ,lakin gafla alimwona issa akiwa emebebwa juu juu hajiwezi.
Minal alisitisha ndipo issa alishushwa mbele ya umati.sangare hakujali aliwawekea vilema ,vipofu kila mtu mwenye ugojwa alivyomaliza alimfuata jobwe kisha akamwekea kwenye ikulu kisha akatabasamu " jobwe kwasasa wewe ni kidume hakikisha mama tini unamfanya afurahi,
Pia alimtibu  jobwe sababu alikuwa hana uwezo wa kumpa mwanamke mimba,
Mtemi alisimama kati kati ya uwanja "alianza kuzungumza " wanakijiji kama mlivyotuona ,tumeshinda kwenye bwaawa kwa ajili ya kuitafuta hio dawa ambae tumempa sangare amewatibu

"Hapa chini nadhani mnamwona kijana wangu ndio amefanikiwa kuipata hio dawa ,kwakuwa kijiji chetu kina upenzani wa sisi kwa sisi basi mzee langu ametunyang'anya dawa ili aseme sangare ndio shujaa. Nathibitisha mimi mtemi wenu sangare hakuipata hio dawa ila kijana wangu issa ndio ameipata.kwanza huyu

Sangare alipotea na wala hakufika kwenye hilo bwawa sababu ni mgeni basi ameokotwa porini ,naomba mmpigie makofi kijana wangu issa kwa ushujaa wake.
Mtemi alipindisha maneno issa akapongezwa na kuonekanika ameshindaa ,mzee langu alishangaa imekuwaje tena sangare apate dawa halafu atajwe mwingine shujaa.
Pale pale  wanakijiji wakabadilisha kuimba walianza kutaja ,issa shujaa ,issa shujaa ,maana wanakijiji wanamsikiliza mtemi jinsi anavyosema.

Minal alimtizama issa ambae amelala chini alianza kulia na kumkimbilia na kumkumbatia " alianza kuita issa inuka basi nikukubalie issa usife asante kwa kuniponya ,inamana mimi ndio nimekuponza hadi uwe katika hali hii inuka issa

"Wakati issa anajifanyisha na ndio mbinu walioipanga na baba yake alimfanya mtoto wa kike alie sana wanakijiji walimwonea huruma sana issa na kumwona ni shujaa amejitoa sadaka maisha yake sababu ya mtoto wa kike.
Sangare aliangalia " akamkumbuka malikia "binadamu ni wabaya hata ukifanya wema bado watakugeuka tu.
Sangare aliyaamini maneno ya malikia mweupe"

Mtemi alisimama na kusema " mwanangu anayo hali mbaya lolote likitokea tutawajulisha kwa sasa wacha tumuwahishe kwe matibabu ,basi issa alibebwa juu juu na kupelekwa kutibiwa.
Issa alijifanyisha na si kana kwamba amelemewa ni mbinu aliyoitumia mtemi.ili kijana wake azidi kuonekanika shujaa.

Wanakijiji walimpongeza mtemi pamoja na kijana wake ,vipofu na vilema wote walimpongeza mtemi .
Sangare akaonekanika alipotea hata kwenye bwawa hakufika.

Watu walitawanyika sangare alirudi nyumbani pamoja na mama yake ,mariamu aliuliza "ni kweli issa ameipata ile dawa au wewe?
Sangare alimwangalia mama yake na kumjibu "ni kweli issa ameipata hio dawa na mimi nilipotea kweli.

Sangare akaamua kuuficha ukweli kabisa ,siku zilizidi kukatika huku issa akizidi kupongezwa kwa kazi aliyoifanya.kile kitendo kilimuuma sana langu ,pamoja na jobwe ambao walishuhudia na macho yao ,vile vile mzee jingi nae ni shuhuda ila hawakuwa na nguvu ya kuongea.

Mzee langu alimwita kijana wake na kuanza kumweleza " jobwe sasa huu wakati wangu wakumnyang'anya huyu mtemi utemi wake ,na njia ya kumnyang'anya kupitia kijana wake na sangare

Twende tukachochee moto kwa issa ili tuwagombanishe tena akishinda sangare basi nakuwa mtemi ambae nitasimamia haki
"Jobwe aliuliza baba unataka kufanyeje?
" mzes langu alijiweka sawa na kuanza kuongea "nataka kufanya hivi " issa najua anapenda sifa na hawezi kushindana ,issa anapenda ushujaa ila ni mwoga ,najua issa anajua kupigana ,na amefanya mashindano ya mapigano  54 yote ameshinda ,amewahi kuua kwenye mpambano ,amevunja watu miguu ,mikono ,issa kweli anauwezo wa kupigana

Sasa nataka wapigane na sangare halafu tuwadhamini kwa mali,mimi natoa mali zangu nusu na mtemi anatoa nusu ,akishinda sangare basi mtemi anakuwa si tajiri tena kwahio hawezi kuongoza wanakijiji na sheria zetu ili uwe mtemi uwe na mali nyingi.
Jobwe alimsikiliza baba yake akamwambia hapana kwa issa ataweza kumuua sangare yule mtaalamu kupambana.

Tukirudi kwa issa alikuwa yupo na minal anamweleza "minal mimi nakupenda nimejitoa maisha yangu kwa ajili yako ,kubali nikuoe ,minal tayari ashamkubali issa alijiandaa amkumbatie ila kwa bahati mbaya eneo ambalo walikuwa wamekaa palikuwa bondeni na kwa upande wa juu palikuwa na jabali,
Gafla jabali likateremka toka juu ,sangare nae alikuwa eneo lile alishuhudia issa wamekumbatiana na minal,

Jiwe linazidi kuteremka kwa chini kuna shimo refu ambao kuna mto umepita chini pia kulia na kushoto pana jabali ambalo linateleza si rahisi kupita 
Na wakizubaa jiwe linawapitia na kuwatupia mtoni
Sangare alipaza sauti " angalieni juu jiwe limeporomoka.,ile wanageuka jiwe hili hapa
Minal alifumba macho huku issa akitafuta njia ya kujiokoa

"Je nini kitaendelea?

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.