Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 21

Story ;SANGARE
BY:mogy shine
No.0621302436
///////////////////////

        SEHEMU YA 21
     Tulipo ishia jana,pale sangare alipo uliza swali " Lile swali la sangare alivyo uliza kuhusu mtoto wa tetere 
Yule mama alidondoka chini huku analia  kwa uchungu
MWENYEJI  wake sangare alisimama kwa hofu na kusema " wewe binadamu nini hiki umefanya huyu malaikia akifa ulimwengu wake pia tunakufa tena wote.
Sangare alipata hofu na kuuliza sasa itakuweje?,sangare ilibidi asogee ile hali ya kwenye ule ulimwengu ,alishangaa watu wote wakikimbia kuelekea kwenye pango flani na kumwacha malaikia mweupe akiwa ameinama kwa uchungu,

Yule mtoto wa tetere alizidi kulia kwa nguvu "ng'aaa! ng'aaa !!ng'aa!!!!
Sangare alibaki kushangaa ,wale watu kwenye ule ulimwengu walichukua mishumaa na kuwasha kisha wakamzingira mama mweupe na kuanza kusali ,
Sali yao ni ya tofati na kusali msikitini ama kanisani
Wao walikuwa wakizomea uweeee!! uweeeee !!uweee !!
Huku mikono wameweka kichwani 
Ni kweli walizomea maratatu ndipo mama mweupe ambae ndio malikia wa huo ulimwengu aliinuka akiwa analia
Jaman mwanangu toka nimzae kila siku yeye analia ,nimejaribu kila uwezo niliokuwa nao lakin mtoto analia,

Mwenyeji wake sangare alimnong'oneza sangare ,yule si mtoto wa tetere kama unavyomwona wewe yule ni mtoto kabisa kama watoto wengine ,ila huwa amemuwekea ulinzi kwa macho ya binadamu wakimwangalia wajue ni tetere 
Sangare kila jambo ambalo anaambiwa kwake alihisi niuongo alimuuliza mwenyeji wake je huu ulimwengu watu wanaishi kwa amani ,je hawa watu walioko humu wametokea wapi?,

Mwenyeji wake sangare ,alimtizama malaikia mweupe kisha akaanza kumjibu sangare maswali aliyouliza " hawa watu unaowaona wazima wanatembea huku na kule ,ni wafu ambao kwa sasa roho zao zimeunganika na mwili ,nawale kule wengii unao waona wamelala ni kwamba walivyokuwa duniani waliuliwa na roho zao zilichukuliwa na kupelekwa mbali na eneo hili ,hivyo miili inaishi ila nafsi zao ziko mbali.

Sikia nikuambie sangare "nafsi yangu ilifugwa kwa mtemi kwenye kiti cha kale na ndio kiti ambao wewe ulikikalia ,wakati umekaa ulirudisha mguu nyuma na kugusa kibuyu kidogo ambacho kilikuwa chini ya kigoda,
Kile kibuyu kilivyodondoka hapo ndipo nilipotoroha na kukufuata wewe kila mahali unaenda
Sababu wewe ndio umenifungua kwenye kifungo ,sangare akauliza " kwanini alikufunga?,huyo mtemi?

Mwenyeji aliendelea kujibu maswali "watu wote unao waona wanazunguka huku ,huko duniani walikuwa waganga ,na uganga wetu ambao tulikuwa tunautumia ulikuwa ni wa aina tofauti ila ulikuwa unamilikiwa na malaikia huyu mweupe.

Hivyo tulikiwa tunatumia ujuzi kupitia huyu malaika ,na nilivyouawa basi mwili wangu ulitupwa kwenye hili bwawa  hivyo nafsi ikafugwa kichawi kwa mtemi ,kwa sasa nashukuru umenisaidia ,ila utanisamehe mimi si rabeka kama ulivyoniona kwenye hilo umbo.
Niliamua kujibadilisha kwenye hilo umbo ili iwe rahisi ya kuleta nafsi yangu kwenye huu ulimwengu .
Ukirudi duniani basi hakikisha maisha ya mwanangu rabeka yanakuwa mikononi mwako ,mtunze kama ndugu zako na umjali kwakila hali kwaheri mimi naondoka.
Yule mwenyeji aliongea vile na kuyeyuka kisha akapotea ,sangare alitamani amwambie nitarudi vipi kwenye dunia niliyotoka ila tayari ashachelewa alijikuta yuko peke yake.

Sangare alifuatwa na malaikia ,alivyomfikia malaikia alinyoosha mkono ndipo watu wake walifika na kumzunguka ,ila mtoto wa tetere bado alikuwa akilia mno.
Malaikia alitabasamu hakika alikuwa mzuri mweupe macho ya kuvutia huku amevaa vito vya thamani aking'ara ng'ara 

"Alianza kuongea " binadamu umekuja kwenye ulimwengu wangu ,nilikupa pumzi ya siku tatu uishi hapa ,kwenye huu ulimwengu nadhani umejionea mengi na sasa limebaki lisaa limoja,nakupa mtihaani ambao ukifanikisha kuufanya na ukafanya watu wangu huku wakafurahia basi nitakuonesha njia ya kurudi  duniani.

Sangare alishangaa imekuwaje aambiwe amekaa siku tatu wakati yeye anaona hata nusu saa haijafika toka aingie kwenye huo ulimwengu,sangare alisema sina namna inabidi nikubaliane kila hali ili niweze kutoka humu.

Malaikia alikuwa amebeba mtoto wake mgongoni wa tetere na aliendelea kumbembeleza tu huku akiendelea kulia,malaikia alimtizama tena sangare,
"Binadamu usiogope hata kidogo jisikie upo huru huu mji hatuui watu ,wote ambao unawaona tayari huko duniani washafariki ,sasa kama mtu ashafariki mara ya kwanza na akapata bahati ya kuishi ulimwengu mwingine basi anakuwa anatii kila amri ili asiuliwe tena ,hakika kifo ni kibaya.

Malaikia alimshusha mtoto wake kisha akampakata mikononi aliomba kija kazi wake amwagie maji usoni mtoto wa tetere ili sangare aweze kumwona vizuri
Kija kazi wake alifanya vile ,ndipo sangare alishangaa kweli alikuwa mtoto mchanga mweupe kama mama yake mwenye nywele ndefu.
malaikia alimwambia sangare" wewe binadamu huyu mtoto wangu toka nimemzaa sasa yapita miaka tisini ,huyu mtoto hakuagi wala hapunguagi jinsi alivyozaliwa hajawa kuongezeka kitu chochote na masaa yote anashindaga analia hasa nyakati za mchana .
Watu wote hawa unaowaona humu washawahi kumshika huyu mtoto lakin bado analia hamna anae weza kumbembeleza anyamaze na asiweze kulia.

Sasa basi nakupa kazi ,mchukue huyu mtoto hakikisha asilie umubembeleze hadi alale na hajawa kubembelezwa na mtu yeyote akalala zaidi yangu ,ukiweza kufanya ivo nakurudisha duniani

Sangare aliona ni mtihani  mgumu Kama watu wote washawahi kumgusa mtoto na hajawahi kunyamaza zaidi ya kulia je yeye ataweza kumtuliza asilie.
Sangare akaona wacha ajaribu bahati yake alimuuliza "malaikia huyu mtoto anaitwa nani?
Malaikia alitabasamu na kusema huyu ni kipepeo mweupe ,mwanangu anaitwa kipepeo .
Sangare alinyoosha mikono kwa ajili Ya kumpokea yule mtoto amubembeleze alale ili aweze kurudi ulimwenguni

Malaikia nae alimkabizi sangare yule mtoto , sangare alivyompokea tu alimtizama machoni akamwambia "
Wewe ni shujaa kipepeo ,unachagua ua zuri na lenye harufu nzuri ,basi hata mkono mzuri lazima utauchagua kutokana na wewe jinsi ulivyo ubwa.
"Kipepeo mimi naitwa sangare ,kutokana na jina langu la kipekee basi nimekuwa mpweke sana ,kipepeo ukilia nami waniliza ,si mimi tu hata  mama yangu duniani atalia sana ,sababu hatoniona  tena.

Kwanini unalia kila siku na kumfanya mama yako akose amani sababu ya wewe kulia ,basi kuanzia leo nitamwambia mama yako asikuite jina hilo la kipepeo sababu kipepeo ni dhaifu.
Kipepeo anawezwa kugeuzwa chakula hata na kinyonga,mjusi hata nyoka ,kuwa kama mimi sangare ni jani gumu ,linaloota kwenye sehemu yeyote.
Na ikitokea maji yamekauka basi jani la sangare huvumilia ukame hadi maji yatakapo rejea
Lala kipepeo na ukiamka utakuwa unaitwa sangare kama lilivyo jina langu.ili usiwe mpweke kama nilivyo mimi.

Malaikia pamoja na watu wake kila mtu alibaki amekodoa macho hawaamini kile wanachokiona hakika ,yule mtoto ambae anaitwa kipepeo mweupe alilala usingizi kitu ambacho hakijawahi kutokea tangu azaliwe .
Mtoto ukimwangalia ni mchanga kabisa ukiambiwa kazaliwa muda ule unaweza ukaamini lakin ,ameishi miaka zaidi ya tisin na bado yuko vile vile.
Ukimwongelesha anasikia ila huwa hajibu kitu chochote.basi sangare alipohakikisha mtoto amelala basi alimrudishia malaikia na kumwambia huyo mtoto wako hatolia tena akiamka mwite sangare ndio jina nililompa mimi ,

Malaikia hakuongea chochote zaidi ya kumchukua na kumpeleka akalale ,huku wale watu wake walifurahi kuona mtoto amelala,
Sangare alioneshwa sehemu ya kukaa kwenye manyoya laini sijui ya nini alikaa kusubiri aruhusiwe kurudi duniani

Malaika alivyorudi baada ya kumlaza mtoto alirudi aliko sangare "alimtizama na kumwambia " umenifurahisha tena si kidogo ila kwenye huu ulimwengu wetu kuna kila utajiri ni kitu gani unataka nikupe  na unahisi kitakuwa kizuri katika maisha yako ,tunamiliki madini,tunamiliki majini  baridi ,hao kazi yako ni kumwagiza kitu chochote unachotaka niambie unataka kipi kati ya hivyo.

Sangare alitikisa kichwa kuashiria hamna hata kimoja anachokita ,sangare alimwambia ,naomba dawa ambayo inatibu ugonjwa mnao usababisha na mngurumo wa jabali linalotema udongo ,vile vile nikatibu vipofu ,viziwi na vilema ili nao wapate furaha ,kama wewe ulivyofurahi baada ya mtoto wako kuweza kulala.
Ha ha ha "malaikia mweupe alicheka na kusema " unahangaikia binadamu siko zote hawanaga shukrani ,nakuambia leo ,taja madini ama jini baridi na si kuhangaikia binadamu wasio kuwa na shukrani utawatibu sawa na watapona wakisha kuona unaendelea wanakuloga ,kibaya zaidi uchawi wote wanao utumia huko duniani lazima upitie kwangu ndio nitume jini liende kwa huyo mtu anae logwa,

Ndio maana huko duniani unaona kuna vichaa ,mara mtu mzima anakufa gafla hio ndio kazi yangu na wanao omba hao majini wawaloge wenzao kwa sababu zisizo za msingi ni binadamu.
Malaikia  alimwambia sangare achague mali anazotaka atapata.

Sangare alijibu "sina kingine mie naomba tu hio dawa ,ya kuwatibu vilema ,vipifu ,viziwi hata wale ambao hawana uwezo wakupata mimba waweze na wasio  weza kuwapa wanawake mimba nao waweze ni hivyo tu.

Malaikia alitabasamu na kusema " hakika wewe ni sangare na mwanangu nitamwita sangare kama jina lako nakupa hio dawa ukawatibu wapate furaha kama nilivyopata mimi najua watakugeuka na kukuloga na uchawi ninao mimi wakikuloga nami naruhusu jini kama kawaida linakufanya unakuwa kichaa ama kukuua kabisa.

Malaikia alichukia sana alifanya kama anachora chini ndioo aridhi ikapasuka akatoa kibuyu chenye maji baridi ,alimwambia sangare haya maji ukawape hao unaotaka kuwatibu unamuwekea sehemu yenye tatizo, asante mtoto wangu amelala kwa maneno yako ,kwa mikono yako hakika wewe ni waajabu
Malaikia akamwambia sangare "haya tizama juu ,alimfunika kitu kama shuka ,
Sangare akajikuta anaibuka kwenye bwawa halafu sehemu aliyoko inakina kirefu mno.
Akaanza kupiga mbizi taratibu kuelekea ukingo ili aweze kurudi nyumbani ,ile anafika ukingoni aliona kundi la vijana wakimnyoshea kidole huku wakisema 
Yule palee ,mwenyewe yule pale
Sangare alivyotizama aliona ni kikundi cha issa tena mkononi ameshika upanga na mgongoni anao upinde

Sangare akakumbuka alivyopataga jiwe la namba sangare alimpiga mshale wa begani ,leo tena amepata dawa ya kumtibu minal ambae issa anampenda sana 
Huyu issa si ataniua leo ,sangare aliwazaa

Je nini kitaendelea?
USISAHAU KU COMMEMT.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.