Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 20

Story;SANGARE
BY;mogy shine
No.0621302436
///////////////////////

       SEHEMU YA 20
      Tulipo ishia jana,wakati sangare anamwambia mtemi amwelekeze ili akachukue dawa "
Mtemi mimi sitaki unipe mali wala kitu chochote naomba unielekeze hio dawa inapatikana wapi,
Kabla hajajibiwa ndipo aliona vijana wamerudi wakiwa hoi,issa ndio kabisa amelegea mwili mzima.
Mtemi kwa mshangao aliuliza mwanangu amefanyeje mbona yuko hoi tumbo limemjaa,
Runde alishusha pumzi "kisha akajibu " mtemi issa alipita kwenye kina kirefu na kuogelea hawezi hivyo amekunywa maji ya kutosha ,mtemi hilo bwawa halifai lina uchawi wa kutisha.

Mtemi aliita walinzi wake kisha wakamchukua issa ili akapatiwe matibabu ,vijana walio enda kwenye hilo bwawa walau kupata hio dawa ili wamtibu minal ilishindikanika.

Sangare alimuuliza runde "kwahio ikawaje mbona mmerudi mmechoka namna hii"?, runde alimtizama sangare na kumwambia ogopa sehemu wanakaa wachawi halafu mnaenda kuchukua dawa ,tumekutana na mauza uza kibao hata siwezi kueleza.
Mtemi alirudi kisha akawaambia vijana wameshidwa kazi hivyo kila mmoja arudi nyumbani kwao ,mtemi aliona njia sahihi ya kumwelekeza sangare aende peke yake hata akifia huko basi amwache mwanae awe huru maana anahisi anamubana.
" sangare hilo bwawa lipo lain chungu we tembea ulizia lain chungu utaoneshwa ni sehemu ambayo ipo wazi kuna mbuga kubwa ambako hilo bwawa liko kati kati,mtemi alimweleza kila kitu sangare na kumwambia aende huko.

Sangare alivyoelezwa na mtemi alitoka na kurudi nyumbani alijiandaa  vilivyo kisha akaanza safari ,wakati anatoka tu kwao rabeka alimfuata huku ameshikilia chombo kidogo huku amekifunga kitambaa cha kaniki.
Sangare alimuuliza rabeka unaenda wapi mbona unaonekanika mnyonge?,
Rabeka alimtizama sangare na kumwambia nimesikia kila kitu ,umeenda kwa mtemi kisha amekupa maelezo ,na sasa umejiandaa kwenda kutafuta dawa kwa ajili ya kumtibu minal si ndio?
Sangare alijibu ndio naenda kuitafuta hio dawa "rabeka alimtizama sana sangare na kumwambia " sangare nina ombi moja uwe kaka yangu tu popote utakapo enda tuendo wote labda subiri nikusimulie kidogo historia ya maisha yangu.
Baba yangu alikuwa mgaanga mkuu kwenye hiki kijiji na alikuwa anakaa kwenye nyumba ya mtemi,
Baba yangu alikuwa mganga mzuri akikuagulia ama kukutibu basi unapona ,lakin kutokana na uwezo aliokuwa nao baba yangu vijiji vya jirani vilimtaka baba yangu akawatibu wanakijiji wao ,ndipo mtemi alikataa ,

Ilitokea vita ya watemi wakimgombea baba yangu ,hadi aliuliwa ,lakin baba yangu kabla hajafa aliniachia hichi kifaa ambacho ninacho kwenye mkono.

Sangare aliuliza kwahio hicho kifaa kina kazi gani?,rabeka alishusha pumzi na kumwambia sangare ,hichi kifaa ndio nafsi ya baba yangu na alivyouliwa mwili wake ulitupwa kwenye hilo bwawa ambalo unataka kwenda.
Nataka niende na wewe nikamwone baba yangu kwa mara ya mwisho ,maana hata mama yangu alipotelega kwenye msitu ambao upo karibu na jabali ambalo lilinguruma na kusababisha minal kuwa kiziwi.

Sangare alichoka alimuuliza rabeka kwahio unaishi na nani?,
"Naishi peke yangu muda mwingi nashinda na nafsi ya baba ,bado ipo hai kuna muda mwingine huwa naongea na hii nafsi na inanijibu kila kitu nikihitaji.

Sangare alichoka ,alimwambia rabeka hebu nione hio nafsi ya mtu ambae alishakufa lakin roho yake bado ipo hai,ni kibuyu kidogo mno rabeka alikafungua ndipo sangare alichungulia aliona kitu kama moshi ukizunguka ndani ya kibuyu kile.
Rabeka alifunga kisha wakaanza safari ya kuelekea  laini chungu likiko hilo bwawa ,

Njiani rabeka aliongea vitu vingi na kumfanya ajisikie raha ,alifurahi sana sangare kukubali kuwa kaka yake,
Mida ya jioni ndipo  walifika kwenye lile bwawa walishangaa kuona bwawa zuri lenye maji masafi kaupepo kazuri kakivuma kwenye lile bwawa.

Sangare alimuuliza rabeka unajua kuogelea?,maana nataka niende kati kati ya hili bwawa nahisi ndio kule ambako kuna nguzo ambae mtoto wa tetere huwa anawekwa hapo ,pia nimeambiwa huyo mtoto wa tetere analia kama mtoto kabisa binadamu wa kweli 
Pia anabembelezwa hadi alale ni kweli? " sangare aliuliza "rabeka alisema " nikweli kipindi baba yangu yuko hai alishawahi kunisimulia ,
Sangare alimwambia rabeka siwezi kukuacha kwenye eneo hili nimesikia lina uchawi mno ,hivyo tunaingia kwenye maji mimi nitapiga mbizi halafu wewe utapanda mgongoni tutaanza safari ya kuingia kati kati ya bwawa ili tukachukue hio dawa.
Ha ha rabeka alicheka na kumuuliza sangare utaweza kuogelea huku umenibeba mimi?
Lini wewe umejifunza kuogelea ,sangare alitabasamu na kumwambia "rabeka mimi nimekulia dar es salamu ,kila mwisho wa wiki tulikuwa tunaenda baharini kujifunza kuogelea ,sasa bahari inamawimbi makubwa na nilikuwa naogelea umbali mrefu sebuse haka kabwawa nauwezo wa kukazunguka.

Rabeka alikubali kuwa atapanda mgongoni wakifika kwenye kina kirefu ,walianza kutembea kwa miguu huku sangare amemshika rabeka mkono walitembea umbali mtefu ndipo walifika kwenye kina kirefu ,
Mtoto wa kike akapanda kwenye mgongo wa sangare wakati huo nguo zote zimeloa.,
Rabeka mtoto wa kijijin hajawahi kuvaa brazia basi maziwa yake yaliyosimama yaligusa mgongo wa sangare ,mwanaume yupo kwenye maji alianza kuhisi hali flani.
Sangare alipiga mbizi kweli alivyokaribia ile nguzo iliyotengenezwa mikono mitatu kati kati palikuwa na kata iliyotengenezwa kwa ngozi ya chui.

Sangare akiwa eneo lile pamoja na rabeka alishangaa anafika sehemu nyingine yenye kina kifupi ndipo sangare alishangaa na kugeuka nyuma sehemu alikopita palikuwa na kina kirefu kakin karibu na hio nguzo ambayo ipo kati kati ya bwawa ndipo maji yalikuwa kwenye magoti

Sangare alimshusha rabeka ili watembee na kusogea vilivyo kwenye ile nguzo ,gafla walisikia mtoto mchanga akilia ng'aa ng'aaa!!!! lakin kila wakitizama hawaoni mtu hata mmoja ,

Mara wakasikia mbuzi wakilia meee ,mara mtu anapasua kuni ,ni kweli wanasikia vishindo watu kabisa wakitembea kama vile hawapo kwenye maji ,wao wakitizama hawaoni

Rabeka alianza kupata wasi wasi na kumshikilia mkono sangare,shiiii nyamaza mtotoo lala nyamaza mtoto lalaa walisikia sauti lain ya mwanamke akimbembeleza mtoto alale lakin kila wakitizama kokote hawaoni mtu,

Sangare alimwambia rabeka hapa hatuna muda wa kupoteza twende kwenye hio nguzo ,wakiwa wanaeleke walisikia sauti za akina mama wanacheka mno,lakin wakitizama hawaoni mtu.
Sangare alisogea na  kunyoosha mkono  ili kuishika kata ,alishangaa mkono haufiki na ile nguzo imesogea umbali mrefu.
Sangare alimwambia rabeka hebu simama hapa ngoja niende mimi ,sangare alishangaa jinsi anavyopiga hatua ndipo anakutana na tope ndani ya maji alipiga hatua kadhaa alishangaa anazidi kuzama kwenye kina kirefu ,sangare akataka aelee juu ili apige mbizi asizame miguu ilinasia kwenye tope ,
Alianza kuzama taratibu ,sangare alimwambia "rabeka mimi nahisi nazama ila wewe simama hapo usisogeze hata mguu mimi kaka yako nitakuwa salama.

Rabeka alianza kuita sangareee ,sangare rudi usizame ,lakin maji tayari yashamfikia sangare shingoni ,rabeka nae alitaka akimbie akamwokoe sangare miguu yake nae imenasa hata kunyanyua mguu hawezi.
Akimtizama sangare maji yamemfika mdomoni sangare alianza kunywa maji  taratibu hatimae akazama mazima,sangare alivyozama kichwa alikumbuka rabeka alimpa kibuyu chenye nafsi ya baba yake ,aliamua aifungue ile nafsi ili kama mwili wa baba yake bado upo kwenye hili bwawa aunganishe mwili na nafsi ili aweze kuokolewa,

Kweli sangare alifungua kile kibuyu mara moja alishangaa kuona moshi unafuka tu kutoka mashariki na wala hayupo tena kwenye maji ,sangare alishangaa yupo eneo la nchi kavu kabisa hamna cha bwawa waka kitu chochote,

Alizunguka kumtafuta rabeka wala haonekaniki,
Sangare aligusa tumbo lake mbona nilikuwa nakunywa maji kwenye bwawa sasa huku nipo wapi?,

Sangare hakuzubaa alianza kutembea kwenye huo ulimwengu ambao ametokea ,sangare alihisi labda yupo kwenye ndoto akatikisa kichwa akajikuta hayuko kwenyendoto,
Sangare aliita "rabeka upo wapi?,mara akasikia rabeka anaitika lakin akitizama sauti inatokea kwe juu ,
Sangare akitizama kwa juu anaona anga kama tunavyoliona sisi

Akajaribu kuita tena rabeka ?,masikin. Rabeka alikuwa anaitika lakini hawaonani ,tukirudi kwa rabeka yeye bado amesimama kwenye kwenye maji ya bwawani  pia jinsi sangare anaita sauti inasikika eneo lile ambae alishuhudia akizama.
Rabeka alianza kulia huku. Akiita sangaree umeenda wapiii

Sangare kwenye ulimwengu ambao aliko anamsikia rabeka ila hamwoni ,sangare alipiga hatua ndipo amekutana na eneo miili ya watu wengi wamelala ,ki ukweli watu walikuwa ni wengi mno ,lakin baba mmoja aliinuka na kusema " kijana asante kwa kunifufua ,kwenye huu ukimwengu mimi nitakuwa mwenyeji wako ,nifuate,

Sangare alianza kutetemeka mtu alikuwa anaonekanika kama ana dege dege jinsi anavyoongea ni sawa na mtu mwenye baridi kali,sangare hakuwa na namna ndipo alimfuata alipelekwa eneo  ambalo watu walikuwa wakipika vyakuka huku mama mweupe alikuwa anabembeleza mtoto alale.
Hapo ndipo sangare akachoka ,jinsi sauti alivyokuwa akizisikia mwanzo mtu akibembeleza mtoto ,kwasasa anamwona kwa macho yake,jinsi alivyokuwa akisikia mtu akipasua kuni basia alishuhudia kwa  macho yake.
Tukirudi kwa rabeka yeye bado alikuwa yupo kwenye bwawa alikuwa akisikia watu wakipasua kuni ila hawaoni.

Sangare aliuliza wewe ni nani na kwanini niwe mgeni wako?,yule mtu alikaa chini kisha akajikung'uta vumbi alijinyoosha vizuri 
Akasema "nimelala mno miaka saba sasa nilikuwa nimelala ,hatimae nafsi yangu umeniletea ,mimi ndio baba rabeka na yule mama unae mwona pale anachochea kuni ni mke wangu,
Ni story ndefu wotee unao waona kwenye ulimwengu huu ni wafu

Isipokuwa huyu mama mweupe anae bembeleza mtoto yeye ndio mwenye mji huu.mama mweupe alichukua chungu cheupe chenye uji mlaini aliuchukua kisha akaenda mahali aliko sangare 

Alichota uji kwa mkono wake na kumrushia sangare usoni alitamka maneno matatu,upole ,utajiri na ushindi alivyomaliza alirudi kubembeleza mtoto wake.wala hakumsalimia sangare

Sangare alimuuliza baba rabeka kama kweli wewe ni baba rabeka mbona mimi nimekuja peke yangu narabeka nimemwacha kwenye bwawa.

Yule baba alisema uliyekuja nae si rabeka bali ilikuwa ni nafsi yangu umenitoa kwa mtemi alinifunga nafsi yangu kwenye kiti,
Na wewe ukivyoenda kumtembelea ili akueleze dawa ya kuponya ugonjwa wa masikio kutosikia ,kwa bahati mbaya alijisahau na kukuambia ukalie kile kiti.
Mtemi aliniua mimi na kuja kuutupa mwili wangu kwenye bwawa lakini leli si bwawa kama binadamu wanavyoliona hilo ni wingu  ambalo mama huyu mweupe ndio kaliweka ,kwa ajili ya kuzuia miale ya jua ,

Huyu mama mweupe ndio malikia wa huu ulimwengu na kama umesikia mngurumo wa jabali hapo ni dirisha la kuwapa taarifa kuwa mwaka ni mzuri watu walime na watapata chakula.
Sangare akimtizama huyo mama mweupe anaona yuko bize anabembeleza mtoto wa tetere cha ajabu lile tetere lina lia kama mtoto.
Sangare aliuliza "kwanini analea mtoto wa tetere?,lile swali alivyouliza vile ,mama mweupe mithili ya mzungu ila weupe wake umezidi kama mtu asiyekuwa na damu
Lile swali la sangare alivyo uliza kuhusu mtoto wa tetere 
Yule mama alidondoka chini huku analia  kwa uchungu
MWENYEJI  wake sangare alisimama kwa hofu na kusema " wewe binadamu nini hiki umefanya huyu malaikia akifa ulimwengu wake pia tunakufa tena wote.

JE NINI KITAENDELEA?

SHARE KWA WINGI ILI STORY NA
COMMENT

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.