Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 19

Story ;SANGARE
BY;mogy shine
No.0621302436
////////////////////////

     SEHEMU YA 19
       Tulipo ishia jana,Mariamu kwa hofu aliinuka na kusema yuko wapi,mungu wangu tayari masikio yake yashaharibika ule mngurumo ni hatari sana,ile mariamu anachungulia nje alishangaa minal anapiga ukunga aiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!kisha akadondoka na kushika masikio yake ,sangare na mama yake wakawahi nje kumwangalia minal ,ndipo walijionea masikio ya minal yakitoa damu.
Sangare alimuuliza mama yake kwahio tunamsaidiaje?
Mariamu alijibu angekuwa anatoka usaha tungemtafutia dawa ,ila anatoka damu basi hatosikia tena

Sangare alimwinua minal huku akiita ,minal minal!!!!,minal akawa anamwangalia tu sangare hata hasikii chochote ,masikio ndio yakazidi kutokwa na damu,
Sangare alimwangali mama yake na kumuuliza tuna fanyaje?,mama alimwambia "sangare huyu tayari ashakuwa kiziwi hamna dawa tena ya kuweza kutibu huu ugonjwa ,na masikio yake baada ya nusuu saa yataacha kutoa damu ,

Ila kila mwezi mchanga ukitokeza yatakuwa yanatoa damu ,yaani ni sawa na mwanamke anaingia kwenye siku zake  za hedhi ndio minal atakuwa hivyo.

Kila mwezi mchanga ukitoka na yeye masikio yake yalizima yatoe damu.sangare alichoka na kumuuliza " mama kwanini mtu akija kwenye hichi kijiji hapewi sheria ambazo ni hatarishi kwa afya ya mtu ,ona binti wa watu amekuwa kiziwi na atateseka na huu ugonjwa maisha yake yote.

Sangare akiwa amemshikilia minal alianza kutokwa na machozi aliumia sana ,minal kuwa katika hali ile,minal akimwangalia sangare anashangaa analia "ila  sangare akizungumza pamoja na mama yake hasikii hata kidogo ,
We sangare unalia nini!!!!!?
Minal aliuliza kwa nguvu ,lakin sangare akimjibu hasikii chochote.

Tukirudi upande wa issa baada ya kunywa pombe alitulia akiwa amekaa alikumbuka mngurumo wa jabali ,akauliza " baba jabali limenguruma leo ,inamana minal ashapewa taarifa kwamba jabali likinguruma alale chini na kuziba masikio?

Mtemi alimtizama mwanae na kumwambia hilo swali unaniuliza mimi kwani nakaa nae kamuulize bibi yake ,issa hakutulia maana anampenda sana minal alikimbia hadi kwa bibi yake minal alifika alimkuta bibi analia baada ya sangare kumpeleka minal
Mjukuu wangu nisamehe sikukueleza mapema kuhusu mngurumo wa jabali ,ona umekuwa kiziwi mimi bibi yako nimezeeka hivyo nilisahau pia ni miaka mitatu imepita na hatujasikia huu mngurumo nisamehe.

Minal akawa anawaangalia ila hasikii chochote.issa kufika hakuuliza alimtandika sangare ngumi ya shavuni puuuu!,mpumbavu wewe nishakuonya kaa mbali na minal wangu ,kwanini wewe hujadhuurika minal kadhuurika peke yake?,

Kwa nini ?nakuuliza wewe sangare akampiga ngumi nyingine ya shavuni sangare akapepesuka na hakumwambia kitu chochote,
Sangare akamwangalia ,minal jinsi anavyowaangalia hasikii masikin ,sangare machozi yalimtoka 

Kitendo cha sangare kutokwa na machozi issa hakuelewa sababu ya sangare kutokwa na machozi yeye alielewa sangare ni mwoga wa ngumi ,amelia baada ya kumpiga,
Hapo issa ndio aliona udhaifu wa sangare ni kumtwanga ngumi ,basi alimfuata na kuanza kumpiga ngumi nyingi kila mahali ,sangare alizidiwa uwezo na issa alimdondosha chini ,issa alimkalia sangare tumbo huku hukusangare kalalachali alianza kumpiga kwa nguvu .
Nakuua wewe ,kwanini minal awe kiziwi wewe uwe mzima sangare nakuua mimi hakika isaa alimpiga sangare ngumi za kutosha ,sangare akawa ametapakaa tu damu.

Bibi yake minal aliwahi na kusema "usimuue mtoto wa watu mimi ndio mwenye makosa sikumweleza mjukuu wangu mapema kuhusu mngurumo wa jabali tafadhali usimpige ,msamehe kijana wa watu.

Issa aliinuka na kumshika mkono minal kisha akamwambia nifuate tukatafute tiba ,nishakuambia kaa mbali na huyu sangare anakuchukia ,minal akawa hasikii ,sangare alienda nae hadi kwao na kumpa daftari na kalamu kwakuwa hasikii ukitaka kumwambia jambo ,basi unamwandikia kwenye daftari halafu anaelewa nae anakuandikia jibu.

Hayo ndio yakawa maisha ya minal ,kijiji kizima kilipata habari kuwa minal ameharibika masikio hivyo hatosikia tena.kama ilivyo desturi ya kijiji waliitisha mkutano ,kila raia alijitokeza ,
Mtemi alisimama na kuanza kuongea na watu wake,

Mwaka huu ni mwaka wa neema nadhani ishara mshazipata ,jabali letu limenguruma kwa nguvu na kutema tope jeusi likiwa linaashiria huu ni mwaka mzuri kwa kilimo.
Wanakijiji wangu natoa tamko kila mwanakijiji aamdae mashamba ya kutosha kwa ajili ya kilimo mmenisikia?
 
Wanakijiji waliitikia ndiooo!,mtemi aliendelea kuongea mkwe wangu minal ambae kijana wangu anataka kumuoa kwa bahati mbaya hakupewa taarifa mapema kwamba akisikia mngurumo wa namna ile alale chini hakufanikiwa hivyo masikio yake yameharibika  dawa inaweza kupatikana ila sitaki kuwatoa wanakijiji wangu mhanga kwa ajili ya mtu mmoja hivyo atabaki hivi hivi kiziwi maisha yake yote.

Kwa leo nifunge kikao niwatakie maandalizi mema ya mashamba,mvua itaanza kunyesha muda si mrefu ,
Wanakijiji walitawanyika ,na kurud majumbani
Issa alimfuata baba yake na kumuuliza " dawa ya kutibu masikio ya minal yaweze kusikia vizuri inapatikana wapi niambie hata iko umbali gani nikaitfute.
Mtemi alicheka na kumwambia issa mwanangu ,tambua wewe ni mrithi wa kiti changu cha utemi siwezi kukuruhusu uende huko utaweza kupoteza maisha kabisaa na si utani yaani heri ukapambane na chui najua utashinda na si kupambana na nguvu  ya mapenzi utaweza kufa wewe.
Issa alimsogelea baba yake na kumwomba amweleze ni wapi anaweza kuipata hio dawa.

Mtemi alitulia na kusema ,mwanangu najua unataka kumsaidia minal ila uwezo wako ni mdogo ila ngoja niwaite vijana wote wa kijiji niwaeleze ni wapi dawa inapatikana atakae weza kuipata basi nitampatia zawadi  nzuri sana.nakupa kazi waite vijana wote wa kijijin kisha niwaambie.

Issa alivyoambiwa vile alianza kazi aliwakusanya vijana wote kijijin wenye nguvu ila hakumpa taarifa sangare sababu anajua sangare kila kitu huwa mshindi na ashakanywa na baba yake asithubutu kushindana na ukoo wa itambu haujawahi kushidwa hata siku moja.

Sangare akiwa kwa mama yake wanasimuliana jinsi walivyoishi pasina kuonana basi kwa mtemi vijana walikalishwa na kuanza kuelezewa "jamani dawa ya kumponya minal ipo kijiji cha LAINI CHUNGU,kuna bwawa moja lipo kati kati ya mbuga ,kwenye hilo bwawa kati kati kuna nguzo ipo kwenye maji ,na hio nguzo kuna mtoto wa tetere la boga ,yale maboga ya kienyeji ,hivyo huwekwa hapo kwa ajili ya kuota jua.

Kwenye yule mtoto wa tetere ametengenezewa kata ambayo  inatunza maji,
Si maji ya kawaida yule mtotowa tetere ni waajabu huwa anakojoa na mkojo wake unahifadhiwa kwenye ile kata .

Sasa kwenye hilo bwawa kuna sehemu lina maji ya chumvi kuna sehemu maji ya moto na sehemu maji baridiii.pia kunalotope ukikanyaga unazama chini na unafia kwenye maji ,vile vile kunao watu ambao wanalea yule mtoto wa tetere ,ila hao watu mara nyingi huwa hawaonekaniki,
Lile bwawa unaweza ukagusa maji ukiyatizama huoni tena bwawa inakuwa mbuga tu .kuna muda mwingine unaliona hilo bwawa.kuna maajabu mengi sana ya kutisha ,kwa atakae weza na akapata hayo maji nitampatia mali nyingi sana.na atakuwa shujaa wa kijiji.
Mtemi alimaliza kuwapa historia ya hilo bwawa kisha akawaambia waende,vijana walivyosikia wanapata mali basi walianza safari kuelekea kijiji cha laini chungu ambako linapatikana hilo bwawa.

Lakin sangare hakupata taarifa kabisa ,akiwa anazunguka kijijin aliona baadhi ya watu wanamsema ,ooh sangare kaogopa kwenda bwawa la lain chungu kwa ajili ya kuchukua dawa ya kumtibu minal.
Sangare aliondoka hadi kwa minal kwa ajili ya kumsalimia ,ndipo alifika na kukuta minal amelala chini ya kivuli sangare alitizama pembeni aliona daftari alilichukua na kupekua alikuta maongezi kwa njia ya maandiko kati yake na issa.
Akiwa anafunua ndipo alikutana na ujumbe kwenye karatasi ,sangare aliufungua na kuanza kuusoma

 "Minal wangu najitoa maisha yangu sadaka kwa ajili yako niombee naenda bwawa la lain chungu kwa ajili ya kukuletea dawa ya kuponya masikio yako ,nakupenda mimi nakuahidi nitaipata hio dawa."

Sangare alivyosoma ndipo akagundua vijana wote hawapo kijijin inamana wameenda huku kwenye bwawa la lain chungu,kama wameenda huko mbona mimi sijapata taarifa.
Sangare aliwaza na kurudisha lile daftari la minal kisha akaondoka kwenda kwa mzee jingi
Alifika na kumkuta akitengeneza jembe,
Shikamoo babu sangare alisalimia ,
Marihabaa "sangare siku hizi huji kunitembelea au sababu umempata mama yako?,
Hapana babu sio hivyo muda si mrefu tutahamia wote na mama kwenye nyumba yako maana wewe kwangu ni wathamani.
Ha ha ha mzee jingi alicheka na kusema itapendeza 
Ehe niambie leo umekuja na ujio gani?

Sangare alimtizama babu na kumuuliza " imekuwaje vijana wote wameenda sijui kijiji cha lain chungu kwa ajili ya kutafuta dawa ya kumponya minal mbona mimi sijapata taarifa?

Haaa!! Mzee jingi alishangaa kisha akaweka pemben jembe ambalo analitengeneza kisha akamjibu "wew si umemwambia issa huendi huko kutafuta dawaa kwa mtu usiyempenda ,
Issa alisema kabisa amekuambia umekataa ,
Sangare alishangaa " babu mie sijakutana na issa toka majuzi tulivyokutana kwa bibi yake minal akanidunda mangumi mie sijakutana tena.
Mzee alisema ndio hivyo wameenda huko kutafuta hio dawa tuwasubiri wakipata basi mtoto wawatu aweze kupona na kusikia ila kwasasaa wewe usiende 
Sangare alimwambia sawa siendi nawasubiri warudi naimani wataipata hio dawa.

Sangare waliagana na babu kisha  akarudi nyumbani  ,zilipita siku  mbili ndipo vijana wote walioenda kutafuta dawa walirudi wakiwa hoi,wengine wamekuwa vipofu wengine wanachechemea ,issa nae alirudi amebebwa juu kwa juu amelegea mwili mzima.
Wakati wanarudi walimkuta sangare yupo kwa mtemi anaomba apewe maelezo na yeye ili aweze kwenda kutafuta hio dawa.

Mtemi mimi sitaki unipe mali wala kitu chochote naomba unielekeze hio dawa inapatikana wapi,
Kabla hajajibiwa ndipo aliona vijana wamerudi wakiwa hoi,issa ndio kabisa amelegea mwili mzima.
Mtemi kwa mshangao aliuliza mwanangu amefanyeje mbona yuko hoi tumbo limemjaa,
Runde alishusha pumzi "kisha akajibu " mtemi issa alipita kwenye kina kitefu na kuogelea hawezi hivyo amekunywa maji ya kutosha ,mtemi hilo bwawa halifai lina uchawi wa kutisha
Ona mwanangu ana hali mbaya mwiteni mganga upesi aokoe maisha ya mwanangu
Mtemi aliinuka akiwa na wasiwasi ,huku sangare akimtupia jicho issa jinsi alivyodebweda baada ya kunywa maji vya kutosha.

JE NINI KITAENDELEA?

SHARE KWA WINGI
COMMENT CHOCHOTE.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.