Notification texts go here Contact Us Buy Now!

SANGARE SEHEMU YA 18

Story ;SANGARE
BY,mogy shine
No.0621302436
////////////////////////

         SEHEMU YA 18
    Tulipo ishia jana,Kila mtu alishangaa ,mariamu gafla aliacha kulia ,mzee jingi akainuka na kusema nimacho yangu ama naota ,minal alitabasamu akasema ooh sangare
MTEMI ,kwa mshangao nae akauliza ni mwenyewe sangare ama tuko ndotoni ,maana haijawahi kutokea mtu kupambana na mbwa mwitu na akashinda
SONGA NAYO

Wanakijiji wote walibaki kimya wengine walianza kunong'ona huyu alijificha hajapambana na mbwa mwitu ,kila mmoja alizungumza lake ,wakati huo sangare anawaangalia tu huku akila sasati zake,

Walinzi walifungua geti ndipo sanagre alitoka na kuungana na wanakijiji ndipo alishangaa kumwona minal akimkimbilia.

Sangare akiwa ameshangaa minal alifika na kumkumbatia huku akilia kwa furaha ,wewe ni shujaa ,hakika sangare wewe ni shujaa na leo kila mtu amegundua wewe ni shujaa ,nilivyokuona kwa mara ya kwanza  nilikudharau na kukuona wewe ni kichaa ,
Hilo hukujali ,ulijali utu wangu na kunisaidia kila nilipokubwa na baya ,sangare wewe ni wa muhimu kwangu ,hebu kumbuka siku tulikuwa tumepanda basi wote ,nilivyopitiwa na usingizi nilijilaza kwenye bega lako hakika nilisikia raha japo sikukuambia ila ukweli nilikuwa nao moyoni,
Sangare kumbuka nilivyokuwa naumwa na tumbo na kujisikia kichefu chefu ulinitibu kwa kunichoma na sindano
Baki na mimi sangaree.
Ni maneno aliyoongea minal mbele ya wanakijiji na kufanya kila mtu ashangae minal aliongea kwa hisia huku akidondosha chozi la furaha ,

Issa aliona wivu aliwahi na kumvuta minal na kumuuliza "unafanya nini na huyu mpumbavu muoga wa mapambano ,mbona amejificha na hajapambana na mbwa mwitu ,angekuwa kidume kweli angepambana na umbwa mwitu aone jinsi wanavyomgeuza kitoea ,
Minal njoo kwangu mimi ndio shujaa nimewaua chui wawili kwa mishale.

Sangare hakuongea chochote aliangalia minal akichukuliwa kwa nguvu ,sangare alitizama upande wa pili alimwona mariamu amehamaki yuko kama amepigwa na butwaa ,haamini kabisa kama sangare ametoka mzima,
Sangare alimfuata mariamu akamwinua na kumwambia " asante hatimae nimeshinda mpambano ,mariamu alishidwa kujizuia alimkumbatia na kuanza kulia ,sangare wewe ni mwanangu ,sangare wewe ni mwanangu lakin mimi mama yako nilishidwa kukulea hatimae leo nimegundua wewe ni mwanangu niliachaga alama kwenye bega lako la kushoto na leo nimeiona ,
Nisamehe mwanangu ,niambie kama ulilelewa na hadija ama na bibi cha upele maana hao ndio walikuwa wapangaji wenzangu
Mariamu akiwa analia huku anapiga magoti ,aliuliza tena ,niambie ni yupi alikulea kati ya hadija au bibi chaupele,

Kitendo cha mariamu kutaja jina la bibi chaupele ndipo sangare alikodoa macho ,haamini kabisa ni kweli amesikia kweli ama anaota,bibi chaupele ndio amenilea je wewe ni mama yangu?
Sangare aliuliza huku akimwinua mariamu chini,sangare alibaki amekodoa macho mariamu alijibu ndio wewe ndio mwanangu ,na mimi si mgumba kama wanavyonisema hapa kijijin,

Kweli mimi natoka ukoo wa itambu ,huwa wanazaa mtoto mmoja tu ,mimi nilizaliwa peke yangu ,baba yangu nae alizaliwa peke yake tu ,hata wewe nimekuzaa peke yako tu kwenye ukoo wetu huwa tunazaa mtoto mmoja.
Pale ndipo wanakijiji waliamini ,kweli ukoo wa itambu huwa wanazaa mtoto mmoja kisha kizazi kinajifunga ,hawawezagi kuzaa mwingine,

Wanakijiji waliamini kweli mariamu si mgumba kama walivyodhani ,mariamu alisogea tena karibu na rabeka ambae ni rafiki yake ,alimwambia 
"Unakumbuka siku nilivyowakuta mkimshangaa sangare akimsaidia mariamu kujenga nyumba yake ,ee niliwaambia sangare siku zote hufanya kitu kwa maana flani ,leo hii amethibitisha kuwa mariamu ni mama yake.

Asikuambie mtu kumpata mama ambae hujamwona.zaidi ya miaka kumi na tisa ,basi walikumbatiana mama na mtoto ,sangare akiwa analia alimwambia " mama nimekua sasa haina haja ya kuomba msamaha ila usinikimbie tena.

Mara mtemi alipuliza filimbi piiii ,kila raia alikaa vizuri kwa ajili ya kumsikiliza mtemi anataka kusema nini,mtemi alisogea kwa sangare na kumkagua kama  ameshindana na hajapata jeraha ,
Kweli alimkagua na kukuta mzima kabisa hajaguswa hata na nyoya la mbwa mwitu.

Mtemi kwa sauti yake nzito aliuliza umepambana kweli na mbwa mwitu?,maana kwenye historia ya kijiji hajawahi kutokea mtu wakuweza kupita eneo la mbwa mwitu na akapita salama,
Sangare alitema kwanza tetere la sasati kisha akatabasamu ,

Aliwatazama wanakijiji ,kisha akamwambia mtemi ,naomba uongozi wako pamoja na walinzi wakakague ni kweli nimepambana na mbwa mwitu ama sijapambana ,
Ikitokea sijapambana basi kwa ridhaa yangu naruhusu unitenganishe kichwa na kiwili wili mbele ya umati.

Ha ha ha mtemi alicheka na kusema walinzi wamfunge sangare minyororo ili wakakague kwanza kama kweli amepambana na mbwa mwitu,walinzi walifanya kama walivyoambiwa na mtemi,kisha mtemi alituma vijana kumi na mbili waingie eneo hilo walete mbwa mwitu kama wameuliwa.

Kweli vijana waliingia kwa wasi wasi maana wanajua eneo lile ni hatari lakin walivyofika kati kati walikuta mbwa mwitu wote wameuliwa ,
Kwanza walishangaa na kujiuliza huyu sangare ni mtu ama jini ,amewezaje kuwaua mbwa mwitu kirahisi namna hii.

Basi waliwabeba wale mbwa mwitu na kuwapeleka nje ili mtemi akashuhudia ,hapo ndipo issa na baba yake walikodoa macho baada ya kushuhudia mbwa mwitu kumi na mbili wote wameuliwa .
Mtemi akawa haamini alimtizama sangare mara mbili mbili ,ndipo mzee jingi akiwa na tabasamu mrua alisogea kwa mtemi na kumwambia jambo "mtemi huyu kijana ni mjasiri sana nilimkataza kata kata asipambane lakin alikataa na kusema ,kwenye mafanikio usiogope kupambana ,
Kweli nimeamini sangare ni shujaa amewaua mbwa mwitu wote  na hajapata hata jeraha 

Sasa sangare ni shujaa amemshinda issa amekwaruliwa mgongoni na kucha za chui.issa alichukia na kuona aibu maana alijitapa yeye ni shujaa lakin sangare amemzidi issa aliamua kuondoka na kurudi nyumbani.

Mtemi hakuongea kitu chochote aliamrisha walinzi wamfungulie sangare minyororo na ndio ameshinda ,japo yeye alisema atapambana  lakini si kwa lengo la kutaka kumuoa minal kama mtemi alivyosema.
Watu walianza kutawanyika na minal hakulazimishwa kuolewa na issa tena ,.aana issa alichukia na kuzira baada ya sangare kushinda
Sangare alimshika mkono mama yake kwa sasa ashagundua ni mama yake kisha wote waliondoka kurudi nyumbani ,minal aliwafuata taratibu kwa nyuma huku akianza kuonesha ukaribu na sangare.

Mtemi alirudi nyumbani alikuta mwanae anakunywa mtukuru kwa hasira baada ya kushidwa mpambano ,mtemi alimtizama mwanae na kumwambia " unahisi ukinywa pombe nyingi ndio utapata njia ya kumzidi akili sangare?
Issa baada ya kuulizwa vile na baba yake alimtizama na kumwambia "baba ni kitu gani unataka kuniambia " wewe si umesema hizo ni mbinu zako za kumpeleka sangare kupambana na mbwa mwitu ili akafie huko ,haya sasa ametoka salama na wanakijiji wanajua sangare ni shujaa kuanzia sasa.
Baba mfukuze tu huyu sangare kijijin ananifanya nachanganyikiwa mimi ,issa aliongea na kubugia kibuyu cha pombe.

Mtemi alitizama juu na kusema "kumfukuza sangare ni kazi ngumu kwa sasa ,tambua ashampata mama yake mariamu kwa hio kwa sasa anayohaki kuishi kwenye hiki kijiji,vile vile jobwe ambae baba yake anayomali nyingi hapa kijijini pia anamkingia kifua sana sangare endapo nitamuua ama kumfukuza basi huu utemi wangu utapinduliwa.
Kinacho nichanganya hata mimi " kama kweli sangare ni mtoto wa mariamu basi atakuwa anatoka ukoo wa ITAMBU.

Nadhani unaufahamu huu ukoo huwa unazaa mtoto mmoja mmoja na haujawahi kushidwa kwenye mpambano wa namna yeyote ,hivyo mwanangu kuwa makini usijaribu tena kuingia mpambano na sangare unaweza kupoteza maisha ,maana ukoo wa itambu haujawahi kufeli mpambano wa namna moja ama nyingine.
Ha ha ha issa alicheka kwa kilevi kilevi ,kisha akaita "baba hata atoke ukoo wa nani ila nakuapia hawezi akaninyang'anya minal wangu ,lazima awe wangu lazima nimuoe mimi.
Mtemi aliondoka na kumwambia " kama sangare hatoonesha nia ya kuwa  na nia ya kumuoa minal basi atakuwa wa kwako 
Ila ukoo wa itambu wakitakaga kitu flani lazima wakipate.

Tambua miaka 50 iliyoopita ukoo wa itambu ndio ulikuwa unaongoza kwa mali nyingi sana ,wakifuatiwa na ukoo wa jobwe  ambao nao ulikuwa na mali nyingi.
Si unamwona mariamu wanamcheka kila siku mtaani ,basi kama sangare ni mwanae anaweza akaibuka na utajiri kama alivyokuwa akimiliki mali itambu.
Mtemi aliondoka.zake na kumwacha issa akitaja minal mke wangu minal lazima nikuoe.

Tukirudi kwa akina mariamu ndipo waliweza kuingia pamoja na sangare ambae ni mtoto wake,mariamu alipiga magoti ili kuomba msamaha asamehewa na sangare
Ila sangare alimkataza nankumwambia "kama nimekuja singida na nimekupata basi tambua moyoni nishakusamehe 
Ila mama naomba uniambie  baba yaangu yuko wapi?

Mariamu ama mama yake na sangare alimtizama mwanae kisha akadondosha machozi na kumwambia " sangare mwanangu
Baada ya babu yangu kuuliwa pamoja na bibi yangu basi mali za ukoo wetu ambao unaitwa itambu ,zilichukuliwa na ukoo wa jobwe pamoja na mtemi,
Baada ya hapo sikupata msaada tena maana baba yangu na mama kama nilivyokuambia walikuwa wanaugua ugonjwa wa ukoma sikuruhusiwa kuwagusa maana wangeniambukiza.
Baba yako alikuwa ni mmiliki wa baa moja ambayo ilikuwa ipo  maeneo ya ukonga banana.
Mama yako nilikuwa na maisha ya shida jiji la dar na kazi zangu nilikuwa nauza baa,na kipindi hicho kama hutambuliki ili upate kazi lazima utoe mwili ili..

Mariamu kabla hajamalizia kuelezea nje palisikika mngurumo mkali ukinguruma ,mariamu aliwahi na kumsukuma mwanae chini kisha akamwambia lala chini na ziba masikio ,ukizubaa unakua kiziwi ziba masikio

Sangare akawa haelewi  alitizama mlangoni alishangaa kumwona minal amesimama mlangoni akiwa anawaangalia ,sangare aliziba masikio pamoja na mama yake nae akaziba masikio ,mngurumo ulizidi kuongezeka  ulikuwa ukinguruma kwa sauti kali mno.
Ulichukua dakika mbili baada ya hapo ule mngurumo uliisha,sangare alimuuliza mama kwani huo mngurumo wa nini na kwanini umeniambia nilale chini nizibe masikio.

Mariamu aliinuka na kusema hichi ndio kijiji cha mtamaa kina maajabu huo mngurumo ni wajabali lile ambao linafungukaga na kutema tope ,kwasasa limenguruma mwezi wa tisa linaashiria mwaka unaokuja utakuwa mwaka waneema ,mazao tukilima yatatoka vizuri.
Ooh sangare aliuliza sasa kwanini ulisema nilale chini na nizibe masikio?
Mariamu alimtizama mwanae na kumwmbia ,kwa mara nyingine ukisikia tuu huu mngurumo lala chini na ziba masikio ,ukikaa ama kusimama ,kuna hewa hupita  chini usawa wa magoti kuelekea juu,
Hio hewa ni mbaya sana ikipita kwenye masikio yako ,unakuwa kiziwi kabisa masikio yako masaa yote yanaweze kuwa yanatoa damu ama usaha 
Hivyo ukilala ile hewa haiwezi kupenya kwenye masikio yako na haiwezi kukuzuru,

Sangare aliuliza kwahio kwamfano nisinge lala ningekuwa kiziwi na masikio yangu yangekuwa yanatoa damu au usaha ?mariamu alijibu ndio,
Sangare alinyoosha mkono mahali amesimama minal nje na kusema mbona minal hajalala na yuko sawa?au inachukua muda gani,

Mariamu kwa hofu aliinuka na kusema yuko wapi,mungu wangu tayari masikio yake yashaharibika ule mngurumo ni hatari sana,ile mariamu anachungulia nje alishangaa mariamu analiga ukunga aiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!kisha akadondoka na kushika masikio yake ,sangare na mama yake wakawahi nje kumwangalia minal ,ndipo walijionea masikio ya minal yakitoa damu.

Sangare alimuuliza mama yake kwahio tunamsaidiaje?
Mariamu alijibu angekuwa anatoka usaha tungemtafutia dawa ,ila anatoka damu basi hatosikia tena,maisha yake yote

Njoo inbox kwa hizi namba 0621302436,kwa mahitajai ya hii story ,inapatikana full ,maanzo hadi mwishoni kwa bei nafuu
Nicheki whatsapp kupitia hio namba hapo juu.

JE NINI KITAENDELEA?
KUISAPOTI HII STORY NISAIDIE KUSHARE ILI NIZIDI KUIPOST KILA SIKU,USISAHAU KU COMMENT

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

إرسال تعليق

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.