MUUZ MAZIW EP 10*
MWISHOOOOOOOOO
Wazo la kuingia kabatini lilikuja tena kichwani kwa muuza maziwa, na Penina bila kuchelewa akaufunga mlango wakabati hilo.
“Penina fungua mlango”
alijua labda mwizi huyo amemteka mdogo wake.
Upande wa lisa alizidi kuchanganyikiwa.
Sauti ya Jerry ilisikika tena huku akizidi kuugonga gonga mlango kwa nguvu, akilini mwake “Fungua Penin…..”
Jerry alikatiza kauli hiyo baada ya Penina kufungua mlango.
“yuko wapi, yuko wapi huyo mwizi?’”
Jerry aliuliza huku akiwa ameishika Bastora yake sawia , tayari kwa kufyatua risasi.
“hapana kaka!”
“hapana nini kakimbia eeh au kaificha?”
“sio mwizi kaka!’
“sio mwizi!? ,nani? Na yuko wapi?”
Aliuliza kwa mshangao.
“Ni ndoto nilikuwa naota “
“Ndoto!!?”
“ndio kaka!”
“ooh! Jamani penina umetushtua wenzako , uuh!”
Aliongea Lisa na kuvuta pumzi , kwani wasi wasi ulimtoka baada ya kusikia kama ni ndoto.
“Penina unauhakika kama ni ndoto!”
Jerry aliuliza huku akiliangalia kabati, kasha akaanza kulisogelea taratibu.
“ndio ! Ndio! Kaka”
Penina aliitikia kwa hofu , alihisi kwamba pengine Jerry amegundua kitu, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Lisa ambae alichanganyikiwa kabisa.
“hapana siwezi kurihusu jambo hili hata kidogo”
Aliwaza Lisa pale Jerry aliponyoosha mkono ili kushika kitasa cha kabati hilo., alimkimbilia haraka.
“Honey umekwisha elezwa kwamba ni ndoto kwanini unapoteza muda , twende tukalale mpenzi mwenzako nimechoka>“
Lisa aliongea kwa sauti laini.
“Hapana nataka kufunga vizuri hili kabati”.
Aliongea Jerry huku akilisukumiza kabati, hakujua kwamba halijajifunga vizuri kwa sababu kuna mtu ndani.
Alilisukumiza huku muuza maziwa akisikilizia maumivu ya kuminywa na kabati hilo, alijuzuia kupiga kelele huku mwili mzima akitetemeka kwa woga.
“Achana nalo hilo Dear kwanza kabati lenyewe hilo bovu.”
“bovu!!!”
“eeh bovu hata mimi wifi alinieleza’
Penina alidakia
“sasa kwanini hamjamuita Fundi?”
“usijali mpenzi nitamuita kesho, twende basi tukalale.”
Lisa aliongea kwa sauti nyororor ambayo ilimshawishi Jerry moja kwa moja.
“Lala salama Penina “
Aliaga
“sawa kaka “
Walitoka na kwenda chumbani kwao wakiwa wamekumbatiana.. Penina aliufunga mlango kwa furaha na kisha kwenda kulifungua kabati. Alikuwa na hamu kweli ya kuwa na Karani wake.
Karani ambae hadi wakati huo alikuwa akitetemeka kwa hofu, hakuamini kabisa kwamba ndani ya chumba hicho yumo yeye na Penina pekeyeo.
“kabla ya yote nikumbatie mpenzi!.“
Penina aliongea akiwa na tabasamu zito usoni kwake . Muuza maziwa hakusita kumkumbatia.
“siamini kabisa mpenzi!”
“hata mimi penina!”
“hivi umejuaje kwamba ninaishi hapa?”
Aliuliza penina akiamini kwamba kilichomleta muuza maziwa humo ni yeye.
“Nilikuona ulipokuwa unaingia”
Muuza maziwa alijibu, hakutaka kumweleza kwamba aliyemleta humo ni wifi yake.
“ndio maana nakupenda Karani!”
“hata mimi nakupenda!”
Karani nae akaitikia
Alimsogelea zaidi na kumbusu
‘mwaaaa!!!’
‘Mwaaa!!!’
Penina nae aliitikia busu hilo.
Muuza maziwa kama kawaida yake akaanza manjonjo yake, Penina alikwisha jua nini kinachofuata akaanza kujichekesha kwa kicheko cha kugunaguna.
“unajua nafanya kazi gani sasa?”
Muuza maziwa aliuliza
“sijui!”
Penina aliitikia
“Nauza maziwa!”
“aah kwa hiyo nikuite Muuza maziwa sio.”
“sawa sawa watu wote wananiita hivyohivyo.”
“haya basi muuza maziwa nataka unipe mambo”
“hapa ndio mahala pake, utapata ondoa hofu!”
Muuza maziwa aliitikia na kuanza kumtekenya Penina kwa ulimi wake. Penina alicheka kwa kicheko cha chinichini, mambo ya muuza maziwa yalimfanya akumbuke kipindi walipokuwa wote kule shule kipindi Karani ni mchunga ng’ombe lakini sasa yuko mjini na ni MUUZA MAZIWA.