Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MUUZA MAZIWA SEHEMU YA 09

MUUZA MAZIW EP 09
ILIPOISHIA…..
“kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1”
Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri.
Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa.
“mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!”
Aliongea Lisa kwa mshituko
“utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?”
Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa.
Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati.
“da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi”
Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi.
MUENDELEZO WAKE :
“kumbe wewe nan……….?”
Penina alijikuta anakatisha kauli yake baada ya kumuangalia vizuri muuza maziwa, hakuamini alichokiona alihisi kama vile yuko ndotoni.
“Karani!!!!”
Aliita Penina kwa mshangao huku akiwa ameduwaaa.
“Penina!!!”
Muuza maziwa nae aliita mara baada ya kumuangalia vizuri penina.
Wote walibaki wakishangaa huku wakiangaliana usoni, kumbukumbu zao zilirudi nyuma miaka miwili iliyopita.
Suji sekondari katika bweni la wasichana chumba namba ishirini na moja. Penina akiwa amelala kwenye kitanda cha dabodeka, ikiwa ni mara yake ya kwanza kulala ndani ya chumba hicho.
Sababu hiyo ilikuwa ni siku yake ya kwanza toka ahamie bwenini , mwanzo alikuwa akikaa kwenye nyumba ya mkuu wa shule.
Akiwa kitandani hapo alisikia mlio wa mluzi ukisikika kwa mbali karibu kabisa na dirishani sehemu ambapo alikuwa amelala.
“it ndizi time!” [ni muda wa ndizi]
Mwanafunzi mmoja aliongea kwa sauti ya kunon’gona kasha wenzake walicheka kwa sauti za chinichini. Penina hakuelewa chochote kilichoendelea.
Mwanafunzi mmoja aliamka na kwenda kufungua mlango. Watu wane wakiwa wamejitanda khanga waliingia ndani, Penina alizani watu hao ni wasichana. Aliduwaa pale walipotoa Khanga zao. Wote walikuwa ni wanaume.
Kila mmoja alienda kwenye kitanda chake waliongea lakini sauti zao zilikuwa za kunon’gona.
Penina alibaki ameduwaa tu asijue nini cha kufanya , katika chumba hicho ni yeye peke yake ndio alikuwa amelala peke yake. Alijaribu kuutafuta usingizi lakini alishindwa , vilio vya mahaba alivyokuwa akivisikia usiku huo vilimtesa kupita kiasi, alitamani na yeye lakini hakukuwa na mwanaume kwa ajili yake. Alibaki akijigaragazaga
ragaza tu kitandani kwake.
Mpaka kufikia saa kumi na nusu alfajiri wanaume walipoondoka bado yeye alikuwa hoi.
Mchna alimfuata maria na kumweleza shida yake.
“na wewe unataka ndizi?”
“mmh, mwenzangu manaake hali mbaya!”
“usihofu , nitamwelza Bakari akufanyie mpango”.
“nitafurahi kweli maanake we acha tu!”
Ahadi ya maria ilikuwa kweli , Penina aliteseka kwa siku moja tu , siku iliyofuata nae aliletewa ndizi yake. Ni hapo ndipo alipokutana naKarani mchunga n’gombe wa akina Bakari, ambae sas ndio muuza maziwa.
Karani alikuwa akimfikisha Penina mpaka basi jambo lililomfanya Penina ampende kupita kiasi, alimuahidi kwamba atakuwa nae milele lakini ajabu ghafla alitoweka. Alipomuuliza Bakari kuhusu swala hilo alimwambia hajui alikoelekea.
“nyumbani katoroka alafu ameiba baadhi ya nguo zangu , hafai kabisa yule jamaa.”
BakaRi aliongea kauli hiyo iliyomaliza kabisa nguvu za Penina. Alimpenda sana Karani na alitaka kuwa nae siku zote za maisha yake. Hakuelewa ataishi vipi bila kuwa nae.
“lakini usihofu Penina nimekuletea mwingine”
Bakari aliongea akiwa ametabasamu huku akishika bega la kijana mpya aliyekuja nae siku hiyo.
Penina alimwangalia kijana huyo kuanzia chini mpaka juu lakini hakuona hakuona cha kumlinganisha na Karani.
“Siitaji tena kama Karani hayupo basi “
Penina alijibu kwa dharau.
“Penina hata huyu yuko bomba tena mkali kuliko hata Kara….”
“Nimesema sitaki husikii”
Penina alifoka tena kwa sauti kubwa jambo ambalo liliwaogopesha wote, sababu lilikuwa ni jambo la hatari, hawakutaka kuendelea kumsemesha waliogopa angewasababishia msala kwa mlinzi endapo ataisikia sauti yake.
Siku iliyofuata Penina aliamua kuhama chumba hicho kwani hakuona raha tena ya kuwa ndani ya chumba hicho wakati Karani hayupo. Rafiki zake walimbembeleza asahau habari ya Karani na akubali kuwa na yule kijana mpya ili arudi kwenye kile chumba lakini yeye aliwakatalia katakata , hakuona mwanaume wa kumfananisha na Karani wake.
Wiki moja baada ya Penina kuhama ndani ya chumba hicho mlinzi alishtukia mlinzi alishtukia kila kitu . Aliwakamata wanaume wote wakiwa ndani ya kile chumba cha kina Maria na kasha wanafunzi wote waliokutwa ndani ya chumba hicho walifukuzwa shule.
Penina alikuwa ameponea chupuchupu, kama isingekuwa Karani kutoroka nyumbani kwa kina Bakari basi leo hata yeye angelikuwa miongoni mwao na Karani wake.
Wiki moja baada ya Penina kuhama ndani ya chumba hicho mlinzi alishtukia mlinzi alishtukia kila kitu . Aliwakamata wanaume wote wakiwa ndani ya kile chumba cha kina Maria na kasha wanafunzi wote waliokutwa ndani ya chumba hicho walifukuzwa shule.
Penina alikuwa ameponea chupuchupu, kama isingekuwa Karani kutoroka nyumbani kwa kina Bakari basi leo hata yeye angelikuw miongoni mwao na Karani wake.
Jambo hilo lilimfanya azidi kumpenda Karani na kujipa ahadi kwamba lazima siku moja atamtafute mahali popote duniani.. Ajabu leo anamkuta ndani ya chumba chake cha kulala.
Hakutaka kumuuliza amefikaje , iwe kweli amekuja kuiba au vyovyote alichofikiria sasa ni kumuokoa ili kaka yake asijue kwamba yumo humo.
“Ngo, ngo ngo”
Mlango uligongwa , Penina pamoja na Muuza maziwa walichanganyikiwa.
“Penina!, Penina! Fungua mlango usihofu nina Bastora!”
Kauli hiyo toka kwa Jerry ndio ilizidi kuwachanganya akili.
“Tafadhari niokoe Penina sitaki kufa leo!”
“Usihofu Karani nitafanya kila njia!”
Penina aliongea.
ITAENDELEA..

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.