Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MUUZA MAZIWA SEHEMU YA 08

*MUUZA MAZIW EP 08*
“nzuri tu kaka, shikamoo!”
Aliitikia Penina na kasha kumwamkia kaka yake
“marhaba mdogo wangu>“
Aliitikia salamu.
“Penine kanenepa kweli safari hii, shule imempenda kweli.”
Aliongea Lisa.
“hapana wifi!?”
Penina aliongea na kasha kucheka, ukweli ni kwamba kweli alikuwa amenenepa na kujengeka shepu kwa mahipsi na makalio yaliyo fungashika kiinye plus gwedegwede.
Waliongea mengi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja tena. Upande wa Lisa moyoni hakuwa na furaha hata kidogo, muda wote alifikiria jinsi ya kumtoa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo.
Alifahamu fika jinsi swala hilo lilivyokuwa gumu kwani chumba alichomficha ndicho chumba atakacholala penina , hakuelewa angeweza vipi kumtoa muuza maziwa katika chumba hicho bila ya Penina kugundua.
“sijui nitafanya nini mungu wangu?”
Aliwaza bila kupata jawabu, hakuona aibu kumshikilikisha Mungu katika uovu wake.
“atalala tu lakini , na hivi alivyochoka, na huo ndio utakuwa muda muafaka”
Alizidi kuwaza,
Hiyo ndio ilikuwa njia pekee aliyoitegemea alitumaini Penina atakapolala ndio uwe muda muafaka.
“wifi vipi mbona utafikiri uko mbali sana!?”
Penina aliuliza baada ya kugundua kwamba Lisa hayupo pamoja nao katika maongezi.
“hapana nipo , mbona tupo pamoja!.“
Aliitikia Lisa haraka haraka baada ya kuzinduka toka kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo.
“kweli Lisa upo tofauti sana leo”
Jerry nae alikazi
“hapana jamani mbona nipo sawa!”
Lisa alizidi kujitetea kwa nguvu zake zote kwani hakutaka mtu yoyote ahisi chochote kuhusiana na swala hilo la muuza maziwa, alichokifanya baada ya hapo ni kujaribu kujichekesha na kuonyesha kuwa ana furaha ili kupoteza kabisa hisia za mumewe pamoja na wifi yake.
Waliongea kutwa nzima mpaka usiku ukaingia , baada ya chakula cha usiku kila mmoja alielekea chumbani kulala Jerry na mkewe chumbani kwao na Penina pia alielekea chumbani kwake.
Wakiwa kitandani kwao si Jerry wala mkewe aliyeonekana kumjali mwenzake, kila mmoja aligeukia upande wake , kila mmoja alirizika na usaliti alioufanya mchana wa siku hiyo. Jerry alipotembea na Sekritari wake wakati Lisa alipotembea na muuza maziwa.
Hakuna aliyejua maovu ya mwenzie kila mmoja alimuona mwenzake karanga bao na kumlalia mzungu wa nne.
xxxxx- – – – xxxxxx—- – — xxxxxxxx
Saa sita na nusu usiku Penina alishtuka toka usingizini , hii ni baada ya kusikia mlio wa kabati likifunguliwa , haraka alisogeza mkono wake kwenye swich ya taa na kuiwasha. Mwanga ulitanda chumba kizima . Penina hakuamini alipomuona mtu akiwa amesimama karibu kabisa na kabati huku kabati likiwa wazi.
“kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1”
Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri.
Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa.
“mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!”
Aliongea Lisa kwa mshituko
“utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?”
Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa.
Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati.
“da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi”
Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi.
ITAENDELEA

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.