Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MAPENZI YA KICHAWI SEHEMU YA 05

SIMULIZI;MAPENZI YA KICHAWI.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.
SMS;0621047841.

SEHEMU YA TANO ( 5 )

ILIPOISHIA.......

Nilimjibu Mtu yule huku nikianza kutetemeka kwani nilianza kujuta taratibu kwa dhambi nazozifanya kwa wakati mmoja ila hatimaye nilisema "POTELEA MBALI"
Mtu yule aliniambia muda umefika wa kunirudisha duniani tena atanirudisha pale pale nilipokuwa nakunywa damu ya Mama ili niendelee na hatua nyingine nazotakiwa kufanya.
Ghafla kimbunga kikali kilikuja na kunichukua bila ya kujua kinanipeleka wapi.
Itaendelea...........

ENDELEA NAYO.......

Kwa muda mchache nilijikuta tayari nipo pale pale nilipokuwa huku nikiendelea kunywa damu ya Mama niliyokuwa nimeiweka kwenye sufuria.
Niliitua sufuria chini kisha nikausogeza upanga wangu pembeni uliokuwa chini huku ukiwa umetapakaa damu,kisha pole pole nikaanza kuvua mavazi ya mwili wa Mama ambao kwa wakati huo tayari alikuwa ameshapoteza maisha,nilifanikiwa kuutoa nguo zote na kuuwacha kama ulivyozaliwa.
Hatimaye nilichukua upanga wangu uliokuwa mkali kuliko maelezo kisha nikaanza kwa kuutumbukiza kwenye mwili wa Mama huku nikiendelea kuzunguka sehemu za siri za Mama,nilifanya hivyo kwa kutumia nguvu nyingi mpaka nikajikuta sehemu za siri za Mama zinachomoka na kuacha shimo maeneo ambayo sehemu hizo zilikuwepo.
Mwanga hafifu wa asubuhi ulianza kuchomoza kwani muda nao ulizidi kwenda,sikutaka kupoteza hata dakika hivyo niliingia ndani chapu chapu huku nikiacha sehemu za siri za Mama zikiwa nje,nikiwa ndani nilichukua kimfuko cheusi pamoja na jembe kisha nikatoka navyo nje.
Niliusogeza mwili wa Mama pembeni kisha nikaanza kuchimba shimo kubwa eneo lile kwa ajili ya kumzika Mama,sehemu ile haikuwa ngumu hivyo nilitumia muda mchache mpaka nikajikuta nimechimba kimo kirefu kitakachoniwezesha kumzika Mama bila ya tatizo lolote.
Harakati za kuendelea kuchimba shimo hilo zilifika tamati,hivyo nikaamua kuubeba mwili wa Mama ambao kwa muda huo tayari ulikuwa umeshatapakaa damu.Niliitumbukiza mwili huo katika shimo hilo kisha nikaanza kuufukia kwa haraka zaidi.
Nilivyomaliza kuufikia Mwili huo,nilianza kwa kushindilia eneo lile kwa kutumia miguu yangu ili mtu yoyote asipate kufahamu eneo hilo lilitokea tukio gani.Damu iliyokuwa imebakia kwenye sufuria pamoja na sehemu za siri za Mama ambazo tayari nilikuwa nimeshaziweka ndani ya mfuko ule mweusi niliyokuwa nimeufuata ndani pia na jembe,vyote hivyo niliingia navyo ndani na kuacha eneo hilo la nje huku likiwa safi zaidi.
Wakati nikiwa tayari niko ndani huku nikiendelea kukaribishwa na sauti za jogoo waliondelea kuwika na kunifanya niamini kumekucha,nilipiga hatua za kuelekea kitandani kwangu kisha nikaketi kwa kuanza kuvuta taswira ya Mama pamoja na matendo mazuri aliokuwa ananifanyia kila siku.
Moyo wangu ulianza kufadhaika kwa kuhofia kukosa upendo kama wa Mama milele,nilianza kudondosha chozi pasipo sababu.Ikiwa chanzo ni kumkumbuka Mama.
Mwili wangu ulikuwa umetapakaa damu,hapo ndipo lilipokuja wazo la kuusafisha,kabla sijatoka nje kwa ajili ya kwenda kuchota maji ya kuoga,nilikumbuka kuhusu kuvihifadhi vitu hivyo vya siri ikiwa ni sufuria la damu ya Mama pamoja na sehemu zake za siri.Nilivihifadhi mahali salama kisha nikatoka nje huku nikiwa nimeshikilia ndoo yangu na kuelekea kisimani moja kwa moja.


Hakika nilianza kutawaliwa na mawazo zaidi juu ya Mama yangu mzazi,Mama niliyempenda na kumdhamini zaidi.
"Mama kwanini nakuwaza ,nakufikiria, naomba unitoke katika akili yangu naomba husinipe mawazo yoyote yale yanayokuhusu..."
Nilizungumza kwa hasira na jazba ya hali ya juu maana ilikuwa kama kero akilini mwangu kwani nilishindwa kufanya kitu chochote kile yote sababu mawazo ya Mama yalianza kunijia bila ya kujua sababu ilikuwa nini.
Niliweka ndoo chini kisha nikafungua kisima na kuanza kuvuta maji.Nilivyohakikisha ndoo hiyo imejaa maji niliibeba na kuelekea bafuni.
Kwakuwa kulikuwa hakujakucha vizuri na kulikuwa kuna kagiza giza fulani hivi,hivyo sikuwa na hofu zaidi kwa watu kuniona jinsi nilivyotapakaa damu,niliingia bafuni kisha nikaanza kuvua nguo zangu kwa lengo la kuoga.
"Mama yangu.....!!!!"
Nilishtuka zaidi baada ya kuona sura ya Mama ikiwa ndani ya ndoo yangu ya maji,sikutaka kupiga kelele wala hata kukimbia ila niliendelea kuyakodolea maji yangu na kutokuamini kilichokuwa kinaendelea,ghafla sura ya Mama ilipotea kwenye yale maji kisha maji yakabadilika na kuwa damu.
Yote hayo nilijiua ni mauzauza ya kawaida hivyo bila ya kuogopa chochote nilianza kuoga maji yale yaliyokuwa yamebadilika na kuwa damu....
"Mama,nakufa nakufa nakufaaaaa,nisaidieni....."
Nilianza kupiga kelele kwa kusikia maumivu makali mwilini mwangu kwani ngozi yangu ilianza kubanduka kutoka katika mwili wangu na kunifanya nianze kutokwa na damu kila sehemu ya mwili wangu.
Itaendelea.........


About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.