Notification texts go here Contact Us Buy Now!

HALIMA SEHEMU YA 01

HALIMA

                             SEHEMU YA   1

                              WHATSAPP 0655585220

...Darasa lilijaa vioja hata pale mwalimu alipoingia bado tu kuna baadhi ya wanafunzi walikua wanaendeleza kero..ilikua ni muda wa mapuunziko saa nne asubuhi..wadada wawili warembo kila mmoja alikua akimshinda mwenzake.Lakini Halima alikua ni nzuri kupita kiasi..msichana huyu alijaaliwa kuwa na kila sifa ya mwanamke nzuri..pili alikua anaringa kwa sababu ya hela iliyokua nyumbani kwaoo kwani baba yake alikua na hela si mchezo....Chaajabu wasichana hao wawili walikua wakizozana kila wakati...mwisho wanakuwa marafiki ..hali hii iliwaletea watu mshangao na maswali magumu yalio kosa maji...
    Mimi na wewe mwisho leo..urafiki wetu umeishia hapa ..Alisikika Halima akipaza sauti kumuambia Asia...Asialikua ni msichampole na  mwenye fahamu nyingi shuleni..ingawa kisura hakubahatika kuwa na sura ya kirembo bali alikua ni mtu wa kawaida tu..mwanamke huyu mbali na uhodari darasani bali alibahatika kuwa na umbo no 8 .hakuwa mjeuri ..alikua ni mkarimu na mpole..
   Ivi wewe Halima unaringa na kunisumbua au kwa sababu ya utajiri wa baba yako.ASIA alijibu mapigo..
    Chaajabu baada ya ugomvi unakuta watu hawa ni marafiki..ilishangaza sana tabia hii..
   Wakati wamasomo uliwadia...kengele ya kuingilia madarasani....wanafunzi waliingia madarasani ..Asia na Halima kama kawa walienda kukaa dawati moja la nyuma karibu na dawati fulani ambalo hukaa mvulana mmoja ..siku hiyo mwalimu wa kipindi ilikua anaingia na kwabahati ilikua ni somo la physics ambalo wanafunzi wengi ilikua hawalipendi..
    Good afternoon madam...ilikua ni saut ya wanafunzi walokua wanamuamkia mwali huyo wa kike.
   Good after ..fine....sit down..mwalimu aliwaamrisha wanafunzi wakae kitako huku akionesha  nupo sirias. hataki mchezo.
   thank u teacher...wanafunzi walijibu...
     Mwalimu alianza kwa introduction fupi mada ilikua ni density....baada ya muda aliwa omba buku ili ajue wanafunzi wake wamefikia wapi kwani yeye ilikua ndio mara yake ya kwanza kuingia kidato cha kwanza A.aligundua kwamba wanafunzi wengi wa darasa hilo hawapendi physics...
   Ok to day I want tu discus about. Archimedes' Principle: ...mwalimu alianzisha mada hiyo..
  wanafunzi wote kimwahuku wakionesha kuchoshwa na somo hilo....
   State Archimedes' Principle: mwalimu aliuliza huku akitegemea jibu zuri..lakini kwa mshanga watu wote kimyaaaa...lakini kabla ya kuuliza tena aliona ishara ya kidole juu ktk benchi ya nyuma karibu na akina Asia na Halima.
   Ok good...mwalimu ali furahi na kumuamrisha mwanafunzi alonyanyua mkono anyanyuke ili ajibu..kibaya zaidi mwalimu yule ambaye kiumri ni kati ya miaka 26 au 27.ambae alikua na sifa ya kupendeza na kuvutia alitoa ahadi ya zawadi kwa atakae jibu.
  Alinyanyuka kwa upole na utanashati...jina anaitwa Hassan ..umri wake ni miaka 18 nimtanshati handsame boy wa nguvu...ingawa kwao alikua ni masikini na bahati mbaya alizaliwa nje ya ndoa yaani mama yake alitembea na mwanaume njee ya ndoa na kumpata mtoto huyo..hivyo basi alikua analelewa ktk mazingira magumu hivyo basi aliamua kuweka mbele masomo kuliko chochote kile..
    Alianza kujibu huku akionesha kutikua na wasiwasi na alichoulizwa....
If the weight of the water displaced is less than the weight of the object, the object will sink

Otherwise the object will float, with the weight of the water displaced equal to the weight of the object.
 Wanafunzi wote hawakuamini kwamba angeweza kujibu kwa weledi kiasi kile...na sio wanafunzi tu bali hata mwalimu alibaki mdomo wazi kwa mshangaoo...alijikuta akisema safi sana mpendwa wangu..
   mmmmmmwah Hassan alijikuta akipata busu zito kutoka kwa Halima mwanafunzi nzuri kuliko wote katika shule hiyo...
   Wanafunzi wote darasani ...mwalimu...na hata Halima yeye mwenyewe hakuamini kilichotokea ...walibaki katika mshangaooo...
   Weee Halima ndio unafanya nini hivyo...mwalimu alimstua Halima aliye kua kazama katika mdomo wa Hassan ..
    Kwa hasira mwalimu alitoka na kumtaka Halima afike ofisini kwa waalimu mara moja..
   Lakini huku akiondoka mwalimu huyo tayari moyo wake ulisha ganda katka upendo na mahaba juu ya Hassan...alionesha ishara ya moyoni mwake kwamba anampenda kimapenzi Hassan.alitamani awe kipenzi chake cha moyo...suala jee wanafunzi wakijua haitokua aibu.na jee waalimu wenzake wakijua jee haitokua soo..kwakweli alikua katika wakati mgumu sana ....
   Upande mwengine nyuma yake alikuwepo Halima ambaye na yeye alionesha kuvutiwa na Hassan juu ya uhodari wake huo...ingawa alikua hodari lakini Hassan vilevile alikua hand some boy...Halima alijisemea kimoyomoyo ..
  "Lolote liwalo naliwe lakini kijana yule lazima awe wangu sijali mwalimu wala nani...lakini ilikuaje mimi nikafanya vile..alijikuta na mambo mawili kwa wakati mmoja ..anajipa moyo huku anajilaumu...dah ilikua shida kweli.
   Waalimu leo sikuamini macho yangu wakati nasomesha kunakijana kajibu suali lililokua likionekana gumu..lakini baada ya kujibu tu huyubibi kanyanyuka bila haya na aibu kaenda kumpiga busu la mdomo huyo mwanafunzi..ilikua ni mwalimu bi  Aisha akitoa mashtaka yake ofisini akimshtaki Halima.
   Waalimu wote walipatwa na mshangao...
kesi iliendelea na mwisho Halima aliomba msamaha..na kusamehewa...lakini zaidi alietoa  wazo la msamaha ni Mwalimu Abdul ambae moyo wake tayari ulisha tekwa na uzuri wa Halima...
    Jamani hii ni mara ya mwanzo na kwa vile ameomba msamaha haina budi tukamsamehe...mwalimu Abdull alizidi kuomba Halima asamehewe..
    Mwisho wote kwa pamoja waliamua kumsamehe Halima...
    Halima aliruhusiwa atoke ofisini ..ingawa mwalimi bi Aisha hakuridhika na msamaha juu ya Halima...
      Wakati anatoka ofisi  Halima tayari alishakua nje alisikia sauti za watu wawili zikimwita..Hebu subiri hapo... ilikua ni sauti ya mwalimu Abduli...lakini na Nyengine ilikua ni sauti ya mwalimu bi Aisha...
   jeee mwalimu Abdull alitaka kumwambia nini Halima..?
  jee na mwalimu bi Aisha alikusudia kumwambia nini Halima..?
  na vipi Hassan alikichukuliaje kilicho tokea darasani..

  ENDELEA KUFATILIA HADITH HII HAPAPA MWANZO MPAKA MWISHO........!!!!! 🏃🏃

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.