Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA SEHEMU YA 06

Barua iliyowahi Kuniumiza
Mtunzi. Yona Fundi
0675278759

SEHEMU YA SITA.

    Siku ambayo barua ya Tina ilivyonipotea katika mazingira ya ajabu huku nyumbani kwangu nikikaribishwa na harufu ya moshi wa gari. Ndani nikipokelewa na hali ya tofauti sana. Jambo lile lilinitia shaka, taratibu niliuendea mlango wangu, lakini safari hii haukuwa umefunguliwa, hata nilipofungua ndani hakuna kitu kilichoonekana kuchukuliwa wala kupekuliwa. Nilitumia muda mwingi kuhakikisha mambo yanakaa vyema.  

  Hofu ilinitawala sana nili lala kwa mashaka katika usiku wa siku hiyo. Saa kumi na moja alfajili usingizi uliniisha. Tafakari nzito ikanipitia, nilimkumbuka Tina katika namna nyingine.

  Haraka nilijitoa kitandani na kuiwasha taa yangu kisha  nikaanza kupambana na miguu yangu kuelekea mahali nilipokuwa nimezihifadhi barua nyingi ambazo Tina aliwahi kunitumia. 
   Mikono yangu haikuchelewa kutoka na shehena za barua ambazo niliwahi kutumiwa na Tina.  
 Taaratibu nilivuta kiti changu, macho yangu yakaanza kupambana na mwandiko wa Tina katika barua moja wapo. Maandishi yale yalinikumbusha mbali sana, yalinikumbusha viapo kadhaa wa kadhaa ambavyo niliviweka kwa Tina wangu. Huku taratibu nikionesha umwamba wa kupambana na machozi yalioanza kunitiririka kwenye uso wangu. 

   Ghafla kilio kilichochanganyika na kwikwi za hapa na pale kilinitawala. Nililia kwa sababu ya mapenzi. Japo nilikuwa shujaa wa kushindana na kazi ngumu lakini sasa mapenzi yalionekana kunizidi ujanja. Na kuniweka katika hali ya tofauti sana. Kama kuna mtu angekuwa anakisikia kilio changu hakika angeniona mtu wa ajabu sana. Mwanaume niliyeweza kuyavumilia maisha magumu leo hii natoa kilio cha kizembe kisa mapenzi. 
Mikono yangu ilishindwa kuendelea kushikilia barua zile, maandishi yake yalionekana kunisurubu pasina mategemeo. Kuepusha yote nilizikusanya barua zile na kuelekea nje, huko kukanipokea. Hali ya utulivu iliyokuwa nje ilinisaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha zoezi ya kuzichoma moto barua zile. 

  Nilirejea ndani na kujibwaga kitandani, usingizi haukuchelewa kunichukua. Nili lala kama mfu. Saa nne, jua likichukua utawala wake kwenye uso wa dunia ndipo nilipopata nafasi ya kuamka.
 Nikaichukuwa simu yangu. 
Hamadi!

  Ile na angalia kioo cha simu yangu, nilikutana na simu kadhaa ambazo sikuwa nimezipokea, nilipotazama jina la mpigaji, hakuwa mwingine bali Muhando. Huku nikikutana na ujumbe mmoja wa kunihitaji kufika nyumbani kwake.
________      
  Nusu saa nilikuwa ndani ya daladala kuelekea Kimara baruti, mahali ilipo nyumba ya Muhando. Hakunichukua muda mwingi, tayari nilifika nyumbani kwa Muhando. Chai nzito ya maziwa ikawa inasindikiza mazungumzo yetu. Nilimuelezea kwa urefu yale yalikuwa yakinisibu tangu pale nilipoipokea barua ya Tina. 

 Hakuna alichonishauri zaidi ya kuniomba nilifuatilie jambo lile kwa kina wala nisilifumbie macho. Akisisitiza huenda kuna jambo limejificha ndani yake na lingeweza kunisabishia madhara kwenye maisha yangu katika muda wowote. Jambo la kwanza aliniambia niende polisi kutoa taarifa.

Naam, nilitii na siku iliyofuata, nilitoa taarifa polisi. Baada ya kulipeleka swala lile polisi, ni kama hawakunielewa. Hapo nikaamua kujiongeza mwenyewe katika kulifuatilia swala lile. 

 Siku ya tatu, baada ya kuzitoa taarifa polisi. Mchana nilikuwa ndani ya basi kuelekea Morogoro nyumbani kwa kina Tina. Sikuipata shida sana kama safari yangu ya kwanza. Japo ulikuwa umepita muda mwingi lakini kumbukumbu zangu hazikunipotea. Masaa matatu basi lilinishusha Mikese, hali ilionekana kubadilika sana, palikuwa pamechangamka sana. Huku nikikaribishwa na pikipiki chache pamoja na baiskeli nyingi kama usafiri wa kuelekea kwa mama yake Tina. Kwa kuwa nilikuwa niliingia jioni, nilitafuta nyumba ya wageni hata hivyo sikuchelewa kuipata.
**********

   Jioni mwili wangu nikaulaza juu ya kitanda cha nyumba ya wageni. Wakati mwili wangu ulipokuwa juu ya kitanda akili yangu ilikuwa mbali na pale. Nilikuwa nikimfikiria mama yake na Tina. Ni majibu gani ambayo yangefaa kuniridhisha kwa kile nilichoenda kukikatafuta, huku kumbukumbu ya majibu yake ya miaka kadhaa iliyopita kuhusu mahali alipo Tina ikiniijia. Nilikumbuka vyema hakuwa akifahamu mahali alipo Tina kwa wakati ule. Lakini moyo wangu ulikuwa mgumu kuamini mpaka sasa. Ni vipi Tina ashindwe kuwapa taarifa wazazi wake sehemu alipokuwa akiishi na huyo mumewe. Hilo niliona haliwezakani. Nikajipa moyo lazima mama yake na Tina atakuwa akifahamu mahali ambapo Tina anaishi.

  Nililala na maswali mengi ambayo si kuwa na majibu yake. Nikitegemea kesho ningeweza kupata majibu ya maswali yangu.
Mapema asubuhi ya siku hiyo, nilijitoa eneo lile na kuelekea sehemu ambapo ningepata usafiri wa kuelekea kwa kina Tina. Kwa vile sikuwa mgeni, sasa nilimuelekeza kijana aliyekuwa akiendesha pikipiki. Mwendo wa dakika arobaini na tano. Nilikuwa nikitazama na nyumba ya Mzee kobero baba yake na Tina.
   Hapakuwa pamebadilika sana. Hata macho yangu yalikiri kuwa sikuwa nimepotea, nilikuwa eneo sahihi kabisa. 
Lakini usahihi ulionekana kupotea baada ya kukaribishwa na wenyeji wa eneo lile. Sura ngeni zilinipokea, salamu za ukaribisho wangu zilichukua nafasi kabla ya kuelezea shida yangu. Ajabu maneno yalikuwa yakipenya kwenye ngoma za masikio yangu. Nilihisi kama niko ndotoni lakini yule mama alikuwa sahihi kwa kile alichokuawa anakiongea, yakuwa Mzee kobero alihama eneo lile na sasa alielekea kijiji cha pili mbali kidogo na eneo lile. 

   Nilimuliza yule mama kama anapafahamu mahali alipohamia Mzee kobero, majibu yake yalinipa matumaini. Nikamuomba anipatie kijana wake ambaye alionekana kupafahamu. Hapo kidogo ulikuwa mtihani lakini ulimalizwa na pesa kidogo. Dakika kadhaa nilikuwa juu ya usafiri wa pikipiki mimi na yule dereva na kijana mdogo aliyekuwa akituongoza kuelekea kwa Mzee Kobero.
Nusu saa pekee tuliitumia na sasa tulifika nyumbani kwa mzee Kobero. Sura ya mama yake Tina ilinipokea katika mtazamo wa tofauti sana. Alionekana kuchukizwa na ujio wangu. Nilijitahidi kupambana na hali ile niliyokuwa nikiiona. Na kwa bahati nzuri Mzee Kobero nilikutana nae, yeye kidogo alionekana kuwa katika hali ya kawaida. 
Baada ya kumalizana na dereva wa pikipiki, huku nikizinakili namba zake kwa ajili ya kunifuata pindi nitapomaliza kilichonipeleka, nilimuomba amrejeshe nyumbani kwao kijana aliyetuongoza.
__________ 

  Sasa nikawa mwenyeji, kwa ufupi sana niliwaeleza dhumuni la kuwa eneo lile tangu hapo na mara ya mwisho kukanyaga ardhi ya Morogoro. Nilichukuwa dakika kama kumi kutawala mazungumzo, kabla ya mama yake Tina kuchukua nafasi ya kuzungumza huku mimi na Mzee Kobero tukiwa wasikilizaji. Alizungumza kwa upole zaidi, maneno yake yakionekana kushindwa uvumilivu wake. Sasa mimi niligeuka mbembelezaji wa kilio cha mama yake na baba yake. Vilio vyao vikiniacha na sintofahamu.

Je nini kitaendelea? 

Angalia filamu yangu mpya! Bonyeza link hii kuitazama.

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.