Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA SEHEMU YA 05

Barua Iliyowahi Kuniumiza
Mtunzi. Yona Fundi
0675278759

SEHEMU YA TANO.

     Ujumbe ulikuwa muhimu mara mbili kuliko nilivyo kuwa nikidhani. Barua ya Tina sasa ilinitesa haswa. Namba za ajabu, upotevu wa barua zilizidi kuniongezea maumivu kwenye kichwa changu, huku udadisi wangu ukikosa kuambulia jibu lenye tija. Cha kushangaza ujumbe ule ulitafsiri mambo yote yaliyopita kipindi kifupi cha nyuma na umuhimu wa ile barua japo kwa uchache. Ni mimi Tina huu ujumbe wangu wa mwisho kwako Emanueli, naona umeyapuuza maombi yangu. Maneno yale yalijirudia rudia machoni mwangu na kuniweka kwenye tafakari nzito, nikijiuliza. Nimepuuzia ombi lipi kutoka kwa Tina?
  Barua ile ilikuwa ya muhimu sana. Huku ikionekana kubeba mambo nyeti. Lakini hakuna ambacho kilionekana kunipa matumaini ya kufahamu kilichomo ndani ya barua ile, ikiniweka katika wakati mgumu zaidi. Mikono yangu haikuchelewa kushika jasho, nikajikuta nikitetemeka mwili mzima.
 
   Fikra mbaya zilinipitia kuhusu habari za watu wengi wanaofanya kazi za madini. Fikra ambazo nilizihusisha ni pamoja na utoaji wa kafara kwa watu wa namna hiyo, ili kujihakikishia kazi zao zinaenda sawa. Nilihisi huenda Tina kuna jambo baya ambalo anaenda kutendewa ama tayari ametendewa na mwanaume wake, ambaye nilifahamu kuwa anajishughulisha na biashara za madini. 

   Naam! Dakika tano tu nilikuwa mbali kimawazo, huku nikitiririkwa na jasho mwili mzima. Mungu wangu weeh! Muepueshe Tina wangu Maneno yakanitoka bila hata kujielewa. Ghafla nikakikanya kichwa changu, kutomuwazia mabaya Tina mtoto wa Mzee Kobero.
************

  Nilijitoa kitandani nikiwa nimetawalia na hofu, taratibu nikaelekea bafuni kuoga. Wakati huo giza lilianza kuchukuwa nafasi kuukaribisha usiku wa siku hiyo. Nilipomaliza kuoga, niliona jambo lile nimshirikishe bosi Muhando, maana lilianza kunitafuna taratibu na hata kupoteza uchangamfu wangu.

   Simu ya Muhando iliita kwa muda mfupi kisha kupokelewa. Maongezi hayakuchukuwa dakika nyingi. Nilimueleza juu ya shida yangu ya kutaka kuonana nae ili kuzungumza nae jambo fulani. Muhando alionekana kutia shaka, lakini nilimweleza kwa kifupi tu kuwa haikuwa shida ya ofisi bali binafsi. Kwa hekima na busara bosi Muhando akanikubalia ombi langu la kwenda kuzungumza nae siku itayofuata, bila kujua nini kingeenda kutokea asubuhi ya siku hiyo. 
   Ilikuwa kama kutua mzigo mzito; kitendo cha kuikata simu nilivuta pumzi ndefu sana. Hakika nilitawalia na hofu pasipo kutegemea. Mwili wangu ulionekana kukosa nguvu kabisa. Miguu yote ilikosa nguvu, huku kichwa kikionekana kushindwa kuubeba mwili. 
  Njaa kali nayo ikaanza kulisumbua tumbo langu, likionekana dhahiri kudai kodi yake ya siku. 
Nilitoka nyumbani kueleka katika mgahawa mmoja ambao haukuwa mbali sana na nyumba yangu. Nukta kadhaa nilikuwa na tazamana nao. Nilijitoma ndani nikaketi, mhudumu hakuchelewa kunipokea. Haraka nikaagiza chakula nilichoona kinanifaa. Zilipita dakika chache nikaanza kupambana na shehena ya wali iliyokuwa kwenye sahani ya wastani.
_______ 
  Nilijitoa eneo lile baada ya kupata huduma iliyoridhisha tumbo langu. Si kuchelewa kufika nyumbani kwangu, saa tatu kamili ilikuwa imetimia. Kutokana na mawazo mengi ambayo yaliendelea kukinyanyasa kichwa changu, usingizi nao haukuonekana kuja mapema kwa siku hiyo kwasababu nililala sana jioni yake. Niliona ni vyema kujiliwaza kwa kuangalia luninga yangu huku nikitafakari ni jinsi gani nitayaweka matatizo yangu kwa bosi Muhando, iliniweze kupata walau tumaini la kujitoa katika jambo ambalo liliendelea kunitesa siku hadi siku. 

 Usiku huo ulikuwa wa tofauti kidogo mpaka inatimia saa saba usiku bado si kuwa nimeupata usingizi, na hata nilipokuja kupitiwa na usingizi ndoto mbaya ilinipitia huku ikiniacha na maswali mengi kichwani mwangu. 

  Ni kama vile nilikuwa nikifahamu jambo fulani lililokuwa likitokea mbali na pale kwa maana asubuhi ya kuamkia siku hiyo. Nilizipokea habari mbaya kwenye ngoma za masikio yangu, punde tu nilipoipokea simu ya bosi Muhando ambayo ilinitoa kwenye lindi la usingizi. 
 Taarifa zile hazikuwa za kawaida, ingawa bosi Muhando aliziongea kwa shida sana lakini nilizielewa. Nilimsihi awe mvumilivu katika kipindi chote kile, ambacho wazi nilifahamu kuwa mama yake mzazi alikuwa amepoteza maisha ghafla kutokana na ugonjwa aliyokuwa nao. Hali ilikuwa tete zaidi hapo sasa mambo yangu nikayaweka pembeni kwa ajili ya kishughulikia msiba uliyomkabili bosi wangu. 
________
   Mwezi mzima hali haikuwa nzuri sana kwa bosi Muhando, nilitumia nguvu kubwa kuhakikisha Muhando anarudi katika hali niliyoizoea. Hatimaye baada ya mwezi na nusu Muhando alirejea katika hali yake ya kawaida.          
 Ndani ya mwezi wa pili, baada ya kumaliza habari za msiba wa mama yake Muhando. Katika jioni moja niliweza kupata fursa ya kuongea na Muhando, mambo ambayo yalikuwa ya kinisibu. Habari za mama kunihitaji kuoa, niliiweka ya kwanza katika mazungumzo yetu. Nilimweleza namna gani moyo wangu ulivyokuwa mgumu kuingia katika ndoa. Huku nikikosa chaguo sahihi la mwanamke wa aina gani ambaye angefaa wazi kuwa mke wangu. 
 Safari hii bosi Muhando alikuwa tofauti sana ni kama vile nae alikuwa upande wa mama, kwa maana alishikilia msimamo wa mama wa mimi kuoa. Si kuweza kubishana na maneno yake, kwa maana nilimuelewa sana na mara kadhaa maneno yake huwa ni dawa kwangu. Hivyo nae nilimtoa shaka katika lile. 
Baada ya kuliweka sawa jambo lile, kilichofata nilimuomba kunipatia likizo ya mwezi mmoja iliniweze kulishughulikia swala lile. Ombi halikuwa na ugumu pasipo mategemeo Muhando aliamua kunipatia likizo. 

Siku ya pili tu baada ya kuianza likizo yangu, mambo yalikuwa tofauti sana. Niliporejea nyumbani kutokea mahali fulani, nilipoenda kufatilia mambo yangu. Harufu ya moshi wa gari ilinikaribisha nyumbani kwangu. Nani huyo amefika nyumbani kwangu? Swali lilinipitia na kunijengea mashaka, haraka niliamua kutoa simu yangu kumtafuta bosi Muhando kwa kudhani huenda alikuja nyumbani. Simu ilipokelewa majibu yake yalinitia hofu kabisa na kunirudisha nyuma katika miezi kadhaa. 

Itaendelea!

Nb. Unaweza kusikiliza simulizi zetu kwa njia ya sauti kwa kubinya link hii. 
https://youtu.be/FevpnWqMdSc
 
Usisahau Vitabu vyetu Vya Makoroboi, Kafara vinapatikana nchi nzima, uliza kwa muuza Vitabu yoyote.  Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa 0675278759

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.