Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA SEHEMU YA 03

Barua iliyowahi kuniumiza
Na Yona Fundi
0675278759

SEHEMU YA TATU.

        Ugonjwa wa kulikosa penzi lake ukanijia. Miezi sita iliyofuata sikuipokea tena salamu wala taarifa iliyomuhusu. Nini kilimkumba Tina wangu? Ukabaki mtihani kwangu. 
Wazo la kuzitafuta pesa kwa bidii na kuzitunza likanijia. Nikazitafuta pesa nia na madhumuni kwenda Morogoro wa ajili ya kumtafuta ingawa sikufahamu sehemu halisi haswa ambayo ningeweza kumpata.
Nilichokuwa ninakumbuka ni kwamba; Tina aliwahi kuniambia kuwa, sehemu waliyokuwa wakienda ilifahamika kwa jina la Mikese.

   Kwakuwa sikuwa mwenyeji wa Morogoro, kitu cha kwanza nilianza kuzitafuta habari zilizohusu mkoa huo. Baada ya takribani siku mbili nilifanikiwa kupafahamu huko kijijini Mikese. 

  Hata nilipopata pesa kwa ajili ya safari na zile za kujikimu ndani ya safari, sikuwa na tabu. Hivyo katika jioni moja nilipanda basi kwa miadi ya kufika, ni lale hapo ili asubuhi ya kuamkia siku hiyo nianze kumtafuta Tina.
___________ 
Safari ya Morogoro haikuwa fupi masaa matatu nilikaa kwenye kiti cha basi. Tukiwa njiani kukaribia Morogoro mjini, tuliweza kukutana na kijiji fulani na hapo konda akanifahamisha kuwa, sehemu hiyo ndo inaitwa Mikese. 
 Akamtaarifu dereva kisha gari likasimamishwa, nilishuka na kukaribishwa na hali ya hewa ya kijiji hicho cha Mikese.  Hata nilipotembea kidogo niliweza kuwaona vijana kadhaa wakiwa wamekaa kwenye gogo moja ambalo lilikuwa chini ya mti mkubwa. Nikawafuata kisha nikaomba wanipatie msaada wa wapi naweza pata nyumba kwa ajili ya wageni.
        Broo, hapa hatupo kwa ajili ya kupoteza muda. Majibu yao yakanishangaza kidogo.
       Mnamaana gani kusema hivyo?
       Tangu lini shida zikatatuliwa burebure?
        Hapo nikawaelewa, nikaingiza mkono wangu mfukoni na kutoa kiasi kidogo cha pesa kisha nikampatia mmoja wao.
Hapo sawa, Akafurahi kisha akaongeza, Unataka gesti zenye kunguni ama gesti safi?
Hapo akaniacha hoi kidogo, lakini kwakuwa sikuhitaji shida nikajibu,  Gesti safi.

  Oooh! Hapa umefika. Akaongeza Oyaa, washkaji eh! Wachanimuwahishe bosi wangu akapumzike. Aliwaaga wenzie kisha tukaondoka eneo lile.
Aliniongoza hadi kwenye moja kati ya nyumba za kulala wageni. Haikuwa mbali na pale, dakika tano nilikuwa nazungumza na mhudumu wa eneo lile. Nililipia pesa ya chumba kisha nikapatiwa ufunguo na namba ya chumba. Ingawa chumba kile kilikuwa cha kawaida sana, lakini kilifaa kunipa hifadhi kwa usiku huo.
_______________
   Usiku wa siku hiyo ulikatika na asubuhi kuingia. Niliamka na kuanza safari ya kumtafuta Tina wangu. Hakika nisingeweza kumpata Tina endapo ningetumia jina lake, lakini baada ya kulikumbuka jina la mzee Kobero, hapo hata sikupata ugumu wowote ule. Dakika kadhaa nilikuwa juu ya usafiri wa baiskeli kuelekea nyumbani kwake.
   Ili tuchukua kama masaa mawili, sasa nikawa na tazamana na nyumba ya mzee Kobero. Nilikaribishwa na mama Tina ingawa alionekana kunisahau, lakini baada ya muda na maneno machache ya awali kumbukumbu ikamjia.
   Tulizungumza mambo mengi sana kabla ya kuelezea dhumuni la ujio wangu.  
      Aliongea kwa basara sana mama yake na Tina, hakusita kugusia upendo uliyokuwepo kati yangu na mwanae.
      Nikweli, mimi na Tina tunapendana sana, lakini mbona simuoni Tina hapa? Nilishanga sana baada ya kumwona mama Tina amebadili sura na kutengeneza sikitiko. Hakuwa na jinsi, hapo ilibidi anieleze ukweli tu, kwamba; Tina wangu tayari alikwishaolewa miezi kadhaa iliyopita, muoaji akiwa ni Tajiri mmoja aliyejihusisha na biashara za madini. Hata hivyo kwa muda huo wazazi wa Tina hawakuwa wakijua ni wapi mtoto wao alikuwa akiishi kwani, mwanzoni aliishi Morogoro lakini baada ya hapo alihama yeye na mumewe bila hata taarifa.
      Maneno ya mama Tina yalikuwa kama msumari ndani ya moyo wangu, yalinichoma vilivyo, yote ni kutokana upendo wa kweli niliyokuwa nao kwa Tina wangu. 
Nilimlalamikia Mungu kwa kuyafanya maisha yangu kuwa katika mirija ya kushindwa kumudu kuishi na Tina. Pengine ndio ilikuwa sababu ya kumkosa Tina. Nilitambua wazi Tina alikuwa akinipenda ila umasikini ndio sababu ya kumkosa Tina wangu.
_________ 
Safari ya kurejea jijini Dar es salam ilikuwa kama mzigo kwangu. Nilijihisi naenda kuchanganyikwa katika siku zijazo. Mapenzi yalinifanya vile yanavyojua nikibaki natapatapa. Niliichukia dunia. Manzese Midizini niliiona kubwa. Nilihisi nimeibeba mgongoni na sasa ilikuwa ikielekea kunishinda.
 Wiki nzima nilikuwa ndani nikiyaugulia maumivu ya Tina.
____________
   Mlio wa simu yangu, ndio ulinitoa kwenye usingizi, nikiwa taabani. Usingizi uliyochangiwa na kupitiwa kumbukumbu ya Tina. Hakuwa mwingine, zaidi ya bosi Muhando. Nikaipokea simu yake huku nikiweka umakini wa kuyapokea majukumu. Sikutaka kumueleza swala lililonitokea jana usiku, nilijua wazi huenda ingempa mawazo na kutilia shaka ufanisi wangu katika kuyakabili majukumu aliyoniachia. Tulizungumza kwa dakika tano kisha nikaipata nafasi ya kwenda kujiandaa kuelekea kazini.
Nusu saa nilikuwa njiani. Nilipita kituo cha polisi kama walivyonitaka usiku wa jana. Hapo sikupata shida, nilifika na kisha nikaanza kuchukuliwa maelezo.  
    Niliwaelezea kiufupi kile ninachohisi juu ya tukio lile. Walinisikiliza kwa umakini huku wakiyaweka maelezo yangu kwenye maandishi. Waliniuliza juu ya upotevu wowote wa mali, niliwajibu hakuna kilichokuwa kimepotea. Sikutaka kuweka wazi juu ya upotevu wa barua niliyotumiwa na Tina. Nilihisi wangeniona mzembe sana. Baada ya kuwaridhisha, waliniruhusu, hapo nikaelekea kazini.
***********
Niliyatimiza majukumu ya kazi ipasavyo. Mapema jioni nikarejea nyumbani. Nikiwa nyumbani, mara simu yangu iliita, nikapokea simu ya Mama yangu.
Ni kawaida yake mama kuongelea swala la kuoa, hivyo maongezi yake nilikuwa nimeshayazoea. 
Hata hivyo aliulalamikia umri wake na kusema, angependa kumtia mjukuu wake mikononi kabla uhai wake haujamtoka. Maneno ya mama ingawa nilikuwa nimeyazoea lakini siku hiyo ni kama yalidhamiria kuniumiza zaidi. Si kwamba nilikuwa sihitaji kuoa bali niliona hakuna mwanamke ambaye angeweza kuwa kama Tina wangu. 
Japo alikuwa ameshaolewa miaka kadhaa iliyopita lakini bado alikuwa ndani ya akili yangu. 
   Kitendo cha Tina kunitumia barua siku iliyopita kiliniweka katika mtazamo mwingine. Kila nikikumbuka kuwa, barua yake ilipotea katika hali ya kutatanisha, nilibaki na mawazo mengi sana, zaidi simu ya mama ilinichanganya pia. 
  Sikuwa na hiyana, nilimuomba mama anipatie miezi michache ya kujianda ilikumpata mwenza wa kufunga nae ndoa na hatimaye hata kunizalia mtoto ili moyo wa mama upate kufarijika.
     Nilimpenda mama yangu, aliishi nami kwa tabu sana, tangu kufariki kwa baba yeye ndio alibaki kuwa msaada wangu. Alinipambania hata kunipeleka shule kuufuta ujinga wa kutojua kusoma wala kuandika. Hivyo sikupenda kumwona akijisikia vibaya kwa ajili yangu. Na kipindi cha sasa sikuwa na cha kujitetea uwezo wa kukaa na mwanamke nilikuwa nao. Tofauti na zamani ambako ningeweza kuusingizia ugumu wa maisha.
________
Usiku wa siku hiyo, nilipokea ujumbe kwenye namba yangu ya simu, ulinishangaza kidogo. Ujumbe ambao ulikuwa umetoka kwenye namba binafsi (private number). 
    Ujumbe ulionesha mtumaji ni Tina, akiuliza kama niliipata barua yake. Ilinishangaza mno. Ni vipi Tina amepata namba yangu? Nilishikwa na bumbuwazi. Nikaviona vidole vyangu vizito kujibu ujumbe ule. Niliogopa kudanganya. Kwa sababu sikuwa muumini wa uongo. 
Wakati nataka kufanya mawasiliano na namba ile japo niweze kusema kile nilichokuwa nataka kukiongea. Nikakakumbuka kuwa ile ni namba binafsi. Hivyo uwezekano wa kufanya mawasiliano ulikuwa haupo. Niliishiwa nguvu, pumzi nilizivuta kwa tabu sana. Nini kimemsibu Tina wangu? Na nini alichokiandika Tina? Ulibaki mtihani usiyokuwa na majibu. Nilijikuta nikijitupa juu ya kitanda.

Inaendelea unaweza ifatilia yuotube kwa kubinya link hii chini..

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.