Notification texts go here Contact Us Buy Now!

BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA SEHEMU YA 02

BARUA ILIYOWAHI KUNIUMIZA
Mtunzi. Yona Fundi
0657477902

SEHEMU YA PILI.
  
      Nilihisi kijasho chembamba kikinitoka. Macho yangu yakiwa yanatazamana vyema na maandishi yaliyo juu ya bahasha, iliyokuwa imetunza barua.
Nililiendea feni na kuiwasha kwa ajili ya kupunguza joto, lakini haikusaidia kitu. Hofu ilinitawala huku ujasiri wangu ukinikimbia na kuelekea kusikojulikana. Maandishi yalikuwa ya kuogofya. Wasiwasi uliambatana na mchafuko wa tumbo, kitendo kilichonifanya nitengeneze urafiki na msalani bila hiyari yangu. Nilipiga safari zaidi ya nne kabla ya tumbo kukaa sawa. 

Hata niliporejea ndani, simu yangu haikuchelewa kuita, nikaitazama nakugundua kumbe mpigaji alikuwa bosi wangu bwana Alfa Muhando. Nilitamani kutoipokea kwani bosi wangu ni mtu asiyeheshimu muda wa mapumziko kwa mwenzie, linapokuja suala la kazi huwa radhi hata kukutoa usingizini.  Hata hivyo sikuwa na sababu za msingi za kumchukia maana ni yeye aliyenitoa kwenye ajira ya kupata elfu saba kwa siku hadi kufikia laki sita kwa mwezi na posho za kila siku nje ya mshahara, kitendo kilichonifanya kutafuta nyumba ya haja na kukikimbia kile kibanda changu kule Mazense na kuhamia Kimara Mbezi, niliko jenga nyumba yangu kwa ajili ya kujihifadhi.
    
   Ninakusubiri huku tulipokuwa juzi, wahi kuna jambo la dharura limejitokeza. Sauti ya bosi wangu ilisikika ikisema hivyo. Hapo nikawa sina jinsi, swala la barua nikalisahau kwa muda na kukisaliti kitanda changu usiku huo. Ndani ya muda tayari nilikuwa sehemu aliyonitaka niende, nikitazamana na sura yake.
  Hatukuchukuwa muda sana tayari tulikuwa ndani mazungumzo ya kikazi. Naam, ilikuwa ni lazima mimi niwe pale maana bosi wangu alihitaji kuniachia majukumu ya kikazi kwakuwa yeye alitakiwa kuelekea Iringa kwa ajili ya kwenda kumuona mama yake ambaye ilisemekana afya yake haikuwa nzuri. Nilipoyapokea majukumu, niliondoka na kurejea nyumbani kwangu.
  
  Nilipoyafikia mazingira ya nyumba yangu, kulikuwa na tofauti sana pua zangu zilikaribishwa na harufu ya moshi wa gari. 
Nani huyu aliyekuja na gari hapa? Swali hilo lilikipitia kichwa changu. Jibu nikalikosa maana mtu pekee ambaye hujakunitazama nyumbani kwangu na gari ni bosi Muhando. Hata hivyo kumbukumbu zilinikumbusha kuwa, bosi Muhando nilikuwa nae masaa machache yaliyopita. Sikutaka kujali sana, nikaichukuwa miguu yangu kuufuata mlango wa nyumba yangu. Nilijikuta nikistaajabu, ati kufuri hakuna? Huku nikijiuliza, mbona wakati naelekea kuonana na bosi niliacha nimeufunga mlango wangu na kufuri?

 Hapo hofu ikanizidi na nikajuawazi lazima kuna jambo limetokea. Nikajipa ujasiri na kuongeza umakini kisha nikaingia ndani. 
 Hata nilipoingia ndani nilikuta chumba changu kikiwa ovyo tofauti na vile nilivyokiacha. Nilijaribu kutafuta labda kuna mtu anaweza kuwa kajificha pahala, lakini sikufanikiwa. Ukimya wa chumba changu ulinifanya niamini kuwa, hakuna yeyote aliye ndani isipokuwa mimi . 
  Nikahisi huenda kuna majizi yatakuwa yamekivamia chumba changu wakati nimetoka, akili ikanituma niangaze vitu vyangu vya muhimu, ajabu hakuna hata kimoja kilichoonekana kuchukuliwa. 
 Mungu wangu? Mwizi wa namna gani huyu? Na nini amefuata humu ndani?... Nilijiuliza maswali mengi ambayo hata sikuyapatia majibu yake. Hapo wazo la kutoa taarifa polisi likanijia. Haraka nikachukuwa simu yangu na kubofya namba ambazo zinazohusiana na polisi, nikapiga. Hawakuchelewa, dakika kadhaa mbele walikuwa nyumbani kwangu, wakafanya uchunguzi wao. Baada ya kujiridhisha walitimua zao huku wakiacha wamenitaarifu kuwa, siku inayofuata ni ripoti kituoni kwa ajili ya maelezo ya ziada.

Mpaka saa tano na nusu juu ya alama, nilikuwa bado ndani ya kukurukakara za kuhakikisha naweka kila kitu kilichokuwa kimevurugika katika hali yake ya kawaida. Ingawa vitu vyote vilionekana ajabu sikuiona bahasha ambayo ndani mwake ndimo ilimokuwa barua ya Tina. Hapo kichwa kikaniuma zaidi, nikajisemea,Huenda itakuwa imeanguka chini ya uvungu. Hata nilipoitafuta bado sikuipata.  Sikutaka kuamini kama imepotea katika mazingira yale, lakini baada ya muda ilinibidi nikubaliane na matokeo. Barua ile ikawa imepotea ilihali hata sijajua inazungumzia nini.

    Baada ya muda niliamua kujipumzisha, hapo usingizi haukuchelewa kunichukuwa na kunipeleka mahala kwingine, kwani nilikuwa nimechoka sana.
________    
 Tina alinipenda mno, alinipenda kwa maana ya kupenda. Ilikuwa kama bahati kumpata msichana wa aina yake. Kipindi hicho moyo wangu, ulishaanza kupona na majeraha ya mapenzi; majeraha niliyopatiwa na wasichana tofauti tofauti ambao sikudumu nao katika mapenzi kutokana na ufukara wangu. 
  Mpendwa msomaji; mazoea kati yangu pamoja Tina yalianza taratibu sana tena kwenye mgahawa uliopo nyumbani kwao, nikiwa kama mteja, nae akiwa kama muhudumu. 
     Tangu nilipoujua mgahawa wao ni kama nililogwanao, sikuwahi kuacha kwenda hata siku moja, mpaka nilipompata ndipo nikapunguza kwenda mgahawani. 

  Hakika Tina aliurejeshea matumaini moyo uliyopoteza imani na mapenzi; alijua kunivumilia, hakuhitaji pesa kama wanawake wengine. Kila kukicha alisisitiza kauli yake kwamba, hakupenda pesa bali penzi langu. Nakiri maneno ya Tina, kuwa hakuzifata pesa kweli maana uzuri wake uliwachanganya vibosile wengi lakini hawakupata nafasi ndani ya moyo wake. Hivyo nami niliamua kumwonyesha mapenzi ya dhati.
*********
   Tina hakuwahi hata siku moja kutamka kutoka kinywani mwake kwamba, Emanueli sikuhitaji labda ingeleta maziko ya pendo lake ndani ya moyo wangu. 
 Penzi langu kwake lilingia katika mtihani mzito. Mtihani ulisababishwa na ugumu wa maisha uliyokuwa ndani ya familia yao. Kabla ya macho yangu kumpoteza nakumbuka aliwahi niambia, nakupenda sana Emanuel wangu lakini nasikitika kuwa muda mchache nitakuwa mbali nawe. Hakika maneno yake yaliniumiza sana.
 
*********
  Ugumu wa maisha ndiyo uliyompelekea mzee Kobero kulihama jiji la Dar es salaam na kurejea Morogoro. Kwa kipindi hicho nilitamani sana walau waondoke wazazi wa Tina pekee na yeye abaki nami, lakini sikuweza kutokana na kipato changu kuwa kidogo nisingeweza kumudu kuishi nae.

Ingawa nilikuwa mbali na upeo wa macho ya Tina lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kutowasiliana nae.  Alinitumia barua mbalimbali, nilizipokea nami nilimtumia za kwangu. Nilizifurahi sana barua zake kwani ndizo zilizokuwa zikiondoa upweke wangu. 

      Niliendelea kupambana na maisha iliniweze kuikamilisha ile ahadi yetu ya kuja ishi pamoja kama mke na mume.
Barua za Tina zilikuwa sababu kubwa yakunihamasisha pindi nilipotamani kukata tamaa. Hakika hakuwahi kunifanya nijihisi mpweke hata kidogo. Mapenzi ya umbali yalidumu kwa muda wa miezi tisa, kilichofuata hapo ndugu kilibadili maisha yangu katika namna ya ajabu sana.

Je nini kitaendelea?
Unaeweza sikiliza simulizi kwa njia ya sauti bonyeza link hii chini. 

Usisahau vitabu vyetu vya Makoroboi, Kafara, vinaptikana nchi nzima...
Wasiliana nasi namba ziko juu hapo..

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Chapisha Maoni

Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.