Notification texts go here Contact Us Buy Now!

MAPISHI YA KUPIKA ROSTI YA MBUZI

*ROSTI YA MBUZI NA VIUNGO MBALIMBALI*

ROSTI YA MBUZI

MAHITAJI YA KUPIKA ROSTI YA MBUZI
  • *Kwa nyama*
  • 500g/ nusu kg nyama ya mbuzi
  • ½ limao
  • Vijiko 1½ vya chakula majani ya kotimiri au
  • giligilani
  • Vijiko 1½ vya chakula majani ya mnanaa
  • Vijiko 1 vya chakula kitunguu saumu
  • Kijiko 1 cha chakula tangawizi ya unga
  • ¼ kikombe mafuta ya mzaituni (olive oil)
  • Chumvi kwa kuonja
  • Viungo vya rosti
  • Viazi ulaya vya wastani 3-4
  • Nyanya 2
  • Kitunguu 1 kikubwa
  • Kijiko 1 cha chai kitunguu saumu
  • Vijiko 2 vya chakula nyanya ya kopo
  • Pilipili kichaa 1
  • Vijiko 2 vya chakula mafuta ya samli au mafuta ya kupikia
  • ½ kikombe vitunguu vya majani
  • ¾ kijiko cha chai tangawizi ya unga (au fresh)
  • Jani la bay 1 ( bay leaf )
  • Karafuu punje 3
  • Iliki 3
  • Kijiko 1 cha chai giligilani ya unga (coriander powder)
  • Kipande cha mdalasini
  • Kijiko 1 cha chai garam masala
  • Chumvi kwa kuonja

JINSI YA KUPIKA ROSTI YA MBUZI

  1. Andaa viungo vya marinate; Katakata majani ya kotmiri au majani ya giligilani; kamua limao; twanga kitunguu saumu
  2. Kwenye bakuli kubwa, changanya nyama na viungo vyote vya marinade vizuri. Funika bakuli, acha viungo vikolee kwa masaa kama manne au vizuri zaidi usiku kucha
  3. Andaa viungo vya rosti; katakata viazi roborobo; kata pilipili vipande virefu; twanga kitunguu saumu; katakata majani ya kitunguu vipande vyembamba, weka pembeni
  4. Weka nyanya na kitunguu katika mashine ya kusagia chakula kutengeneza rojo, weka pembeni
  5. Kwenye sufuria katika moto wa wastani, weka mafuta ya samli. Yakichemka ongeza kitunguu saumu na viungo vizimavizima; karafuu, iliki na mdalasini. Kaanga kwa dakika kama 2; au mpaka kitunguu saumu kiive vizuri
  6. Ongeza nyama iliyokuwa marinated. Kaanga kwa dakika kama 5, au mpaka iwe ya kahawia kiasi
  7. Ongeza jani la bay (bay leaf) rojo ya nyanya pamoja na viungo vikavu; giligilani ya unga, tangawizi ya unga na garam masala. Ongeza na chumvi kwa kuonja. Pika mpaka nyanya ziive vizuri kabisa
  8. Ongeza vikombe 2 maji. Funika na mfuniko, acha nyama iive moto wa chini kiasi kwa dakika 20 hadi 30; au mpaka ilainike kabisa na maji yaanze kukaukia
  9. Ongeza viazi. Pika mpaka viazi viive vizuri na sosi iwe nzito
  10. Ongeza majani ya kitunguu, pika kwa dakika 1 nyingine
  11. Pakua kama utakavyopenda
  12. Enjoy

About the Author

Hello,I am Web Designer and Expert facebooktwitteryoutubeinstagramexternal-link

Maoni 1

  1. Mchuzi Wa Nyama Ya Mbuzi Na Bamia
    Michuzi

    [img]http://www.alhidaaya.com/sw/UserFiles/Image/mapishi/Vitoweo%20na%20michuzi/Mchuzi%20wa%20mbuzi%20na%20bamia.jpg[/img]

    Vipimo

    Nyama ya mbuzi 2 Lb (Ratili)

    Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi 1 Kijiko cha supu

    Bamia Kiasi

    Pilipili mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha chai

    Vitunguu 2

    Nyanya iliyokatwa katwa 4

    Chumvi kiasi

    Garam masala 1 Kijiko cha supu

    Kotmiri ½ Kikombe

    Pilipili manga ½ Kijiko cha chai

    Nyanya ya kopo 3 Vijiko vya supu

    Ndimu 1

    Mafu…
Cookie Consent
We serve cookies on this site to analyze traffic, remember your preferences, and optimize your experience.
Oops!
It seems there is something wrong with your internet connection. Please connect to the internet and start browsing again.
AdBlock Detected!
We have detected that you are using adblocking plugin in your browser.
The revenue we earn by the advertisements is used to manage this website, we request you to whitelist our website in your adblocking plugin.
Site is Blocked
Sorry! This site is not available in your country.